Kwanini BRICS inavutia sana nchi za Afrika?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111445542478.jpg


Mkutano wa 15 wa wakuu wa nchi za BRICS utafanyika Johannesburg, Afrika Kusini kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwezi ujao. Ukiwa chini ya kaulimbiu ya "BRICS na Afrika: Ushirikiano wa Wenzi wa Ukuaji wa Kasi ya Pamoja, Maendeleo Endelevu na Utaratibu Shirikishi wa Pande Nyingi", mkutano huo utaangalia jinsi ya kukuza ushirikiano kati ya BRICS na nchi za Afrika ili kuleta maendeleo na ukuaji wa uchumi wa bara la Afrika.

Kwa mujibu wa serikali ya Afrika Kusini, mwenyeji wa zamu wa mkutano huo, viongozi wote wa nchi za Afrika wamealikwa kuhudhuria mkutano huo. Barani Afrika kuna nchi 55. Iwapo mialiko yote ikipokelewa, litakuwa tukio ambalo halijawahi kutokea katika historia ya BRICS.

Kinachofurahisha sio tu idadi ya viongozi wa Afrika ambao wanaweza kuhudhuria mkutano huo, bali wakati mkutano ukikaribia, nchi mbalimbali za Afrika, zikiwemo Misri, Ethiopia, Zimbabwe, Algeria, Nigeria, Sudan na Tunisia, zinatafuta namna ya kujiunga na kundi la BRICS. Mjumbe maalum wa Afrika Kusini kuhusu mambo ya BRICS Anil Sooklal hivi karibuni alidokeza kuwa zaidi ya nchi 30 kutoka Afrika, Amerika ya Kusini, Mashariki ya Kati na Ulaya Mashariki kwa njia rasmi au isiyo rasmi wametoa ombi la kutaka kuwa mwanachama wa familia ya BRICS.

Je, kwa nini nchi za BRICS zinavutia sana? Kwanza, nchi za BRICS zikiwa ni pamoja na China, Russia, India, Brazil na Afrika Kusini, idadi ya watu wake imechangia asilimia 42 ya watu wote duniani, na mchango wa BRICS kwa ukuaji wa uchumi wa dunia umezidi ule wa kundi la nchi tajiri G7 mwaka 2020, na hali hii itaendelea kuimarika. Shirika la Fedha la Kimataifa IMF linakiri kuwa ifikapo mwaka 2028, kiwango hicho cha BRICS kitafikia 33.6%, na G7 kitashuka hadi 27.8%, hivyo pengo hilo litaendelea kupanuka kadiri nchi nyingi zinavyokuwa BRICS. Wakati huo huo, takwimu za miaka ya hivi karibuni zimeonyesha kuwa kiwango cha biashara kati ya nchi na BRICS, haswa na China na India, kimekua kwa kasi. BRICS imezidi kuwa mshirika muhimu wa kibiashara wa nchi mbalimbali, hasa kama chanzo muhimu cha uagizaji bidhaa kutoka nje. Kutokana na sababu hizi halisi, nchi nyingi zimeomba kujiunga na BRICS "kwa kuzingatia mabadiliko ya nguvu za kimataifa ".

Pili, watu wanazidi kutoridhishwa na umwamba wa nchi za Magharibi katika mfumo wa fedha wa kimataifa, na nchi nyingi hasa za Afrika zimeanza kuiona BRICS kuwa ni fursa ya kujikwamua na amri za madola ya kimagharibi. Katika maeneo mengi, nchi za BRICS zinaweza kushirikiana na nchi za magharibi, lakini katika maeneo mengine, lazima zizingatie maslahi yao ya maendeleo, na kuwa na uamuzi huru wa kusema hapana kwa nchi za Magharibi. Kwa mfano, kutokana na matumizi mabaya ya umwamba wa dola za kimarekani, nchi nyingi za Afrika zimeamua kupunguza utegemezi wao kwa dola ya Marekani katika biashara zao za kimataifa baada ya kukumbwa na mfumuko mkubwa wa bei na msukosuko wa fedha. Moja ya ajenda zinazohimizwa hivi sasa na nchi za BRICS ni kuhamasisha matumizi ya sarafu za kienyeji katika biashara za kimataifa, au hata kubuni sarafu moja itakayochukua nafasi ya dola ya kimarekani.

Tatu, ni matarajio ya pamoja ya nchi za Afrika kujenga dunia iliyo na ncha nyingi badala ya kutawaliwa na nchi moja au mbili. Kwa muda mrefu, nchi zinazoendelea zimekuwa zikitengwa katika mchakato wa utandawazi, na matatizo ya nchi hizi hayajazingatiwa kama mambo muhimu katika mageuzi ya mfumo wa utawala duniani. Nchi za BRICS zinatoa njia mpya kwa nchi za Afrika kushirikiana na nchi nyingine za Kusini ambazo zina changamoto na mitazamo inayofanana, ili kuongeza ushawishi wa kimataifa, na kuhimiza mageuzi ya taasisi za kimataifa kama vile Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia.

Wakati nchi za Magharibi zinapounda "kikundi cha nchi zilizoendelea" na kushindwa kutekeleza ahadi zao kwa nchi zinazoendelea, nchi za BRICS zimekuwa shirika la kimataifa la pande nyingi linaloonyesha na kulinda maslahi ya nchi za Kusini. Nchi za Afrika zimeona matumaini kwenye BRICS na zina hamu ya kuwa mojawapo.
 
Back
Top Bottom