Kwani hakuna uwezekano wa kufanya hivi wakitaka kujenga Fly Over?

20040abc39d7fd4dbf91e1c25603297a.jpg
7e0909f842b75bf605a462b89b31fd66.jpg


Baada ya Rais kutembelea miradi miwili ya ujenzi wa Barabara za Juu maeneo ya Tazara na Ubungo, Rais aliagiza kuwa Makao Makuu ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) lililopo eneo la Ubungo sambamba na jengo la Wizara ya Maji yawekwe alama X tayari kwa kubomolewa kupisha ujenzi wa mradi huo.

Sipingani na Rais yuko sawa katika amri ya kubomoa, ila hoja yangu hakuna uwezekano kufanya kama picha zinavyoonyesha hapa? Maana nijuavyo ni kwamba unajenga Fly Over kuepusha msongamano wa magari wakati huo huo shughuli zingine kama za Ofisi au Kibiashara zikiendelea maeneo hayo. Au hata Ulaya nako wanabomoa majengo wakitaka kujenga Fly Over, Au Ubungo Interchange?

Nawasilisha

==========
Mdau Mwingine
anabalansisha ile imbalansi ya kuvunja Kimara na kutokuvunja Mwanza.
 
Hata zuio la mahakama dhidi ya ubomoaji ilikuwa ni sheria au vipi?.

Kama tuliamua kula nguruwe kwa kutolifuata agizo la mahakama la kuzuia ubomoaji basi tunaweza kula aliyenona zaidi kwa kutafuta njia za kunusuru hilo jengo la thamani ya mabilioni
Umemjibu vizuri sana. Kama tunajinasibu kuwa tunafuata sheria na kuzitii mbona zuio la mahakama lipo kisheria na hatukulitii?
 
Kubomoa kwake ni political mileage. Anadhani anakonga nyoyo za wananchi fukara waliobomolewa nyumba zao
 
Huwezi pitisha njia ya hivyo kwenye lile ghorofa la tanesco kwakuwa itahitaji kuvunja baazi ya nguzo na jengo litapolomoka. Hiyo picha uliyotuwekea ghorofa na hiyo flyover vili dizainiwa kuwa pamoja kabla ya ujenzi.
Unahakika na unachosema au unahisi
 
Ahhhhhh Watu kama nyie hamtaki Maendeleo mnataka sanaaa. Na kama unajua historia Hakuna Nchi iliyoendelea bila kuwa na Iron leader. Kuweni wakweli tu. Nani asiyejua Watz wapenda mteremko. MANENO ndo mtaji wenu Kazi Zero. Swala lilikuwa utaratibu unasemaje hayo majengo toka akiwa Waziri yalitakiwa kutoka ila siasa kama zako ndo zilikwamisha na watu mkasema. Leo siasa hakuna tena mnarudi. Ukitaka TZ iendelee ziba maskio. Wapumbavu na wasanii mi wengi kuliko .kazi yenu Kupinga tu. Hata JPM akitangaza Leo Watu kawaida lazima waende choo mtakuja na uzi kuwa HAMNYI
Mbona Povu jingi ndugu imekuwaje? huyo jamaa yako kuna lipi la Maana alilofanya mpaka sasa zaidi yakuvunja Nyumba za watu!
 
Zuio, sio maana yake zisibomolewe au kwamba hazitabomolewa.
Mahakama kuzuia, ni inaweka mambo fulani sawa as long as zilikuwa ktk hifadhi ya barabara. Kwa hiyo sooner or later zingebomolewa tu.
Kwa huu mchango wako, nasikitika sana kuutangazia umma wa JamiiForums kwamba wewe hautumii akili yako kufikiri!

Ni bora ungekaa kimya kuliko kuonesha upopompo wako mkuu!

Aibu ya mwaka hii!
 
Uko sahihi, ila Sheria ya hifadhi za barabara inasemaje?? Je kuna uonevu wowote?? Mimi kwa mtazamo wangu naona ni sahihi. Wewe kwa mtazamo wako waona sio sahihi.

KUVUNJWA KWA JENGO LITAKUWA SOMO MOJA ZURI SANA KWA WAVAMIZI WA HIFADHI ZA BARABARA.
Mnatumia viungo gani kufikiri? hebu nisaidie kujua unapoishi Kama umewahi kukumbana na Adha yakuvunjiwa Msiongee tu kwakuwa midomo ni mali yenu
 
Tuna mengi ya kushangaza, we fikiria kujenga daraja toka agakhan mpaka kokobichi wakati pesa hiyo ingejenga flyover ya hatari pale selander. nakubaliana na Ghazwat kwamba umasikini wetu ni wa kujitakia
Salenda hakutakuwa na folen kubwa kama la koko likijengwa
 
20040abc39d7fd4dbf91e1c25603297a.jpg
7e0909f842b75bf605a462b89b31fd66.jpg


Baada ya Rais kutembelea miradi miwili ya ujenzi wa Barabara za Juu maeneo ya Tazara na Ubungo, Rais aliagiza kuwa Makao Makuu ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) lililopo eneo la Ubungo sambamba na jengo la Wizara ya Maji yawekwe alama X tayari kwa kubomolewa kupisha ujenzi wa mradi huo.

Sipingani na Rais yuko sawa katika amri ya kubomoa, ila hoja yangu hakuna uwezekano kufanya kama picha zinavyoonyesha hapa? Maana nijuavyo ni kwamba unajenga Fly Over kuepusha msongamano wa magari wakati huo huo shughuli zingine kama za Ofisi au Kibiashara zikiendelea maeneo hayo. Au hata Ulaya nako wanabomoa majengo wakitaka kujenga Fly Over, Au Ubungo Interchange?

Nawasilisha

==========
Mdau Mwingine
Mh Rais JPJM msikilize Ghazwat kama yeye kachora huu mchoro
 
View attachment 631659

Siju ni wangapi walishaliona hili udogoni, kulikuwa na watoto waharibifu na wenye matumizi mabaya na vitu.... Watanunuliwa michezo nguo nk lakini vitu vyao ndio vitakuwa vya kwanza kuharibika ama kupotea... Hii hali inaendelea mpaka shuleni na hatimaye Kwenye maisha ukubwani

Tumeshashuhudia pia maranyingi Kwenye magari mmoja ana gari namba A na mwingine ana gari namba D, lakini utakuta namba A ni mpya kuliko D, hizi ni roho za uharibifu, roho za kuangamiza, roho za kufuja... Watu hufuja mpaka wenza wao, mwaka mmoja wa ndoa unakuta mwanamke kachakaa kabisa

Kila jambo lina kinyume chake, ukijaaliwa roho ya kutunza mwenzako atajaaliwa roho ya kuharibu.. Hizi ni nguvu zilizo juu ya utashi na uwezo wetu, hatuwezi kuzi control... Hivyo mwenye kipawa cha kutunza hiyo ni tunu hapaswi kumcheka mwenye roho ya kuharibu... Mungu ndio huchagua ampe nani na ampe nini!

Mwenye roho ya kuharibu hafanyi hivyo kwa makusudi, ana nia njema tena thabiti hasa lakini matokeo ya maamuzi kusudiwa hugeuka kuwa hasi... Na hata akitaka kufanya jambo jema kabisa halitimii kwa ukamilifu ama huwa na hasara nyingi kama si mapungufu...

Habari za kubomolewa wizara ya maji na jengo la Tanesco ubungo kupisha ujenzi wa barabara za mzunguko limepokelewa kwa mshtuko na wengi na kumekuwa na maoni na mijadala mingi mitandaoni...

Mshtuko huo umewafanya wengine waanze kuhoji kuwa kuna nini kinaendelea katika ulimwengu wa kiroho

Wanahoji
Matokeo ya kesi ya meli ya samaki yalikuwaje
Matokeo ya Kivuko cha MV Dar es salaam
Matokeo ya Ndege za bombadia
Matokeo ya Barabara ya Morocco mwenge
Matokeo ya Bomoabomoa kimara
Matokeo ya Dhahabu na makinikia
Matokeo ya vita dhidi ya rushwa nknk
Kuna baadhi ya mambo ni coincidence tu yasiyo na uhalisia wowote lakini watu hupenda kuyaweka kwenye mizania ya uhalisia na mijadala huanzia hapo
Inshort ni kuwa kama liko barabaran na barabara inabidi itanuke mpaka apo
Halina budi kuangushwa

Tatizo watu wana ushabiki
Ata mie ningekuwa simkubali jamaa ningepinga2
Naona anania njema sana na sababu kubwa na nzr ila ndo hvyo watu wana hoja za kijingakijinga2 kupinga
Kweli hilo jengo ni kivutio
Lkn kujenga hilo jengo ni bilion40 bwa uchumi wa sasa kitu ambacho ni sawa na walivyokuwa wakiilipa richmond ya utapeli kwa miez3
 
Mumempa jina la Bulldozer, hata kwenye habari za BBC zinapomzungumzia lazima zimpe sifa hii ya Bulldozer. Sasa anafanya kile Bulldozer linachoweza kufanya. Wengine wanamwita kichwa cha pasi, pasi kazi yake ni kunyoosha tu na watu wananyooka sasa. Mkitaka apunguze kasi mwiteni Povu la soda, tena fanta halivuki ata chupa....
Walishajaribu kumuita hapo mwanzoni hilo jina, it didnt take long wakagundua JPM ni mumber nyingine kabisa! kupunguza speed sahau, labda kuongeza.
 
unaanzaje tu kupitisha barabara katikati ya jengo...load ya hiyo flyover ilijumlishwa wakati ilo ghorofa linajengwa???????
Jengo halikuguswa hapo na wala mtikisiko unaosababishwa na magari hautikisi jengo hata kidogo.Wonderful engineering.
 
Watabomoa kama wanavyotaka, ila lazima swala lijadiliwe kwamba kulikuwa na alternatives, nawo waelewe hivyo, hii ndio JF, mazuri yatapondwa, mihemko naye lazima ile knuckles, tuna discuss, huwa wanapita humu, itasaidia siku nyingine wanapotaka kukurupuka kufanya jambo watulize akili na brainstom kwanza..
 
Hiyo budget ya kujenga jengo jipya je?, vipi kuhusu kuhamisha hiyo mitambo? Hakutakuwa na katizo la umeme kipindi cha kubomoa na kuhamisha plant? Hasara za kiuchumi na kijamii zitakazotokana na katizo la umeme (kama litakuwepo)? Waangalie vyema/upya cost benefit analysis.
Tunapaswa kujua kuwa kurekebisha uhovyo tuliokuwa nao ni lazima maumivu yawepo. Hoja yako ni kama ya LOWASA eti hawa wenye vyeti feki wana familia na eti familia zao zitaathirika. No wacha ziathirike lakini Nchi na serikali ni lazima irudi kwenye mstari sahihi - Tunataka Tanzania Mpya kwa tulipokuwa tumefikishwa ili kurekebisha MAUMIVU hayakwepeki mkuu.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom