Kwanini baadhi ya watu hawali kitimoto?

inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
2,420
4,922
Inasemwa kuwa eti mfalme mmoja aliekuwa na wake wawili wazuri alialika wageni nyumbani kwake. Akaagiza wachinjwe wanyama wa kila aina kutoka katika mifugo yake - mbuzi, ng'ombe, ngamia, kuku, bata, kondoo, nguruwe, nakadhalika.

Baada ya mapishi kuwa yamekamilika wake wa yule mfalme waligundua kuwa miongoni mwa mapishi yale, nyama ya nguruwe ndiyo ilikuwa tamu kuliko zote kule jikoni.

Basi mke mmoja miongoni mwa wake wa mfalme yule aliamua kwa makusudi kuificha ile nyama tamu ili baadae wageni watakapokuwa wamekwisha kuondoka akampakulie mumewe ale. Na kwa akili ya yule mama alidhani kwa kumfanyia hayo mfalme yeye (huyu mama) atapendwa zaidi kuliko wake wenza.

Baada ya wageni kuwa wamekula na kushiba hatimae muda wa kuaga kuondoka kurejea makwao ukafika. Wakaenda zao.

Basi yule mke wa mfalme aliyekuwa ameficha ile nyama tamu akaipakua na kumtengea mfalme. Huku na kule mfalme akahoji kulikoni nyama ile iletwe hali wageni washaondoka? Mke akasema aliona ni vyema aifiche kwa ajili ya mfalme ili ampende zaidi.

Mfalme akasusa kuila akasema yeye aliandaa karamu kwa ajili ya kula na wageni wake na si kula peke yake kiuchoyo. Basi mfalme akatangaza mbele ya mkewe yule kuwa nyama ile haili na kwamba chakula kile (kitimoto) ni haram.

Kumbe wote tunakula kitimoto ila tu wengine wanakula kwa kificho na wikiendi ndo hii. Hapa Euro pale sahani ya kitimoto 😋
 
inasemwa kuwa eti mfalme mmoja aliekuwa na wake wawili wazuri alialika wageni nyumbani kwake.

akaagiza wachinjwe wanyama wa kila aina kutoka katika mifugo yake - mbuzi, ng'ombe, ngamia, kuku, bata, kondoo, nguruwe, nakadhalika.

baada ya mapishi kuwa yamekamilika wake wa yule mfalme waligundua kuwa miongoni mwa mapishi yale, nyama ya nguruwe ndiyo ilikuwa taamu kuliko zote kule jikoni.

basi mke mmoja miongoni mwa wake wa mfalme yule aliamua kwa makusudi kuificha ile nyama tamu ili baadae wageni watakapokuwa wamekwisha kuondoka akampakulie mumewe ale. na kwa akili ya yule mama alidhani kwa kumfanyia hayo mfalme yeye (huyu mama) atapendwa zaidi kuliko wake wenza.

baada ya wageni kuwa wamekula na kushiba hatimae muda wa kuaga kuondoka kurejea makwao ukafika. wakaenda zao.

basi yule mke wa mfalme aliekuwa ameficha ile nyama tamu akaipakua na kumtengea mfalme. huku na kule mfalme akahoji kulikoni nyama ile iletwe hali wageni washaondoka? mke akasema aliona ni vyema aifiche kwa ajili ya mfalme ili ampende zaidi.

mfalme akasusa kuila. akasema yeye aliandaa karamu kwa ajili ya kula na wageni wake na si kula peke yake kiuchoyo. basi mfalme akatangaza mbele ya mkewe yule kuwa nyama ile haili na kwamba chakula kile (kitimoto) ni haram.

kumbe wote tunakula kitimoto ila tu wengine wanakula kwa kificho. na wikiendi ndo hii. hapa Euro pale sahani ya kitimoto 😋
Usipende kuamini upuuzi mkuu, hizi ni hadithi tu za kizushi. Watu tunakula nguruwe toka utotoni na hatuna maradhi yeyote, kuna waislam wanafakamia nguruwe kama hawana akili na hawana tatizo lolote la kiafya.
 
Inasemwa kuwa eti mfalme mmoja aliekuwa na wake wawili wazuri alialika wageni nyumbani kwake. Akaagiza wachinjwe wanyama wa kila aina kutoka katika mifugo yake - mbuzi, ng'ombe, ngamia, kuku, bata, kondoo, nguruwe, nakadhalika.

Baada ya mapishi kuwa yamekamilika wake wa yule mfalme waligundua kuwa miongoni mwa mapishi yale, nyama ya nguruwe ndiyo ilikuwa tamu kuliko zote kule jikoni.

Basi mke mmoja miongoni mwa wake wa mfalme yule aliamua kwa makusudi kuificha ile nyama tamu ili baadae wageni watakapokuwa wamekwisha kuondoka akampakulie mumewe ale. Na kwa akili ya yule mama alidhani kwa kumfanyia hayo mfalme yeye (huyu mama) atapendwa zaidi kuliko wake wenza.

Baada ya wageni kuwa wamekula na kushiba hatimae muda wa kuaga kuondoka kurejea makwao ukafika. Wakaenda zao.

Basi yule mke wa mfalme aliyekuwa ameficha ile nyama tamu akaipakua na kumtengea mfalme. Huku na kule mfalme akahoji kulikoni nyama ile iletwe hali wageni washaondoka? Mke akasema aliona ni vyema aifiche kwa ajili ya mfalme ili ampende zaidi.

Mfalme akasusa kuila akasema yeye aliandaa karamu kwa ajili ya kula na wageni wake na si kula peke yake kiuchoyo. Basi mfalme akatangaza mbele ya mkewe yule kuwa nyama ile haili na kwamba chakula kile (kitimoto) ni haram.

Kumbe wote tunakula kitimoto ila tu wengine wanakula kwa kificho na wikiendi ndo hii. Hapa Euro pale sahani ya kitimoto 😋
Nahisi utakuwa una akili timamu....hivi unaamini upuuzi huu kweli?
 
Usipende kuamini upuuzi mkuu, hizi ni hadithi tu za kizushi. Watu tunakula nguruwe toka utotoni na hatuna maradhi yeyote, kuna waislam wanafakamia nguruwe kama hawana akili na hawana tatizo lolote la kiafya.
Swala si tatizo la ki afya je umetii amri ya aliyekuumba? Si waislam wala wakristo wote aliyetuumba amekataza nguruwe kuliwa , kwa nini anajua yeye mwenyewe kwa hyo kazi kwetu kutii na ukikataa kutii hii itakua juu ya nafsi yako
 
Back
Top Bottom