Kwanini ajali ya mabasi 2 na lori la mafuta kuungua moto iliotokea Mlandizi haiongelewi? Wembamba wa Morogoro Road ni janga la taifa

".. akauziwa kicheche .."
Ye baba ajali za kuovateki mara nying zinatokea kwa kuwa kuna mmoja anakua kaunga tela kisa wa mbele katoka wa nyuma nae anatoka ...

Mana mara nying ukiovatek kwa hesabu au hata ukibugi hesabu kdg gari inayokuja huwa inatoa fair kwa kupunguza spidi then unapita sasa unakuta kakupunguzia ww spid urudi kwako kumbe kuna chizi nyuma nae kaliunga we ukirudi haoo wanaumana....
 
Pamoja na upumbavu wa madereva, pia uzembe na upuuzi wa mamlaka za uma unahusika. Barabara kuu yenye msongamano namna hiyo yahitaji upanuzi. Lazima barabara kuanzia Dar hadi Morogoro iwe na zaidi ya lane 2.
Hadithi ya mradi wa PPP barabara hiyo imeishia wapi?
Watu wetu wanaagamia kwa kukosa maarifa (madereva na Tanroad)
 
Kwani njia 8 ya JPM imejengwa barabara ipi?
 
Huu mtindo wa kuovertake hata mimi unanishangaza sana
Akiovertake mmoja ,wote wanafuata
Mbaya zaidi wanaovertake hadi sehemu hatarishi kama Kitonga..hadi unawaza hawa madereva wanatutakia nini haswaam
 
Serikali umesahau kwamba kuuza bandari kunatakiwa kwenda sambamba na barabara inayokwenda huko bandarini.
Kwa foleni iliyoko Kati ya Kibaha na Chalinze na Ile ya kule mpakani tunduma, hata Kama DPW wanaweza kufanya 100 moves per hour bado congestion bandarini itaendelea kuwepo na container turn around itakua mbaya zaidi.
Sawa na kujenga choo kizuri halafu ukasahau kuunganisha bomba la maji.
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=-JLclXeyawA
Ni uzembe wa madereva kutanua na kufukuzana kwa mwendo mkali yakiwa yameachana mita umbali kiduchu.

Hii ni hatari sana mabasi kuwa ktk mwendokasi yakiwa yamekaribiana mna kukitokea kitu ghafla ndiyo hilo la basi moja na lingine kuhusika ktk ajali ya Lori la Mafuta na mabasi ya kampuni hizo

Madereva lazima wakubali kusoma mazingira iwe barabara nyembamba, kona kali, kilima, mwinuko n.k na kuendesha kwa tahadhari ili kujihami na ajali inayoweza kuwakabili kufutana na mazingira halisi ya barabara

 
Kumbe aiseee iligonga mwamba ?!
Yap waliivuta kwa kutumia Satellite wakaja na majibu pana jamaa Eng wa wapi sijui aliambiwa akate juu ilivyogeuka watu walikua wanapiga kelele maana ilikua inazama taratibu baada ya kuikata lile eneo lililokua linaonekana ilizama kwa siku chache...
 
Yap waliivuta kwa kutumia Satellite wakaja na majibu pana jamaa Eng wa wapi sijui aliambiwa akate juu ilivyogeuka watu walikua wanapiga kelele maana ilikua inazama taratibu baada ya kuikata lile eneo lililokua linaonekana ilizama kwa siku chache...
Dah nasikia ilikuwa meli kubwa sana. Ila sidhani kama ni kubwa kama hii mpya MV MWANZA
 
Hawani mipango mikakati, wanajiamria tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…