Kwani, watu wa mitandaoni siyo Watanzania? Rais Samia amejiongoza vibaya!

Mlaumu Kikwete kwani ndiye mshauri wake mkuu ona hata watu anaowachagua, wengi wao ni vilaza waliofukuzwa kwenye awamu iliyopita na sasa anawarudisha madarakani kwenda kucheza karata ofisini.
 
Embu tukumbusheni waliopiga kura kuwachagua ccm president candidates na wenye kutumia internet wapi wengi ?
 
Labda raisi aliposema kikundi cha watu wachache mitandaoni alimaamisha Twitter Republic.

Watanzania wengi wanatumia mitandao kukimbia stress za siasa na maisha; kama sehemu ya kujiliwaza.

Ebu pita vijiwe vya vijana waliozibuka mkoa wowote waulize makamu wa raisi yupo wapi kama wanajua au kufanya nini hivi karibuni.

Halafu watu hao hao waulize nini kina trend insta hasa kama kuna ugomvi wa watu wanaowafuatilia uone kama kuna asiejua.

Ushasoma post za vijana kwa yule dada yao akiwapa habari za siasa. Utawasikia ilo jambo tushakuelewa sasa hivi tunatakauongelee sijui nani kafanya, au siku akigombona utawasikia haya ndio mambo ninayoyapenda; kaazi kweli kweli kwa vijana wa kesho.
 
Labda raisi aliposema kikundi cha watu wachache mitandaoni alimaamisha Twitter Republic.

Watanzania wengi wanatumia mitandao kukimbia stress za siasa na maisha; kama sehemu ya kujiliwaza.

Ebu pita vijiwe vya vijana waliozibuka mkoa wowote waulize makamu wa raisi yupo wapi kama wanajua au kufanya nini hivi karibuni.

Halafu watu hao hao waulize nini kina trend insta hasa kama kuna ugomvi wa watu wanaowafuatilia uone kama kuna asiejua.

Ushasoma post za vijana kwa yule dada yao akiwapa habari za siasa. Utawasikia ilo jambo tushakuelewa sasa hivi tunauongelee sijui nani kafanya, au siku akigombona utawasikia haya ndio mambo ninayoyapenda; kaazi kweli kweli wa vijana wa kesho.
Samia amekuwa na kawaida ya kujichanganya Sana hususani katika mazungumzo ya papo kwa papo! Kwani yeye hufuata Nini huko mitandaoni na wakati mwingine kukiri kuyafanyia kazi maoni ya mitandaoni kama "walioko mitandaoni hawana maana"?!

Samia hajipangi vizuri kwenye mahojiano ya papo kwa papo na hotuba za hadharani; ajirekebishe or else mkanganyiko wake utampeleka pabaya, ataichukia press bure buree!
 
Samia amekuwa na kawaida ya kujichanganya Sana hususani katika mazungumzo ya papo kwa papo! Kwani yeye hufuata Nini huko mitandaoni na wakati mwingine kukiri kuyafanyia kazi maoni ya mitandaoni kama "walioko mitandaoni hawana maana"?! Samia hajipangi vizuri kwenye mahojiano ya papo kwa papo na hotuba za hadharani; ajirekebishe or else mkanganyiko wake utampeleka pabaya, ataichukia press bure buree!
I agree partly

Ningekuwa mimi ndio Samia ningemuuliza Kikeke watanzania gani walimwambia wanataka katiba mpya? Ana research yoyote iliyofanyika yenye sample size iliyotoa majibu watanzania wanataka katiba mpya.

If anything swali alilopewa lilikuwa ni ‘leading question’ na yeye akaingia mkenge kulijibu kwa stahili aliyotumia, sasa ukizingatia juzi katoka kuteua Director of communication ambae anatakiwa kuwa mtaalamu wa hayo mambo na kumwongoza raisi namna ya kujibu maswali kama input yake ndio hiyo sio far, ni kazi bure tu.
 
"Tusimame kukataa kurudishwa kwenye mfumo wa chama kimoja" , ni mstari katika Aya yako ya mwisho;

1. Je watawala wanataka kufuta vyama vingi na kubaki na chama kimoja?
2. Hayo maneno yanamanisha mnataka katiba mpya ili kujinufaisha kisiasa?
 
Watanzania wa kawaida hatuitaki katiba mpya ya serikali 3 itatuongezea mzigo wa Kofi

Kama CDM mpo tayari kudai katiba mpya yenye serikali 2 semeni tuwaunge mkono
Warioba alipunguza vyeo na size ya bunge na serikali. In fact serikali 3 ilikua cheaper kuliko mfumo wa sasa ambao kuna uongozi unao overlap mfano MBUNGE,DC,MEYA,MKURUGENZI.... Hao wote wapo wilayani ila majukumu tofauti ilihali ungeweza Baki na wawili tu kati ya hizo post.
 
Martin Maranje Masese:

Andiko ni zuri lakini nini hasa dhumuni lako mkuu ?

Tunamlenga mtanzani gani wa jukwaa la social network/ vijijini ambao network mpk kupanda juu ya mti au anayesubiri barabara na maji yamfikie ??
Hivi kwanini mnaifanya katiba ni zero sum game, yaani ukidai katiba basi hautaki maji na barabara? In fact katiba mpya (Warioba) ingerahisisha hayo kupatikana maana hta wananchi wanaweza kumtoa mbunge midway kma asipotekeleza maendeleo aliyoahidi.

Pia ingeongeza uwajibikaji maana mawaziri wasingetoka bungeni hivyo kutokua na maslahi directly na chama tawala.

Pia wabunge wangechapa kazi kupeleka maendeleo maana hawatokua na option ya kupata uwaziri.

Pia ingesave gharama za uendeshaji serikali maana vyeo vingepunguzwa hivyo kuacha excess funds zikatumike kwa maendeleo.

Yes ingeleta mahakama huru hivyo mafisadi wangekua wanavyooshwa na wizi ungepungua kuliko sasa ambako mahakama inapangiwa mambo na serikali?

Kiufupi katiba ingeleta uwajibikaji hivyo hata hayo maji na barabara wanayotaka upo secured na katiba mpya kuliko hii ya sasa ambao hata bajeti ukiipinga basi bunge linavunjwa.

Yaani chombo ambacho kimewekwa kumsimamia Serikali alete barabara na maji kikiona kuna udhaifu kwenye bajeti kikaigomea basi Anayesimamiwa anaweza kulivunja? Hapo kuna uwajibikaji kweli?
 
Halafu mtu useme tuna Rais. Mimi nadhani Rais inabidi awe na high mental power of reasoning
 
Kwani, watu wa mitandaoni siyo watanzania? Rais Samia amejiongoza vibaya!

Nani anamdanganya Rais wetu Samia? Kama Rais wetu hajadanganywa, kwanini ameamua kujiongoza mwenyewe vibaya katika hili la uhitaji wa katiba?

Nimemsikiliza vyema sana na kurudia mara kadhaa akimueleza mwandishi wa habari, Salim Kikeke wa BBC katika mahojiano maalum kwamba suala la katiba mpya linapigiwa kelele na watu waliopo mitandaoni na siyo watanzania.

Kauli ya Rais Samia naibeba kama taswira halisi ya CCM. Hawataki wimbo katiba mpya kabisa. Wanaamini ni njia ya kuwaondoa madarakani.

Ni kweli wataondoka tu. Hakuna chama cha kudumu madarakani milele. Lakini, katiba mpya itazungumza masuala mengi, haki, uhuru, usawa, utawala bora, afya, elimu, demokrasia. Wananchi, tuwalizimishe, tusiwabembeleze!

Nani alimueleza mpendwa Rais Samia kwamba watu waliopo mitandaoni siyo watanzania? TCRA wanaeleza mwaka 2014 watumiaji wa intaneti walikuwa 14.21M.

Kufikia mwaka 2016 idadi ya watu wenye kutumia simu za mkononi ilifikia watu 39.81M. Hii ni 69% ya watanzania wote. Kufikia mwaka 2016 wanaotumia intaneti walifika 19.86M. Ni kweli, TUNATAKA KATIBA MPYA!

Takwimu za TCRA (mamlaka ya serikali inayohusika na Mawasiliano) imetueleza hadi 2016 ni watanzania 39.81M walikuwa wanatumia simu za mikononi na watumiaji intaneti walikuwa 19.86M, vipi sasa takwimu za miaka 6 baadae, 2022? Ni wazi watumiaji wa intaneti wameongezeka. Ndivyo!

Dunia ipo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda ambapo shughuli nyingi zinafanyika kwa kutegemea TEHAMA ikiwemo kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda, uchimbaji madini, biashara, utoaji wa huduma kama vile afya, elimu. Watanzania pia ni sehemu ya Dunia, wanatumia mitandao kwa shughuli zao.

Oktoba 14, 2021 katika kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, wiki ya vijana na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru zilizofanyika katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, Kwa kutambua umuhimu wa Tehama, Rais SSH alisema Serikali imeondoa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye simu janja, vishikwambi na modemu ili kuwajengea vijana mazingira ya kujiajiri kwa maendeleo yao.

Siyo uongo, TEHAMA imewezesha shughuli nyingi kurahisishwa katika upatikanaji wake. Huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi kama vile Ufugaji, Kilimo, Uvuvi, Afya, huduma za kibenki, uchimbaji madini, ulipaji wa bili za maji na nishati ya umeme kwa njia ya mtandao, ulipaji wa kodi na mapato ya Serikali,

Pia, urahisashaji wa upatikanaji wa huduma za afya na tiba, elimu, huduma za Vipimo, masoko, biashara, taarifa za hali ya hewa na upatikanaji wa taarifa mbalimbali na kupunguza upotevu wa mdana na gharama za kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kwa ajili ya kupata huduma na mahitaji mbalimbali. Maana yake, watanzania wapo mitandaoni wengi tu

Rais wetu, Samia amejiongoza vibaya katika hilo. Anasema watanzania wanataka maji, barabara, shule, hospitali, miundombinu, umeme na uchumi ulioharibika.

Nani aliharibu uchumi? Ninyi wenyewe mlitupa hadithi za uchumi wa kati wa viwanda na ukuaji wake wa kasi ya 7.3%. Nani kaharibu uchumi wenu imara usiotegemea mabeberu.

Hao wanaosema wanataka maji, barabara, shule, hospitali, miundombinu,umeme na uchumi ulioharibika wapewe, ni haki yao.

Wanalipa kodi, siyo hisani, ni haki yao kurejeshewa huduma stahiki za kijamii. Hao wanaotaka katiba nao ni haki yao. Katiba yetu imepitwa na wakati na haina misingi simamizi ya kujisimamia. Wapewe!

Hao waliopo mitandaoni ndiyo hao wapo mtaani. Mfano, mimi, MMM, nipo mtandaoni, lakini pia ninaishi mtaani, ninayo familia. Mke na watoto.

Tafsiri ya Rais ya kwamba waliopo mitandaoni siyo sahihi. Yeye pia yupo mitandaoni, ana akaunti Twitter na inaongoza kutoa salamu za vifo. Hivyo naye tumhesabu kama mmoja kati ya waliopo mitandaoni au wale waliopo ardhini, Magogoni na hawataki katiba?

Rais Samia anajua, labda kama amekubali kudanganywa au ameruhusu madaraka yamzidi nguvu. Samia alikuwa makamu mwenyekiti wa bunge maalum la katiba (BMK) mwaka 2014.

Bunge hilo lilifanya kazi ya maoni ya wananchi, kupitia tume ya Jaji Warioba, walitoa maoni yao nchi nzima, wanataka katiba mpya. SSH hajui alikuwa alifanyia kazi maoni ya wananchi na siyo CCM?

Wakati wa kukusanya maoni ya tume ya mabadiliko ya katiba, uliwekwa utaratibu kwa wananchi kutoa maoni kwa ambao watakuwa mbali na hawawezi kufika mbele ya tume.

Iliwekwa namba ya simu, unaandika ujumbe wako humo. Pia kulikuwa na ukurasa wa Facebook. Sasa hivi Kuna Clubhouse, Instagram, Facebook, Twitter etc, ndiyo SSH ashangae watu wa mitandaoni kutaka katiba mpya?

Rais Samia asikwepe jukumu na wajibu wake. Katiba hii haikumpa madaraka awe mfalme au Sultan, hapana. Ni LAZIMA atusikilize SISI waajiri wake.

Tunataka katiba mpya. Kama anadhani sauti haitoshi, anaweza kuunda kamati au tume maalum kukusanya maoni ya umma au kura za maoni. Athibitishe!

Hii haitakuwa mara ya kwanza kuunda tume. Harakati za kudai kurejeshwa mfumo wa vyama vingi zilipokolea nchi nzima mwaka 1991, Rais Ali Hassan Mwinyi aliteua Tume iliyoongozwa na Jaji Mkuu, Francis Nyalali kukusanya maoni ya wananchi na kutoa mapendekezo kujua kama taifa lilihitaji mfumo wa vyama vingi au kuendelea na mfumo wa chama kimoja.

Harakati hizo zilisababisha kubadilishwa kwa Katiba ili kurejesha mfumo huo ambao ulikuwa umefutwa Januari 14, 1963 kwa Azimio la Halmashauri Kuu ya Tanu.

Kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi kulisababisha kuanzishwa kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo kwa mujibu wa Sheria namba 5 ya mwaka 1992, mbali na kusajili vyama anapaswa kuhakikisha sheria hiyo inafuatwa na vyama vya siasa.

Rais SSH anapaswa kutambua kwamba katiba mpya tunayohubiri kila uchwao, itaweka misingi ya kiuchumi imara ambayo itapambana na ufisadi mkubwa na ubadhirifu wa mali za umma unaofanywa na watawala na watumishi wa umma. Hatutataka tena kuwaona mafisadi wa ESCROW, EPA, RICHMOND, wakitamba mtaani. Katiba iwashughulikie.

Uchumi imara lazima uwekewe misingi. Lazima ziwepo itikadi na falsafa za kiuchumi ambazo tunatakiwa kuzifuata katika uchumi wa Dunia.

Je, katiba yetu imeweka misingi hiyo? Nchi yetu haina 'blueprint' ya kiuchumi. Tutaiweka vizuri katika katiba mpya. Itawajibika kutuongoza, tusiyumbishwe na upepo.

Serikali inayokusanya kodi kwa wananchi, haipaswi kufanya huduma za kijamii kama ni hisani. Ni wajibu wa serikali kutoa huduma za kijamii na hazipaswi kuzuia mambo mengine muhimu kufanyika. Tunaweza kupata fedha za kutengeneza katiba yetu (hata kwa kuchangishana) kama kilio chenu ni fedha.

Kama mnaweza kupata Shs. 11 bilioni za kutengeneza filamu yenu ya 'Royal Tour' ambayo hatujui kesho inaweza ikafanikiwa au isifanikiwe kutuletea neema, na mmetumia Shs. 7 bilioni, sioni sababu ya ninyi kusema fedha za kutengeneza muundo upatikanaji katiba mpya ni tatizo. Tunazo fedha. Fedha zipo. Umma tunazo. Tuwape?

Mwl, Nyerere alifuta mfumo wa siasa wa vyama vingi mwaka 1965 baada ya safari ya China. Tanzania ilirejea katika mfumo wa vyama vingi vya siasa Julai 1992.

Kilikuwa kipindi muhimu na cha mafanikio kwa wanaharakati wa mageuzi kama Mabere Marando, James Mapalala, Bob Makani na Edwin Mtei na wengine ambao waliongoza harakati hizo za kupigania mfumo huo.

Hata huu muundo wa siasa za vyama vingi vya kisiasa, CCM na wengine wengi (80%) hawakuupenda. Waliukata. Ni 20% tu walisema twende nao.

CCM Waliendesha kampeni nzito hadi kwenye taasisi za umma na vyombo vya kijeshi, wakatae. Na kweli waliukataa. Wachache walisema tunataka mfumo huo. Na busara 'za watu timamu' zikasema twende na wachache.

Chama cha siasa kinatakiwa kufanya siasa bila kujali vikwazo na changamoto zilizopo, kuepuka vyama shikizi vinaibuka nyakati za uchaguzi. Lakini mazingira ya kufanya siasa kwa uhuru yamekuwa na wakati mgumu, hasa baada ya Serikali kupiga marufuku shughuli za vyama vya siasa.

Sasa mmepiga marufuku mikutano ya hadhara, Maandamano ya vyama vya siasa ambayo yameruhusiwa na Sheria ya vyama vya siasa.

Ni Kwa namna gani vyama vya siasa, vitawafikia wananchi wao, kuwapa elimu ya uraia na kuwauliza kuhusu uhitaji wa katiba mpya? Acheni uoga. Tuwasikilize watu

Msijitazame tu kama CCM. Tokeni nje ya sanduku hilo, muone Tanzania yote. Mnaweza kuwa mnasikilizana wana CCM pekee, nje hamsikii, na ukizingatia mmewapa hofu wananchi, hawawezi kuandamana kuonyesha hisia zao na vyama vya siasa vipo kifungoni, hamsikii sauti za katiba mpya.

Uhuru wa kiraia na kisiasa si wa kudumu na unabanwa na sheria na kanuni nyingi sana nchini Tanzania. Uhuru huo unadhibitiwa na dola kupitia Jeshi la Polisi na vyombo vingine.

Chaguzi zilizopita hazikuwa huru na za haki. Rais Samia anapaswa kulitibu hilo kwa kutuacha na katiba mpya ambayo itaweka uwanja sawa wa kufanya siasa za vyama vingi bila dola kupora mchakato wa uchaguzi.

Dunia inabadilika, inastaarabika, inalinda misingi ya utawala bora ndani ya mipaka yao kupitia katiba, sisi tunabaki na kuganda hapo hapo tulipokuwa mwaka 1977.

Tutakuwa na aakili kweli? Bila shaka tunapaswa kustaarabika, Dunia inabadilika na sisi tunapaswa kubadilika pamoja na Dunia.

Nanukuu kauli ya Freeman Mbowe ameitoa Machame, Hai, Kilimanjaro, 20/3/2022 wakati akitoa shukrani kwa Kanisa la KKKT, Usharika wa Nshala Machame - Hai, kumshukuru Mungu na kanisa kwa kumuombea kwa kuwekwa gerezani kwa siku 227 tangu alipokamatwa July 2021, Mwanza katika kongamano la katiba mpya

“Huwa najiuliza, katika suala la katiba hivi tunagombania wapi, na kwanini tugombane. Hawa wanasema wanataka katiba na hawa wanasema wanataka shule, kwani aliyesema anataka shule wapi alisema hataki katiba bora?. Tukae tuzungumze tofauti zetu ziko wapi.” - Freeman Aikaeli Mbowe

Wananchi ndio jeshi la mstari wa mbele la ulinzi wa Katiba ya nchi yoyote Duniani. Tusimame kukataa kurudishwa kwenye mfumo wa chama kimoja.

Umoja wa ulinzi wa demokrasia (Democratic Front ) Ni muhimu zaidi hivi sasa kuliko wakati wowote katika miaka 30 ya uwepo wa demokrasia yetu. MSIOGOPE!

Muda wa katiba mpya ni sasa, siyo jana, siyo kesho, siyo vinginevyo. Saa ya ukombozi ni sasa!

#MMM, Martin Maranja Masese

Watu wanaoyafanya malalamiko ya katiba yawe na mashiko ni hawa wanaovamia fani za watu, waliozoea holela katika uongozi wa kila taasisi.

Hao wakiweza kuondolewa na kila taasisi ikaongozwa kwa weledi hakutakuwa na vilio vya katiba mpya. Ni makaratasi tu, ni taratibu tu za kuongoza nchi ingawa zinaonekana ni za muhimu kwa kulitazama hilo ombwe la kiuongozi la kitaasisi.

Kila udhaifu wa kiserikali, kitaasisi na kijamii kisingizio ni katiba mpya. Tunaitumia kama kichaka cha kuhalalisha maovu yote yanayotokea.

Kenya waliweza kufanya mabadiliko ya katiba, ufisadi wa kiwango cha juu bado upo pale pale. Pengo kati ya masikini na tajiri lipo pale pale.

Siku zote ukitatua tatizo moja linazaliwa jingine na pengine linaweza kuwa kubwa kuliko la mwanzo. Cha muhimu ni sera nzuri kuwepo na watu wenye weledi kupewa nafasi serikalini.
 
Martin Maranja Masese anzeni kwanza kuboresha Katiba ya CHADEMA iondoe Uwenyekiti wa kudumu wa Freeman Mbowe.

Jisafisheni kwanza nyinyi ndiyo mtushawishi tuone ubora wa Katiba Mpya
Kipengele Gani kinasema uenyekiti ni WA kudumu? Unaweza ukakiweka hapa.

Kuna Uzi humu wa Dr slaa na Mnyika ni WA 2012 hii hoja ilishajibiwa nashangaa 10 years later mnahoji kitu ambacho hata kwenye katiba nikikwambia unionyeshe hamna?

Btw Mbowe alipoingia Cha kwanza kufumuliwa ilikua katiba, na ndio unaona mafanikio yote haya tumepata. So unapodai tuboreshe katiba unataka afanye mara mbili? Ameingia alikuta hatuna BAWACHA Wala BAVICHA yaani chama hakina wing ya vijana au wanawake?? Hivi huwa mnafuatilia siasa kweli au mkishiba maharage mnaingia jf kucomment?
 
Kenya waliweza kufanya mabadiliko ya katiba, ufisadi wa kiwango cha juu bado upo pale pale. Pengo kati ya masikini na tajiri lipo pale pale.
Siasa za Kenya unazijua kweli? Hawa ni mafisadi waliofikishwa mahakamani yupo Governor wa Kiambu, Governor wa Tana River, Governor wa Nairobi, Governor wa Kirinyaga n.k unadhani bila katiba mpya kuna fisadi angefikishwa mahakamani.

Kingine imeleta uhuru wa mahakama na uwajibikaji unaweza ona serikali ikileta bajeti isiyoeleweka bunge linakata na Rais Hana la kufanya. Na hata serikali ikifanya maamuzi ya kukopa au mkataba bila kushirikisha bunge (isomeke wananchi) basi hta Bodaboda akipenda mahakamani kuweka zuio serikali inaangushwa na mifano ipo kibao tu.

Kama hujui tokea katiba mpya ifike sasa pesa nyingi zinaenda mashinani yaani kwenye halmshauri kuliko hivi sasa ambapo halmshauri zipo hoi ila serikali Ina mapesa ya kuwekeza kwenye miradi kibao. Huko Kenya pesa zinashuka kwa wananchi na wanajipangia bajeti zao kuendana na mahitaji na competitive advantage ya Jimbo lao!!

So usijaribu kushusha umuhimu wa katiba mpya kwa reference ya Kenya ambavyo ipo miles ahead kwenye uwajibikaji wa serikali na bunge na mahakama.
 
Ukweli ni kwamba, watz wengi hawana kabisa habari za katiba mpya.
Na hata hilo kundi la wanaodai katiba mpya haifahamiki wazi nia yao ni nini hasa?
Na kama tunatamani kujua ukweli, basi kwenye sensa liwepo swali la wanaotaka katiba mpya na kwa nini!
Pasiwe na hamasa yoyote ya kujibu, kila mmoja ajibu kwa uhuru kadri anavyofahamu.

Watanzania wanahitaji maendeleo ikiwa ni pamoja na miundombinu bora ya barabara, maji, umeme, huduma za afya, elimu, usawa na haki! Je, katiba mpya ndio suluhisho la hayo yote?
Wananchi hawataki? Kwa hiyo Mama Samia alipokua naibu spika BMK hawakufika pale sababu ya maoni ya wananchi?

Anyway kuna mambo serikali inaleta bila kuhitaji maoni ya wananchi ila inaangalia tu faida za muda mrefu. Mfano ni lini serikali imechukua maoni kuwa ifufue ATCL, Lini serikali imechukua maoni kuwa ikope kope IMF na AfDB? Ni lini serikali ilisubiri maoni ya mkazi wa Mwangeza au Kinampata kuwa waanzishe wizara ya ICT ama Jinsia?

Uongozi ni initiative sio reactionary, ndio maana Nyerere alikubali vyama vingi licha ya 80% kukataa maana aliona umuhimu wake na alijua ipo siku tu watu watadai hivyo vyama so akachagua kuwa initiative mapema otherwise majaribio ya mapinduzi yangeendelea kutokea tena na tena!!

So kiongozi mwenye vision ana forecast mahitaji sio mpka asubiri mkazi wa Rwenzela asiyejua hta kusoma na kuandika aseme anataka katiba ndio eti alete. Ingekua hivyo maamuzi mengi ya serikali yasingefanyika mpka leo
 
Lakini hao hao wa mitandaoni wasioonekana kuwa na impact ndio walisababisha Twitter kufungiwa kwa miezi almost 7.

Na hao hao wa mitandaoni ndio walisababishs huduma ya internet kuwekwa kapuni na jiwe kwa siku 6 kwenye uchafuzi mkuu.

Kwa ulimwengu wa sasa huwezi narudia huwezi kuidharau nguvu ya mitandao ya kijamii huyu mama kama aamini awaulize watangulize wake mwanzoni walidharau vipi mtandao na nini kilitokea baadae.

Hatuko 2005 sasa eti jambo linatokea tunasubiri hadi kesho either tulisikie redioni au gazetini .
Ila kwa Tanzania au watanzania wengi huko mitandaoni hufuatilia habari za udaku kuliko mambo muhimu ya kitaifa.
 
Hivi kwanini mnaifanya katiba ni zero sum game, yaani ukidai katiba basi hautaki maji na barabara? In fact katiba mpya (Warioba) ingerahisisha hayo kupatikana maana hta wananchi wanaweza kumtoa mbunge midway kma asipotekeleza maendeleo aliyoahidi.

Pia ingeongeza uwajibikaji maana mawaziri wasingetoka bungeni hivyo kutokua na maslahi directly na chama tawala.

Pia wabunge wangechapa kazi kupeleka maendeleo maana hawatokua na option ya kupata uwaziri.

Pia ingesave gharama za uendeshaji serikali maana vyeo vingepunguzwa hivyo kuacha excess funds zikatumike kwa maendeleo.

Yes ingeleta mahakama huru hivyo mafisadi wangekua wanavyooshwa na wizi ungepungua kuliko sasa ambako mahakama inapangiwa mambo na serikali?

Kiufupi katiba ingeleta uwajibikaji hivyo hata hayo maji na barabara wanayotaka upo secured na katiba mpya kuliko hii ya sasa ambao hata bajeti ukiipinga basi bunge linavunjwa.

Yaani chombo ambacho kimewekwa kumsimamia Serikali alete barabara na maji kikiona kuna udhaifu kwenye bajeti kikaigomea basi Anayesimamiwa anaweza kulivunja? Hapo kuna uwajibikaji kweli?
Zitto Jr.

Upo sahihi nami nakubaliana na wewe. Ila kundi linahitaji elimu. Hii nchi ni yetu sote hakuna mwenye uhalali kuliko mtu mwingine. Kuna sheria zimepitwa na wakati na zinahitaji marekebisho ya haraka. Pengine tuwe na Katiba itakayodumu miongo mingi mkuu. 🤝
 
Back
Top Bottom