GE2025 Kwanini account za Ikulu zinarusha tukio la Mgombea Samia kuchukua fomu ya kugombea? Watarusha na wagombea wa vyama vingine?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Blessed Tajiri

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2023
Posts
221
Reaction score
659
Wakuu,

IMG_20250809_113113_267.jpg

Hili ni tukio la kichama, katika shughuli ambayo kama atafanikiwa basi acc hizo za ikulu ndio zitatumika kirusha matukio yake.

Kwanini zinatumika leo Samia akienda kuchukua fomu kama mgombea wa CCM, ni kwamba wameshapitisha kwamba yeye ameshakuwa Rais?

Vyama vingine vikienda kuchukua fomu za Urais nazo watarushwa kwa account ya Ikulu? Wasipowarusha pia hiyo itakuwa ni upendeleo wa wazi wazi, na tayari mapema kabisa mmeshaonesha wananchi kuwa Samia kashawazidi kete wengine, hadi ameanza kutumia vitu vya serikali.

Leteni hizo povu tukafulie nguo!
 
Kama ni la kichama , kwa nini ADC na Walinzi wamejaa kila kona?
 
Wakuu,

Hili ni tukio la kichama, katika shughuli ambayo kama atafanikiwa basi acc hizo za ikulu ndio zitatumika kirusha matukio yake.

Kwanini zinatumika leo Samia akienda kuchukua fomu kama mgombea wa CCM, ni kwamba wameshapitisha kwamba yeye ameshakuwa Rais?

Vyama vingine vikienda kuchukua fomu za Urais nazo watarushwa kwa account ya Ikulu? Wasipowarusha pia hiyo itakuwa ni upendeleo wa wazi wazi, na tayari mapema kabisa mmeshaonesha wananchi kuwa Samia kashawazidi kete wengine, hadi ameanza kutumia vitu vya serikali.

Leteni hizo povu tukafulie nguo!
Hiyo siyo tume huru ya uchaguzi, ni tume ya ovyo sana ambayo imeundwa na makada wa CCM. Acheni uongo, huo uchaguzi ni haramu kama walivyo wagombea wa CCM waliojichagua wenyewe na baba yao Kikwete. Hakuna uchaguzi....Mnaoufanya ni upumbavu.
 
Siku hizi hata kwenye sare zao za chama wanaweka Logo/nembo ya bibi na bwana kulia na kushoto ya chama chao CCM.

Usistaajabu wakati wa kuchinja hata kuku huwa kuna purukushani nyingi ukitetereka anaweza kuzabua kibao au kukuponyoka.

Stay still hizo mbwembwe ni nyingi mno lakini hazitakuwa na msaada siku si nyingi.
 
Tuungane na chadema
No refors no election'
 
Dah, yani kule naona watu wanahoji kwa nini TBC haijarusha, huku watu wanahoji kwa nini akaunti za Ikulu zinarusha.
Mtu anaweza kusema unamtimulia vumbi mkiwa kwenye bwawa la maji
 
Dah, yani kule naona watu wanahoji kwa nini TBC haijarusha, huku watu wanahoji kwa nini akaunti za Ikulu zinarusha.
Itakua wanawashangaa TBC,siyo kawaida yao.
 
Dah, yani kule naona watu wanahoji kwa nini TBC haijarusha, huku watu wanahoji kwa nini akaunti za Ikulu zinarusha.
Mambo ni moto, lakini TBC imeishura, itakuwa huyo aliona matangazo yalipokuwa yamekata dk fulani, ila wamerusha
 
Back
Top Bottom