Kwanini anga lina rangi ya blue?

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,677
106,779
Salute..

Naomba mnisaidie kufahamu hii kitu. Kwanini anga ni la blue? Nimejaribu kutumia ka elimu kangu ka Rangi na Reflection of Lights kutoka sekondari ila nimeshindwa kutambua.

Mimi nachofahamu rangi ya anga linaonekana hivyo lilivo kutokana na ukomo wetu wa kutazama, yaani hiyo rangi ya blue inaonekana kwakua hapo ndiyo macho yalipoishia kutazama.

Lakini pia kwanini tusione rangi zingine tunaona blue tu? Watalamu wa macho nisaidieni.

Karibuni mliopta shule....

Mkimaliza kujibu rangi mniambie mbinguni ni wapi, maana sijui watu wa Babeli walijenga vipi mnara ukafika mbinguni.
MICHANGO YA WADAU
Wick anasema...
Mkuu usisahau kunitag ukifungua uzi wako, Lakini kulijibu short swali hakuna sehemu ambayo unapata rangi ya blue ila kuna eneo ambalo miale ya jua ikifika ndio inatawanywa!..
Upeo wa macho yako unafanya uhisi sehemu fulani angani ukifika kuna rangi ya blue kitu ambacho sio.
Miale inapotoka kwenye jua ikaifikia sayari yetu kuna layer inapofika inakutana na molecules za aina mbalimbali, vumbi kulingana na shughuli za sehemu husika, kuna moshi wa viwandani, ukungu, barafu na shughuli zingine za kibinadamu zinazopelekea kuharibu/kuchafua anga sasa hivi vyote vinapelekea ile miale itawanye huko angani, kuna kitu kinaitwa sky radiation na kwa vile miale ya blue ina wavelengths fupi kuliko mingine basi inapelekea yenyewe itawanywe eneo kubwa zaidi na ndio maana unaona anga lote la blue, lakini kiuhalisia kuna maeneo anga lao sio blue kama unayoiona wewe huku!..
Na hiyo blue unayoiona ni pale jua linapokuwa direct juu yako lakini likienda upande unapata rangi nyingine sababu miale inayokuja na kutawanywa blue inakuwa weak so unakuta unaona rangi nyekundu au njano au zingine (asubuhi n jioni).
Kuhusu rocket kupita kwenye ublue na jua nahisi unatania haupo serious

Avatar mok
Kuna kitu inaitwa 'scattering' kama inavojulikana kwamba mwanga wajua una range tofauti za rangi na zenye wavelength tofauti kutoka x-ray hadi hizo blue..

Turudi kwenye swali.. why anga ni la blue.. sababu ni mwale unapotoka kwenye jua unabeba waves tofauti za rangi tofauti. Ktk hizo range rangi y blue ina wavelength kubwa yaani kipenyo chake kutoka crest moja kwenda nyingine, pia kitu chenye wavelength kubwa kina frequency ndogo ya kupenya vitu.. mfn xray ina frequency kubwa na wavelength ndogo ivyo unaweza pata pich ya mifupa.

Angani kuna particles tofauti, za gas na dust.. rangi ya blue inapogonga izo particles inatawanyika 'scattering' hivyo basi tunaona rangi ya blue.

Nimejaribu kudadavua ...
View attachment 1245596

reyzzap
na hiki ndio nijuacho,
kwa kuongezea tuu, n kwamba rangi hii ya blue hutolewa na jua(jua lina rangi takriban 7, kwa ufupi zile rangi zote unazoziona kwenye upinde wa mvua ndio zipo kwenye jua kwa mpangilio ule ulee), kwenye ule mpangilio(light spectrum) km sikosei inaanza red ambayo ina high wavelengt, ya pili kutoka mwisho ni blue na ya mwisho ni violet ambayo ina short wavelength kuliko zote,
yenye short wavelenght ndio rahisi kusambaa hivyo ni rahisi kuiona

swali: je ni kwa nn hatuoni anga au bahari ikiwa na rangi ya violet yenye wavelengh ndogo kuliko blue(kumbuka yenye wavelength ndogo ndio rahisi kusambazwa na rahisi kuiona)

Jibu: violet inasifa yakua absorbed katka atmosphere hivyo kufifia/kutofika/kupungua nguvu hivyo reflection yake inakua ndogo kwenye macho yetu,
kwa ufupi macho ya binadamu ni more sensitive to blue colour kulinganisha ni violet.

Na hii ndio sbb bahari huonekana ya blue sbb ya reflection, nenda baharini angalikiwa jeupe km utaona bahari ya blue.

Kitu kingne unachopaswa kuelewa ni
HAKUNA KITU CHENYE RANGI YAKE DUNIANI; WALA HAKUNA RANGI KATIKA ULIMWENGU HALISI BALI THEORETICALY ILA TUU KUNA MWANGA WENYE WAVELENGHT(HII NDIO HULETA RANGI) TOFAUTI.

Rangi ni matokeo ya Mwanga mweupe(mwanga mweupe unabeba rangi zotee), uwezo wa jicho lako na Brain perception.
ndio maana Kuna mda unaona watu wakibishana kuhusu rangi,

Kila kiumbe kina uwezo wake wa kuona rangi tofauti tofauti kulingna na type za cons alizonazo,

wakiongozwa na Ndege, samaki, Nyukii, wadudu hawa wanaona mpk ultraviolet light, sbb wanatype nne za cons(sitazungumzia kuhusu cons this is simple Biology karbun wote tulisoma wala light inavyofanya kazi kwenye cornea this is simple Physics ya O-level ambayo weng tumesoma n suala la kukumbuka tuu),
kwa waliosoma Baadhi ya kozi za chemistry vyuoni watakumbuka Spectroscopy, masuala ya EMR hope ni part ya inorganic Chemistry hii kitu si shida,

Hawagusii inavyofanya kazi kwenye jicho ila inazungumzia sana wavelength na frequency ambavyo ndio nguzo kubwaa,

Tukifuatia binadamu wenye corns tatu pamoja na apes na chimps, sisi rangi zetu kubwa ni Blue, green, na red(rangi zote uzionazo ww ni matokeo ya hizi rangi tatu, uwezo wa macho na brain perception ndio vitaamua uone ipi, mfn yellow ni matokeo ya mchanganyiko wa red na green n.k n.k
NA KM ULIKUA HUJUI , TV ZINATENGEZWA KWA HIZO RANGI TATU TUU, HAYO MARANGI MENGNE UNAYO YAONAGA NI MAPICHA PICHA TU YA JICHO LAKOO

Paka, panya, mbwa ni kundi la wanyama wanaaoona rangi chache sanaa, wao rangi zao kubwa ni black and white, Sbb n kwamba wao hawatumii sana cornea bali hutumia rods ambazo huhusika ktk low light reflection na zipo sensitive to black and white colour tuuu.

aisee nashindwa kuandika vyote hapa km una swali uliza, pia narudusu kukosolewa, kusahihishwa na kupingwa, hizi elimu zote ni mapokeo, pokea ujue, hujui leo kesho unajua...
 
Salute..
Naomba mnisaidie kufahamu hii kitu.. kwanini anga ni la brue nimejaribu kutumia ka elimu kangu ka Rangi na Reflection of Lights kutoka sekondari ila nimeshindwa kutambua.
Mimi nachofahamu rangi ya anga linaonekana hvo lilivo kutokana na ukomo wetu wa kutazama..yani hiyo rangi ya blue inaonekana kwakua hapo ndio macho yalipoishia kutazama. Je niko sahihi?
Karibuni mliopta shule....
Blue
 
Mkuu..tupe majibu inaonyesha una madini mno..
Nakupa mfano mwepesi sana usipotafakari basi ukalale: Maji ya Ziwa , Maji ya Bahari ukiwa mbali huonekana Blue but ukisogea ukayachota yanakuwa Hayana rangi (colorless ) Hii inakuonyesha sehemu yoyote yenye kina kirefu ikipata mwanga kwasababu inakuwa aina mwisho kwa upeo wa macho yako basi huliflect rangi ya Retina ndani ya jicho la mwanadamu kuashiria hakuna Reflaction ya kutengeneza object ndani mfumo wa jicho.
 
Naomba nichangie kwa sauti ya chini kabisa, inasemekana eti ile blue inatokana na mwanga wa jua na gesi tofauti zilizopo hewani,
 
Back
Top Bottom