Kwanini baadhi ya watu hawali kitimoto?

Inasemwa kuwa eti mfalme mmoja aliekuwa na wake wawili wazuri alialika wageni nyumbani kwake. Akaagiza wachinjwe wanyama wa kila aina kutoka katika mifugo yake - mbuzi, ng'ombe, ngamia, kuku, bata, kondoo, nguruwe, nakadhalika.

Baada ya mapishi kuwa yamekamilika wake wa yule mfalme waligundua kuwa miongoni mwa mapishi yale, nyama ya nguruwe ndiyo ilikuwa tamu kuliko zote kule jikoni.

Basi mke mmoja miongoni mwa wake wa mfalme yule aliamua kwa makusudi kuificha ile nyama tamu ili baadae wageni watakapokuwa wamekwisha kuondoka akampakulie mumewe ale. Na kwa akili ya yule mama alidhani kwa kumfanyia hayo mfalme yeye (huyu mama) atapendwa zaidi kuliko wake wenza.

Baada ya wageni kuwa wamekula na kushiba hatimae muda wa kuaga kuondoka kurejea makwao ukafika. Wakaenda zao.

Basi yule mke wa mfalme aliyekuwa ameficha ile nyama tamu akaipakua na kumtengea mfalme. Huku na kule mfalme akahoji kulikoni nyama ile iletwe hali wageni washaondoka? Mke akasema aliona ni vyema aifiche kwa ajili ya mfalme ili ampende zaidi.

Mfalme akasusa kuila akasema yeye aliandaa karamu kwa ajili ya kula na wageni wake na si kula peke yake kiuchoyo. Basi mfalme akatangaza mbele ya mkewe yule kuwa nyama ile haili na kwamba chakula kile (kitimoto) ni haram.

Kumbe wote tunakula kitimoto ila tu wengine wanakula kwa kificho na wikiendi ndo hii. Hapa Euro pale sahani ya kitimoto 😋
Asilimia 70 ya wanaosema hawali kiti moto hula pembeni...
 
Kiukweli hivyo vyakula vyote vinasubiri kwa kitimoto, labda kama hujawahi kuila hiyo kitu.. weka mbali na watoto hiyo nyama aisee+ kimea ndio kbsaa
Ngoja nimalize kazi za watu nikajilipue na huyu mdudu hapo Micasa
 
Ngoja nimalize kazi za watu nikajilipue na huyu mdudu hapo Micasa

Mimi mda huu nimetoka kuchukua kilo 3 buchani nataka niiandae mwenyewe ndio hua nainjoi zaidi. Mchana naipiga na ugali mkubwa sana inayobaki jioni inapigwa na ndizi rosti..😋😋 Bila kusahau coke baridi na altar wine
 
Mimi mda huu nimetoka kuchukua kilo 3 buchani nataka niiandae mwenyewe ndio hua nainjoi zaidi. Mchana naipiga na ugali mkubwa sana inayobaki jioni inapigwa na ndizi rosti.. Bila kusahau coke baridi na altar wine
Mkuu acha kunitamanisha basi ukizingatia haya makazi mpaka niyamalize ni saa kumi na moja

Na hii njaa nimeihifadhi kimakusudi kabisa
 
Jamaaa umetuzungushaa kumbe nyama ziko chini kama mtori
 
Back
Top Bottom