Kwamba Mzee Warioba, Butiku, Shivji, Bagonza, Pengo, Kitima wamelipwa kukataa Mkataba wa DP World?

Wanaokuja na madai hayo wanathibitisha kuwa ni mabogazi vichwani.
Kama wanaweza kuwa na uhakika wa hayo madai yao hawaoni kuwa wanazidi kuonyesha kuwa serikali wanayoitetea ni dhaifu na imelekea kama uzi? Kama kuna watu wamehongwa, je serikali ipo wapi??? Inarembuarembua tu au?
Aste Aste
 
Hao wezi waliokuwa wananufaika na Bandari wana nguvu sana; kama wameweza kumwonga na kumshawishi hadi Waziri Mkuu mstaafu Jaji Warioba , Mzee Butiku ambao ni wazee wa CCM nani tena watashindwa kumwonga?

Kwa taarifa zilizotoka hivi karibuni zinaonyesha wanaopinga mkataba huu ni wezi waliokuwa wananufaika na Bandari na kwamba wanatumia nguvu kubwa kuwahonga wananchi kupinga nia nzuri ya serikali.

Nini mtizamo wako kuhusu version mpya ya utetezi iliyoanzishwa na serikali? Hao wanaohonga ni wakina nani? Niwatanzania wenzetu? Kwanini serikali inashindwa kuwashtaki Kisutu? Je, wakishindwa kuwapeleka Kisutu watawezana na huyu bwana mwenye mkataba wakwenda kuishtakiwa Uingereza au South Afrika?

Kila siku tunatiwa hatiani huko ulimwenguni je tunapokwenda kumwabudu binadamu aitwaye DP World tutamdhibiti vipi asihonge?
Mwenzao Rostam Aziz alipoisema vibaya mahakama, aliomba msamaha mapemaa..!!! Hapa inabidi hao wanaoambiwa kuwa wamehongwa, huyo anayesema hivyo apelekwe mahakamani akathibitishe.
 
Hao wezi waliokuwa wananufaika na Bandari wana nguvu sana; kama wameweza kumwonga na kumshawishi hadi Waziri Mkuu mstaafu Jaji Warioba , Mzee Butiku ambao ni wazee wa CCM nani tena watashindwa kumwonga?

Kwa taarifa zilizotoka hivi karibuni zinaonyesha wanaopinga mkataba huu ni wezi waliokuwa wananufaika na Bandari na kwamba wanatumia nguvu kubwa kuwahonga wananchi kupinga nia nzuri ya serikali.

Nini mtizamo wako kuhusu version mpya ya utetezi iliyoanzishwa na serikali? Hao wanaohonga ni wakina nani? Niwatanzania wenzetu? Kwanini serikali inashindwa kuwashtaki Kisutu? Je, wakishindwa kuwapeleka Kisutu watawezana na huyu bwana mwenye mkataba wakwenda kuishtakiwa Uingereza au South Afrika?

Kila siku tunatiwa hatiani huko ulimwenguni je tunapokwenda kumwabudu binadamu aitwaye DP World tutamdhibiti vipi asihonge?
Hebu elezea kidogo tujue walikuwa wananufaikaje na Bandari zetu.
 
Pengo
Kitima
Bagonza ..
Hawahitaji kuhongwa ...wao Wana uadui wa kiimani na waarabu....

Shivji haihitaji kuhongwa,Shivji ni Communist ndo maana wala hasemi mkataba urekebishwe ..anasema serikali ifanye kazi hiyo...haelewi dunia ya sasa hata serikali za Uingereza na Ujerumani zimebinafsisha bandari...
Shivji kabaki Karne ya 20...ya kina Nyerere na Mao Zedong...na Lenin ..

Warioba na Butiku wanahitaji anything wawe relevant....hawa ni wazee wa Karne ya 20... Hardliners conservative...wafuasi wa Nyerere....
Hawa wote wanaongea wanayo yaamini huku Karamagi akiwalainisha na kuwapa nguvu financially
Nimejaribu kuwaza, najiuliza maswali yafutayo;

1. Wale mashehe ambao nao waliukosoa mkataba/makubaliano ya Tanzania na DPW, nao wana uadui wa kiimani na waarabu?

2. Wanaohoji kuhusu mkataba huo ni wazee pekee? Hakuna vijana wanaohoji?

3. Wanaohoji kuhusu mkataba huo, ni wasio waislamu pekee? Kwamba hakuna muislamu anayehoji?

4. Mtu kuwa conservative, maana yake kila kitu atakosea? AU anakuwa hajui kitu?

CC Pascal Mayalla
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
wakati wao hawana hata kontena moja la nguo wanalohangaika kulitoa hapo bandarini.
Wewe unaongea nini?
Nimekwambia wazee wanatetea bandari ibaki kwa wananchi,hayo malonyalonya unaita nguo huwezi hata kujua hawa wazee wanachotetea?
We unatoa dharau kwao na hiyo mitakataka toka china.
Mbona wamesema kwa busara tu.
Mkataba unaweza kufanyika ila kuna vipengele virekebishwe.
Wangekua na tamaa na makabaila
km wewe hiyo nafasi yako kuleta mzigo wangejaza kijiji chao kizima na ndugu zao na watoto km wanavyofanya wengine.
We usingekua au kupata chance kuleta hizo taka.
 
Pengo mnufaika wa kwanza, hao wengine wameshazeeka na wwananukuliwa vibaya na au wanaongozwa wajibu nini na waandidhi walionunuliwa.
Bibie hili sakata la DPW limekufanya mpaka uwe unakosea sana kuandika,ulivyo hodari wa kukosoa wenzio wakikosea tu hata herufi moja.Basi uwe unatulia unatuandikia maneno kwa usahihi ili usomeke na ueleweke vizuri.
 
Katika kutengeneza hakikisha una nguvu ya kuamua juu yao..america theory hiyo . Mark Zuckerberg anaitwa na senate au Google ceo. Bill Gates anaamuliwa nini cha kufanya duniani aseme nini. Kifupi control ndio inapiganiwa sio operation issues. Uendeshaji hawa wazee yaweza kuwa hata email hawajui kutumia natania. Issue ni control ili uweze kuamua leo nafanya hivi kesho ondoka na pia Fiscal na Monetary policy. Kumbuka uwekezaji endelevu hizingatia social acceptance. Kifupi tunapenda kuendelea kuwa na maamuzi kwenye shamba letu sio kulima.
Mijadala inachukua muda mrefu sana na kila mtu ni mjuaji kuliko mwingine.

Majirani zetu wanatafuta mbadala wa bandari yetu, inasikitisha iwapo tutapoteza wateja wa reli iliyojengwa kwa trilioni 17 kwa sababu tu ya kuendekeza mdomo zaidi kuliko maamuzi yenye faida kwa uchumi wetu.

Tumekuwa nchi fulani ya wapumbavu sana katika miaka hii 25 ya mwisho, tofauti kabisa na mawazo pamoja na malengo waliyokuwa nayo waasisi kina Julius Nyerere na Mzee Karume.
 
Wewe unaongea nini?
Nimekwambia wazee wanatetea bandari ibaki kwa wananchi,hayo malonyalonya unaita nguo huwezi hata kujua hawa wazee wanachotetea?
We unatoa dharau kwao na hiyo mitakataka toka china.
Mbona wamesema kwa busara tu.
Mkataba unaweza kufanyika ila kuna vipengele virekebishwe.
Wangekua na tamaa na makabaila
km wewe hiyo nafasi yako kuleta mzigo wangejaza kijiji chao kizima na ndugu zao na watoto km wanavyofanya wengine.
We usingekua au kupata chance kuleta hizo taka.
TICTS wamekuwa wawekezaji pale Bandarini kwa miaka 22, mbona haijawahi kuondoka mikononi mwa wananchi?.

Tatizo la sasa ni kwamba kuna wenye maslahi wanakwenda kupotezwa kabisa iwapo mfumo wa kuiendesha utakuwa mwingine tofauti na huu wa sasa.

Hao wazee na wao wanapitwa na wakati tena kwa kasi kubwa, wanachoshindwa kujiuliza ni kwamba pato la bandari linapoongezeka hata wao pesa za kuwatunza na familia zao zinaongezeka pia. Mipango ya kitaifa tunaiwezesha kwa pesa za ndani za kwetu wenyewe.

Tatizo wanakuja kujipotezea heshima yao uzeeni, japo sijui wamelipwa kiasi gani cha pesa na hao wapigaji wa bandarini.
 
Mijadala inachukua muda mrefu sana na kila mtu ni mjuaji kuliko mwingine.

Majirani zetu wanatafuta mbadala wa bandari yetu, inasikitisha iwapo tutapoteza wateja wa reli iliyojengwa kwa trilioni 17 kwa sababu tu ya kuendekeza mdomo zaidi kuliko maamuzi yenye faida kwa uchumi wetu.

Tumekuwa nchi fulani ya wapumbavu sana katika miaka hii 25 ya mwisho, tofauti kabisa na mawazo pamoja na malengo waliyokuwa nayo waasisi kina Julius Nyerere na Mzee Karume.
Come clean mzee.
 
Mkataba wa ticts unafanana na huu sio. Air land and water and forever. Remove hivyo vipengele then waendelee. Mbona uk wapo wanapiga kazi. Na huwezi

Kwa nini msijenge bagamoyo port kama mpango wa awali ili mlishe sgr. Tunapoteza biashara kwa mengi sio operation efficiency tu hata mindset zetu ambazo hatuzipi kazi ya kufikiri. Tunataka vitu kwenye sahani vimepayikanaje hatujui. Na je una uhakika kuwa una kipato kidogo au matumizi mabovu?
 
Pengo
Kitima
Bagonza ..
Hawahitaji kuhongwa ...wao Wana uadui wa kiimani na waarabu....

Shivji haihitaji kuhongwa,Shivji ni Communist ndo maana wala hasemi mkataba urekebishwe ..anasema serikali ifanye kazi hiyo...haelewi dunia ya sasa hata serikali za Uingereza na Ujerumani zimebinafsisha bandari...
Shivji kabaki Karne ya 20...ya kina Nyerere na Mao Zedong...na Lenin ..

Warioba na Butiku wanahitaji anything wawe relevant....hawa ni wazee wa Karne ya 20... Hardliners conservative...wafuasi wa Nyerere....
Hawa wote wanaongea wanayo yaamini huku Karamagi akiwalainisha na kuwapa nguvu financially
udini umekudhalilisha sana !
 
Uingereza na ujermani wamebinafsisha kwa 25% tu wao kama nchi wamebaki na 75% na wana maamuzi juu ya bandari zao, ninyi mazuzu hamuelewi mna asilimia ngapi maana MOU yenu haiwapi hata nafasi ya kuamua maamuzi yoyote juu ya bandari hadi ruhusa mkaombe kwa waarabu, yaani hata mkitaka kufunga rada mtaenda kuomba ruhusa wajinga ninyi
 
Na hao waTanzania wengine wanaosoma nyaraka ya "Makubaliano" na kuielewa kwa uovu uliomo humo ndani unawaweka fungu gani?

Sawa, tukubali akina Pengo na wenzake, umesema "hawahitaji kuhongwa...wao wana uadui wa kiimani na waarabu"; na wewe je?
Huhitaji kuhongwa kwa vile una urafiki na waarabu; kwa kushinda kutwa ukitetea kila kitu ambacho wengine wanaona kina kasoro?
Udini wa huyo jamaa hata shetani anashangaa !
 
Hata kama ni wasaidizi wake yeye Hana akili? Yeye Hana mamlaka ya kubatilisha anachoona hakiko sawa? Sema ameamua tu kuwakabidhi wajomba zake Mali za Tanganyika ijulikane bhas na watanzania bara hawapo tayari kuona hilo likifanyika pasipo maslahi ya nchi kuwekwa bayana.
Watanzania bara wa sasa ni tofauti na wale walioko kipindi cha Mwinyi akiwa raisi wa JMT hii ileweke.
Watanzania bara walishaupoteza Utanganyika wao, hivyo hakuna mali za watanzania bara wala watanganyika.
Kwani Bunge si lina watanzania bara wengi, mbona husikii wakilalamika.
Ila kuna kauli kaizungumza mzee Butiku - kuna .......hata tunaodhani wamekubali pengine hawakukubali.
Kama ni kweli, basi kumbe kuna wabunge wameburuzwa
 
Rushwa inapunguza uwezo wa kufikiri. inapunguza utu na heshima ya mpokeaji.
Mtu kama wewe siyo wa kutetea mambo ya ajabu kama makubaliano haya ya kukabidhi bandari , ardhi, n.k. kwa DP World.
Unaujuwa ukweli tatizo siyo kuwapa wawekezaji bandari, tatizo siyo DP World bali kilicho andikwa kwenye mkataba/makubaliano.
Rushwa inapofusha macho ,
 
Hao in timu moja kila hoja ikitokea wanjipanga kuipinga kwakudanganya kwamba wametumwa na sisi wananchi wakati hawana idhini yetu.

Muhimu hapa hoja ziko mbili na kila mmoja anayo haki ya kutetea hoja yake mwisho mshindi atapatikana baada ya kuona nani mwenye hoja yenye Mashiko.
 
Mkataba wa ticts unafanana na huu sio. Air land and water and forever. Remove hivyo vipengele then waendelee. Mbona uk wapo wanapiga kazi. Na huwezi

Kwa nini msijenge bagamoyo port kama mpango wa awali ili mlishe sgr. Tunapoteza biashara kwa mengi sio operation efficiency tu hata mindset zetu ambazo hatuzipi kazi ya kufikiri. Tunataka vitu kwenye sahani vimepayikanaje hatujui. Na je una uhakika kuwa una kipato kidogo au matumizi mabovu?
Huu ni mkataba mkubwa na wa kisasa. Mindset ni tatizo kubwa kwa maana ya watu kukosa ufahamu wa kipi kinachokwenda kufanyika na pia kuwepo kundi fulani la watu wanaofaidika na hizo biashara mfano za ICDs pembeni ya Port hawa ni tatizo kubwa kwani wanatumia nguvu kubwa mpaka ya hawa wazee wanasiasa wastaafu ilimradi waendelee kupotosha na kujificha kwenye siasa za uzalendo wa kuidai Tanganyika.

Hata hiyo Bagamoyo Port ilipingwa na hayati JPM tena mbele ya mkutano wa wafanyabiashara. Suala la bandari litapatiwa tu suluhisho japo muda huwa hauna urafiki kwa mipango ya binadamu.
 
Uingereza na ujermani wamebinafsisha kwa 25% tu wao kama nchi wamebaki na 75% na wana maamuzi juu ya bandari zao, ninyi mazuzu hamuelewi mna asilimia ngapi maana MOU yenu haiwapi hata nafasi ya kuamua maamuzi yoyote juu ya bandari hadi ruhusa mkaombe kwa waarabu, yaani hata mkitaka kufunga rada mtaenda kuomba ruhusa wajinga ninyi
Mikataba iliyosainiwa Uingereza ni tofauti na hii inayokwenda kusainiwa huku TZ. Usiite watu mazuzu wakati bado mikataba ya kibiashara haijasaniwa, huko ndiko tunapokuwa na sauti katika mijadala ya kibiashara.

Linapita azimio la bungeni haujapita hata mkataba mmoja wa kibiashara kati ya DPW na Tanzania.
 
Hao wezi waliokuwa wananufaika na Bandari wana nguvu sana; kama wameweza kumwonga na kumshawishi hadi Waziri Mkuu mstaafu Jaji Warioba , Mzee Butiku ambao ni wazee wa CCM nani tena watashindwa kumwonga?

Kwa taarifa zilizotoka hivi karibuni zinaonyesha wanaopinga mkataba huu ni wezi waliokuwa wananufaika na Bandari na kwamba wanatumia nguvu kubwa kuwahonga wananchi kupinga nia nzuri ya serikali.

Nini mtizamo wako kuhusu version mpya ya utetezi iliyoanzishwa na serikali? Hao wanaohonga ni wakina nani? Niwatanzania wenzetu? Kwanini serikali inashindwa kuwashtaki Kisutu? Je, wakishindwa kuwapeleka Kisutu watawezana na huyu bwana mwenye mkataba wakwenda kuishtakiwa Uingereza au South Afrika?

Kila siku tunatiwa hatiani huko ulimwenguni je tunapokwenda kumwabudu binadamu aitwaye DP World tutamdhibiti vipi asihonge?

“Kwa taarifa zilitoka”
Zimetoka wapi? Ukiwa na vielelezo na ushahidi prove ulichokiandika.

Id mpya mpya kama za kwako halaf unakuja na hoja nyepesi? Unataka watu waamini maneno?
Empty words? Kwenye dunia hii ya science and tech?

Kuwa serious
 
Back
Top Bottom