Kwanini baadhi ya watu hawali kitimoto?

Inasemwa kuwa eti mfalme mmoja aliekuwa na wake wawili wazuri alialika wageni nyumbani kwake. Akaagiza wachinjwe wanyama wa kila aina kutoka katika mifugo yake - mbuzi, ng'ombe, ngamia, kuku, bata, kondoo, nguruwe, nakadhalika.

Baada ya mapishi kuwa yamekamilika wake wa yule mfalme waligundua kuwa miongoni mwa mapishi yale, nyama ya nguruwe ndiyo ilikuwa tamu kuliko zote kule jikoni.

Basi mke mmoja miongoni mwa wake wa mfalme yule aliamua kwa makusudi kuificha ile nyama tamu ili baadae wageni watakapokuwa wamekwisha kuondoka akampakulie mumewe ale. Na kwa akili ya yule mama alidhani kwa kumfanyia hayo mfalme yeye (huyu mama) atapendwa zaidi kuliko wake wenza.

Baada ya wageni kuwa wamekula na kushiba hatimae muda wa kuaga kuondoka kurejea makwao ukafika. Wakaenda zao.

Basi yule mke wa mfalme aliyekuwa ameficha ile nyama tamu akaipakua na kumtengea mfalme. Huku na kule mfalme akahoji kulikoni nyama ile iletwe hali wageni washaondoka? Mke akasema aliona ni vyema aifiche kwa ajili ya mfalme ili ampende zaidi.

Mfalme akasusa kuila akasema yeye aliandaa karamu kwa ajili ya kula na wageni wake na si kula peke yake kiuchoyo. Basi mfalme akatangaza mbele ya mkewe yule kuwa nyama ile haili na kwamba chakula kile (kitimoto) ni haram.

Kumbe wote tunakula kitimoto ila tu wengine wanakula kwa kificho na wikiendi ndo hii. Hapa Euro pale sahani ya kitimoto
Ungeuliza kwa nini wengine hawali panya?(ukiwemo na wewe,mwenyewe),wakati wapo watu wanakula panya.
 
Kijana wacha ujinga, jiulize tu.....huyo Mungu alikushukia lini na kukukataza wewe kula nguruwe? Usipende kusikiliza hadithi zilizotungwa na watu kwenye vitabu kutishia wenzao, kama Mungu hataki wewe ule nguruwe, believe me atakushukia wewe na kukuonya ila HAWEZI kumshukia mzungu au mwarab na kuwaambia nenda kamuonye baby zu asile nguruwe. Tumia akili zako, dini ni usanii tu, zimewekwa kwa ajili ya kutawala binadamu na ndiyo maana unaona waumini wengi ni masikini na wajinga.
Wako watu wanakula,panya,nyoka,chura,mbwa,paka,majongoo,mafunza,mizoga iliyooza,nk.Wewe unakula hivyo?
 
Story za kutunga kutoka kwenye Quran
Hakuna story hiyo kwenye Qur'an ya mfalme.Wapo watu hawali panya,na wako wanaokula.Kuna watu hawali nyoka,na wapo wanaokula.Wapo wahali mende,na wapo wanaokula.Wapo wasiokula nyoka,jongoo,na wapo wanaokula,hao mbona hatuletei story zake,ilikuwaje wasile hizo nyama.
 
Nakula sasa hivi utanitapisha
Ndio ujuwe mleta mada, hana maarifa,sio nguruwe tu,wapo wanaokula na wapo wasiokula,hata Yesu,hakuna maandiko yalionyesha alikula nguruwe.Ikiwa mwenzako Hali kitu fulani,usiwe unaleta kashifa,wapo watu wanakula mpaka nyama za binadamu,lakini wapo ambao hawali.Lakini wanaokula nyama hizo,hawaleti story za kutunga,dhidi ya wasiokula.
 
Back
Top Bottom