Kwani kuotea ndevu nyumbani ndio kigezo cha kufukuzwa? Naambiwa nikajitegemee wanataka (wazazi) nife kwa njaa!

Attelan

JF-Expert Member
Oct 12, 2023
433
697
Kiukweli ukishangaa ya Firauni utayaona ya wazazi wa Ki-Tanzania.

Mimi bado kijana (kwa ninavyojiona), japo udevu ushaniota ni mtu fulani hivi ambaye kiukweli maisha ya kuzungusha bahasha naona ni uduwanzi na nimeamua kukaa nyumbani mpaka muda huu. Nina miaka 27 na mara chache chache navusha demu zangu kwenye geto la nje nililopewa.

Kilinichonishangaza ni kwamba wazazi wanataka niondoke nikajitegemee. Sasa nijitegemee kivipi wakati sina hela? Na nitatokaje wakati sina cha kujilisha huko nje.

Kwasasa nina trade forex nasubiri mambo yakae sawa nipate nauli nikimbilie kwa sisteri ambaye yuko huko Dar Es Salaam ili na mimi nikainjoi mechi kwenye kiwanja cha Mkapa (kuoshaosha macho).

Hivi kweli mzazi unamfukuza mwanao nyumbani je unataka akafie huko huko kwa njaa? Kiukweli nimeumia na nimejua hizi ni siku za mwisho upendo wa wengi umepoa.

Mimi ni mhitimu wa kozi ya Uhasibu. Nasubiri kazi ya Serikali nikunje hata 1M, kuhusu CPA nitasoma nikitulia. Kwasasa nina mawazo nashindwa hata kula.
 
Pole kwa wazazi wako. Mkubwa wewe usijione bado mdogo. Hata kama huna kazi jishughulishe hapo nyumbani na wewe uonekane umo.
Na ndio maana na trade kwa forex. Wao wanaona nalala wakati napambana na wave kila siku natafuta entry
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom