Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,802
- 71,229
Jengo la Tanesco pale Ubungo limejengwa kwa fedha nyingi kwa mabilioni na ni fedha za wananchi masikini wa Taifa hili. Ni kweli mradi wa Fly over ni wa muhimu na ni maendeleo kwa nchi lakini unapoleta maendeleo hupaswi kukurupuka na kuharibu vile vya thamani ulivyokuwa navyo awali. Huo utakuwa ulimbukeni na kukurupuka. Nani kasema Fly over lazima inyooke? Kuliko kuvunja jengo la bilioni kadhaa, zingetumika milioni kadhaa kupata mshauri elekezi kutengeneza mchoro wa kukwepesha barabara kwa juu kwa hiyo section isiyozidi hata mita mia moja. Kuliko kuvunja jengo kama majigambo wakati ni hasara. Mbona wenzetu wanaweza kufanya hivyo? Wataalamu wa kufanya hivyo wapo, tusipende wataalamu rahisi wa kubomoa. Oneni mbona hawa wameweza?