Kwani, watu wa mitandaoni siyo Watanzania? Rais Samia amejiongoza vibaya!

Sio rahisi kwa CCM wajiue wenyewe kwa kuruhusu mchakato huru wa katiba ufanyike. Ni kama wapewe kisu halafu wajichinje wao wenyewe.
Kwanini wajiue? Kwani katiba mpya inaongelea tu mambo ya chaguzi? Anyway hvi chaguzi zikiwa huru na haki Samia akishinda haoni atawashushua wapinzani wanaodai wanaibiwa Kila siku?

Ndio haya haya ya Lowassa na Membe waliona wataishia CCM milele siku wanahamia upinzani wanagundua umuhimu wa tume huru!!

Hata polepole alijuta kusimamia sheria kandamizi za mawasiliano na takwimu.

Kwa hiyo hata hao CCM wajue watakua Kina Sabaya na Polepole wa baadae hivo waandae mazingira mazuri ili siku mambo yakigeuka wawe na safe haven ya kudondokea.
 
Mnajua demokrasia is a problem?

1. Sii lazima watu wote waamue ila wanoelewa waamue fairly kwa niaba ya wengine! Wakati wa tume ya Warioba kuna baadhi ya wananchi walisema unywaji gongo uhalalishwe na uwe katika katiba mpya eti kwa vile walikuwa nakamatwa kwenye gongo- mawazo ya hawa hawa wananchi ndo demokrasia-....sii sawa!

2. Fairness katika kufanya maamuzi ndo muhimu.. huwezi kuamka asb ukaenda kujenga uwanja wa ndege kijijini mwako bila mtu yoyote yaani bunge wala mahakama kuuliza na kukataa....not fair!

3. Hata huwezi kutumia raslimali za watu milioni 60 Shilingi zaidi trilioni 2 na zaidi huhamia Dodoma tena kwa haraka bila sababu.. these are not fair decisions! Katiba mpya itaweka mipaka ya maamuzi ya mtu au kikundi cha watu kufanya maamuzi hata kama ni kufanya referendum juu ya jambo kabla ya maamuzi. Nani kasema wananchi Igunga wanataka maji au mji mkuu uhamishiwe Dodoma tena kwa haraka na kwa gharama kubwa? Je Wanaigunga waliulizwa?

4. Hoja ya katiba mpya kuweka checks na balances of power katika kufanya maamuzi ni muhumu kwa sasa na vizazi vijavyo na sii hoja ya waliopo ktk social media!!

5. Nawasilisha!
 
Wananchi kuhitaji sio mpaka aseme ila wanapolilia mahitaji Fulani unakua wanahitaji nni.

Mfano mlipolilia bando kupanda bei cjui huduma za kielektroniki ziongezwe n.k ndio serikali ikabuni wizara ya ICT. Ingawa hakuna mtu alisema iletwe wizara ya ICT!!

So mnapolalamika Kila siku kuwa bunge haliisimamii serikali mara chaguzi haziko huru mara viongozi wanaamua mambo alafu wakikosea hakuna kuwajibika n.k hayo yote yanakua summarized kwa neno moja KATIBA MPYA!! Maana ndio itaweka legal framework na institutional independence ya kushughulikia vilio vingi vya waTanzania.
Wengine wanaona tunahitaji kuanza na tume huru na wengine wao wanataka katiba mpya.
 
Wengine wanaona tunahitaji kuanza na tume huru na wengine wao wanataka katiba mpya.
Tume huru bila katiba mpya ni sawa na mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya. Yaani katiba hairuhusu kupinga matokeo ya urais mahakamani je hta tume huru ikiwepo wasipokutangaza huna pakwenda!!

Tume huru ila wakurugenzi (wanaoteuliwa na Mwenyekiti wa CCM) ndio wanasimamia chaguzi!! hapo kuna chaguzi huru?
 
Tume huru bila katiba mpya ni sawa na mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya. Yaani katiba hairuhusu kupinga matokeo ya urais mahakamani je hta tume huru ikiwepo wasipokutangaza huna pakwenda!!

Tume huru ila wakurugenzi (wanaoteuliwa na Mwenyekiti wa CCM) ndio wanasimamia chaguzi!! hapo kuna chaguzi huru?
Sasa hapo tutasema wananchi wanahitaji katiba mpya au tume huru?
 
Ukweli ni kwamba, watz wengi hawana kabisa habari za katiba mpya.
Na hata hilo kundi la wanaodai katiba mpya haifahamiki wazi nia yao ni nini hasa?
Na kama tunatamani kujua ukweli, basi kwenye sensa liwepo swali la wanaotaka katiba mpya na kwa nini!
Pasiwe na hamasa yoyote ya kujibu, kila mmoja ajibu kwa uhuru kadri anavyofahamu.

Watanzania wanahitaji maendeleo ikiwa ni pamoja na miundombinu bora ya barabara, maji, umeme, huduma za afya, elimu, usawa na haki! Je, katiba mpya ndio suluhisho la hayo yote?
Pongezi kubwa sana kwako,na huo ndio ukweli wenyewe,
 
Watanzania wa kawaida hatuitaki katiba mpya ya serikali 3 itatuongezea mzigo wa Kofi

Kama CDM mpo tayari kudai katiba mpya yenye serikali 2 semeni tuwaunge mkono
Kama ni kutokuongeza mzigo au kupunguza mzigo kama utakavyo kwanini isiwe serikali moja badala ya mbili ili kuweka usawa, kama haiwezekani moja ni bora ziwe tatu.
 
Hata waliopo mitandaoni ni Watanzania.

Katiba ni hitaji la wanasiasa wanaogombania madaraka.
Kwahiyo wote wanaopigania katiba mpya mitandaoni(mfano hawa wa humu JF) ni wanasiasa wanaogombania madaraka?
 
Lakini hao hao wa mitandaoni wasioonekana kuwa na impact ndio walisababisha Twitter kufungiwa kwa miezi almost 7.

Na hao hao wa mitandaoni ndio walisababishs huduma ya internet kuwekwa kapuni na jiwe kwa siku 6 kwenye uchafuzi mkuu.

Kwa ulimwengu wa sasa huwezi narudia huwezi kuidharau nguvu ya mitandao ya kijamii huyu mama kama aamini awaulize watangulize wake mwanzoni walidharau vipi mtandao na nini kilitokea baadae.

Hatuko 2005 sasa eti jambo linatokea tunasubiri hadi kesho either tulisikie redioni au gazetini .
Kwenye mitandao ni sehemu ya porojo na kujilisha upepo,hakuna lolote,humu kuna watu walio na hasira za maisha magumu,kuna watu wasomi wasio elimika wasio na kazi na wengine wenye vyeti feki,ukikutana nao humu jiandae,
 
Samia yupo sawa maana watu wa ulimwengu halisi ni waoga sana hawawezi ongea publicly kuhusiana na issue yeyote.

Ni wanafiki mno. Ukizungumza lolote wataishia kukushangaa tu

Ila wakitoka hapo wanakimbilia mitandaoni kutukana.
Sio watu wa ulimwengu halisi,sema wana CCM ndio hawawezi ongea publicly maana ni manafiki balaa.
Kwenda mbele yanataka.
Kurudi nyuma yanataka.
Kwenda kushoto yanataka.
Kwenda kulia yanataka.
CC M ndivyo mlivyo.
Mwananchi mmoja hapa Zuzu -Dodoma aliniuliza,inakuwaje waziri aliyeunga mkono kuwa hatuna UVIKO 19 wakati wa JPM leo anakiri upo na kupokea chanjo na bado yupo ofisini!!???
Jana ilikuwa watoto wa kike wakipata mimba wakiwa shuleni hakuna kurudi kusoma....makofi.
Leo imekuwa watoto wa kike wakipata mimba wakiwa shuleni waendelee na masomo....makofi.
Yapo mengi ambayo CCM hawajui wawe upande upi.
CCM hawana mpango wa kuleta maendeleo kwa nchi hii,wao swala lililopo akilini kwao ni kushinda uchaguzi tu na kuendelea kukaa madarakani ''by all means''.
 
Kwenye mitandao ni sehemu ya porojo na kujilisha upepo,hakuna lolote,humu kuna watu walio na hasira za maisha magumu,kuna watu wasomi wasio elimika wasio na kazi na wengine wenye vyeti feki,ukikutana nao humu jiandae,
Kwanini mitandao ilifungwa kwa siku 6 kuanzia October 28 ,2020?
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Kama haamini Watanzania wanataka katiba mpya uko kwenye Bunge la katiba alifuatwa nini? Tena akawa Naibu Spika... Au alikuwa pale kula posho...!?

Kama Watanzania hawataki katiba mpya hiyo Tume ya Warioba ilitoa wapi hayo maoni wanayotuambia ni maoni ya wananchi.

Watanzania siyo wajinga.
''HUKO KWENYE BUNGE LA KATIBA ALIFUATA NINI TENA AKAWA NAIBU SPIKA''Hii mada ya Mkuu MMM Umehitimisha kwa swali zuri sana, hawa ndio maccm mahili sana kujitoa ufahamu WANAJUA VYEMA katiba ikibadilika tu wao unawatoa nje ya reli.Nguvu yao kuu ni usalama wa taifa ,tume ya uchaguzi na vyombo vya dola kwisha ukivitoa hivyo vyote wanabaki kama watoto yatima wakilia.
 
Tuliwaambia msipende kuwasifia viongozi Ili wasilewe amsikiii. Kusifiwa ni tabia za utoto
 
Martin huna akili kabisa. Wewe unataka kusikilizwa wakati kwa akili zako za kipumbavu huwa mtu akiwa na maoni tofauti unakimbilia kupiga block??!!! Hii tabia kwa CHADEMA unayo sana wewe na Malisa GJ. Mama Samia ana mambo mengi hawezi poteza muda wa kukusikiliza pimbi mmoja kama wewe wakati kuna mamilioni ya watanzania wanamhitaji awaongoze.
 
Back
Top Bottom