Mfumo wa BRICS+ wapongezwa na nchi za Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111450644579.jpg
Mkutano wa 15 wa viongozi wa nchi za BRICS unafanyika nchini Afrika Kusini, ambapo viongozi wanaohudhuria mkutano huo wanajadili kwa kina mada mbalimbali ikiwemo kuimarisha ushirikiano na kupanua mfumo wa BRICS kuwa BRICS+.

Afrika Kusini, ambayo ni nchi mwenyeji wa mkutano huo, imewaalika viongozi wa nchi zote za Afrika kushiriki katika mkutano huo. Kabla ya hapo, nchi nyingi za Afrika zikiwemo Misri, Ethiopia, Zimbabwe, Algeria, Nigeria, Sudan na Tunisia zimeeleza nia yao ya kujiunga na mfumo wa ushirikiano wa BRICS, na baadhi yao zimewasilisha maombi rasmi.

Katika miaka ya hivi karibuni, nchi za Afrika zimezidi kutoridhika na mfumo wa usimamizi wa mambo ya kimataifa unaodhibitiwa na nchi zilizoendelea za Magharibi, zikilalamikia zaidi mfumo wa kifedha wa kimataifa ulioanzishwa baada ya Vita ya Pili ya Dunia. Mamalalamiko yanatokana na kwamba, sheria za kimsingi za mfumo huo zimetungwa na nchi zilizoendelea kama vile Marekani na nchi za Ulaya, na zinapuuza sana maslahi ya nchi zinazoendelea. Takwimu zinaonesha kuwa, kati ya mikopo ya dola bilioni 650 zilizotolewa na IMF mwaka 2021, dola bilioni 160 zilikwenda kwa nchi za Umoja wa Ulaya, huku nchi za Afrika zikipata dola bilioni 34 tu.

Kulingana na idadi ya watu, mtu kutoka nchi tajiri za Umoja wa Ulaya alipata fedha karibu mara 13 kuliko mtu wa nchi maskini za Afrika. Zaidi ya hayo, nchi za Afrika zinalazimika kubeba gharama za mkopo ambazo ni mara 4 hadi 8 zaidi kuliko nchi zilizoendelea. Matokeo ya hali hii ni kwamba nchi tajiri zinazidi kutajirika huku nchi masikini zikizidi kuwa masikini, na ni vigumu kwao kutimiza maendeleo endelevu.

Kwa miaka mingi, nchi za Afrika zimekuwa zikitamani kuwepo kwa mfumo wenye nguvu wa nchi zinazoendelea ili kukabiliana na makandamizi ya nchi za magharibi, na sasa, mfumo wa ushirikiano wa BRICS umeleta matumaini. Mfumo huo ulianza mwaka 2006, na nchi wanachama wake zilichukua asilimia 26.46 ya ardhi yote ya dunia na asilimia 41.93 ya idadi ya watu duniani.

Mwaka 2021, jumla ya uchumi wa nchi tano za BRICS ilifikia takriban asilimia 25.24 ya jumla ya uchumi wa dunia, na kupita Kundi la Nchi 7 (G7) linaloongozwa na Marekani. Kiwango cha mchango wa nchi za BRICS katika ukuaji wa uchumi wa dunia umezidi asilimia 50 kwa miaka mingi mfululizo. Wakati huo huo, kutokana na maendeleo ya mfumo wa BRICS, mada ya kupanua mfumo huo imewekwa kwenye ajenda, na kujadiliwa kwa kina katika mkutano huo wa Afrika Kusini, na kuzipatia nchi za Afrika fursa ya kujiunga na mfumo huo.

BRICS+ imetoa njia mpya kwa Afrika, ambayo ni kwamba, kwa kushirikiana na nchi wanachama wa mfumo huo, ambazo zote pia ni nchi zinazoendelea, na kukabiliwa na changamoto sawa na zenye maoni mengi sawa kuhusu mambo ya kimataifa, zinaweza kupata misaada ya maendeleo na kuhimiza kuboresha usimamizi wa mambo ya kimataifa, ili kutimiza kihalisi maendeleo endelevu.
 
Kama BRICS ni binamu, mjomba, baba mdogo etc nitakubaliana nao. Vinginevyo what matters is economic interests za waanzishaji wa huo mfumo na siyo wanaounga mkono.

Kama 'United States of Africa' imetushinda, huko tunakoenda tunajisumbua tu? Hakuna msaada wowote, bali ni ku'endorse, masilahi ya hao BRICS na si ndugu zetu. Ila kwa vile tunataka misaada tutadhani tutaipata kutoka China, India na Russia etc. Tusubiri vya bure. Kuna stori moja ya Fr Anthony de Mello ameitumia kwenye kitabu chake nadhani kinaitwa "Song of the Bird". It goes: "A man walking through the forest saw a fox that had lost its legs and wondered how it lived. Then he saw a tiger come with game in its mouth. The tiger had his fill and left the rest for the fox. The next day too God sent the tiger to feed the fox. The man began to wonder at God’s greatness and thought. “I too shall lie in a corner trusting the Lord to give me all I need. ” He did this for a month, and was almost at death's door when he heard a voice that said, “O you who are on the path of error, open your eyes to the truth! Imitate the tiger, not the fox." Na mara nyingi sisi tuna'imitate' the fox and not the tiger. Shida iko hapo!
 
Wapuuzi hamzalishi chochote kujitosheleza, mtamuhitaji USA kununua vitu kwake muweze ku-survive, atawatoza kwa dola. CT Scan, MRI mtaipata wapi bila dola?

WAJINGA WANAKUTANA KUJADILI UJINGA NA WAKITOKA HAPO NI KUKUBALIANA KUTOKUBALIANA
Kila kitu kikubwa lazima kiwe na mwanzo changamoto hazikosekani

Brics wanajiamini,acha watatue matatizo yao,kama wao wanaona wanaweza,wewe iweje uwaite wajinga hawawezi?

Punguzeni ujuaji wa kijinga huo
 
Wapuuzi hamzalishi chochote kujitosheleza, mtamuhitaji USA kununua vitu kwake muweze ku-survive, atawatoza kwa dola. CT Scan, MRI mtaipata wapi bila dola?

WAJINGA WANAKUTANA KUJADILI UJINGA NA WAKITOKA HAPO NI KUKUBALIANA KUTOKUBALIANA

Unamawazo ya darasa la pili watu wako chuo.
mkuu izo nchi unazichukuliaje kwan mbona kama ujaona uwezo wao na nini wanacho
 
Wapuuzi hamzalishi chochote kujitosheleza, mtamuhitaji USA kununua vitu kwake muweze ku-survive, atawatoza kwa dola. CT Scan, MRI mtaipata wapi bila dola?

WAJINGA WANAKUTANA KUJADILI UJINGA NA WAKITOKA HAPO NI KUKUBALIANA KUTOKUBALIANA
Maliza kwanza stress na matatizo Yako ndo uweze kuja kuchangia haupo sawa au kama una mikopo kausha damu maliza kwanza hayo madeni nikupe hii Kwa kifupi kwamba Bidhaa tunazo tumia hasa developing countries Kwa maisha ya sasa ni zaidi ya 90% zinatoka BRICS eg mabasi mengi ni Chinese brand, vifaa vya umeme, spare parts, electronics etc vingi kutoka china na pia upande wa madawa iwe ya binadamu au pembejeo nyingi ni Chinese or indian brands ambazo ni kutoka BRICS
 
Na kitu kilichonishangaza zaidi ni Soud Arabia ilivyoweza kujiunga na Brics,yaani nchi iliyokua ikipendwa na USA kwa sababu za kiuchumi,Leo imehamia kambi nyingine.
Hili ni pigo kubwa sana kwa USA.
Pia china na pengine Urusi walicheza karata zao kwa akili sana,kwanza waliamza kuwapatanisha Iran na Soud Arabia,kisha wakaziingiza zote mbili,lkn moja ambayo imeiumiza sana USA ni kuachwa na mshirika wake kipenzi w middle east, Soud Arabia.
 
Mrusi na mchina wanahangaika sana, ni swala la muda tu wote watapoteana
Sasa hapa Urusi na uchina wanahangaika Nini ?
Mbona west Wana umoja wao wa G7 husemi wanahangaika?
Kwa hiyo hairuhusiwi kuunda umoja wa ushirikiano?

G7 Wana umoja wao na hawataki kualika nchi nyingine,Sasa hizi nchi nyingine zisianzishe umoja wao?
Haya kwa mfano wakipoteana hao Brics wewe mtanzania mwenzngu utafaidika na Nini?
Tuanzis na kwako TU wewe binafsi,utafaidika na Nini kwa Brics kupoteana?
 
Kila kitu kikubwa lazima kiwe na mwanzo changamoto hazikosekani

Brics wanajiamini,acha watatue matatizo yao,kama wao wanaona wanaweza,wewe iweje uwaite wajinga hawawezi?

Punguzeni ujuaji wa kijinga huo
Hii nchi ngumu sana hii.
Kuna watu nchi hii,wanajiona Wana akili sana kuliko raia wote wa nchi za Brics,wakati wananchi wa nchi za Brics wanafurahia umoja wao kwa ajili ya kutatua changamoto zao kama ulivyosema ila utakuta kijitanzania kinaponda.aisee nchi hii Ina maajabu yake.
Ila wakisikia umoja wa G7 wanaona kama umoja wa malaika hivi.
Ni utumwa,utumwa na utumwa wa kimawazo.
 
Wapuuzi hamzalishi chochote kujitosheleza, mtamuhitaji USA kununua vitu kwake muweze ku-survive, atawatoza kwa dola. CT Scan, MRI mtaipata wapi bila dola?

WAJINGA WANAKUTANA KUJADILI UJINGA NA WAKITOKA HAPO NI KUKUBALIANA KUTOKUBALIANA
Kwamba mchina na mrusi hawana uwezo wa kuunda hizo MRI na CT Scan? Au unafikiria kwa kutumia makalio? 😂
 
Back
Top Bottom