Kwako Waziri wa Afya: Matatizo matatu ya Hospitali ya Muhimbili na Mloganzila ni haya

Ul
Mheshimiwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, hizi ni Hospitali pacha zenye uzoefu wa uzembe zina matatizo haya matatu;
  1. Madaktari Wazoefu kuhangaikia Hospitali za Mitaani kuliko mwajili wao
  2. Kuwatumia Wanafunzi kujifunza bila Daktari mzoefu mbele ya mgonjwa
  3. Madawa ’feki’ kwa wingi ndani ya Hospitali
Madaktari wako hospitali za Umma kama Kituo cha kutafuta Wateja na kuwaelekeza kwenye vituo vyao vya mitaani ikiwa ni pamoja na Hospitali za binafsi. Kuna sababu gani ya kuendelea kuruhusu Daktari kuhudumu Hospitali za mitaani? Je, Askari Polisi au Askari Jeshi anaweza pia kuhudumu Kampuni Binafsi za Ulinzi?

Nasikia NHIF wanawalipa kutokana na malipo ya Mgonjwa hii ni hatari! Inawafanya kujiingiza kwenye tiba kubwa hata wasizoziweza ili tu wapate pesa

Wanafunzi wamefikia hatua ya kufanya mitihani mbele ya Mgonjwa ambaye hajapewa huduma lakini anatumiwa kama Kituo cha mtihani. Bila hata kuomba samahani, ukiwa hospitali Daktari anajiona kama anakumiliki, ni specimen yake.

Kuna madawa ’feki’ mengi yako kwenye maduka ya hospitali hizi. Yaonekana ni kwa sababu kuna Wagonjwa wengi na waletaji wana dili zao na wahusika.

Mara nyingi utapewa dawa inayoaminika kufanya vizuri katika ugonjwa lakini ukitaka usalama bora ununue ya maduka ya mitaani

Utawala wa hospitali ujiangalie upya! Hili siyo kutafuta sifa.
Uliyoyaandika hapa mkuu ni karibu hospitali zote nchini dispensary na vituo vya afya
 
Hawa ni watu wa kusamehewa nchini mkuu. Hawa cku zote wanaamini siasa kuliko utu. Hawa ndio watesaji na wauwaji wa yeyote atakayesema ukweli. Kiufupi hawana utu hata kidogo. Wanaamini serikali wanayoishabikia siku zote iko sahihi bila kujua kuwa serikalini pamoja na ndani ya vyama vya siasa kuna wanasiasa ambao kiu yao kubwa ni sifa, utajiri na nguvu ya kukandamiza wengine.

Kikubwa ni kuwapuuza tu na kuungana na wengi ambao ni wapenda maendeleo na wanaokosoa ili marekebisho yafanyike ubora uonekane.

Kuliko kujibu comment zao ni bora kutumia muda huo kuendelea kuwashauri wasikivu na wapenda maendeleo
Wanaotoa Taarifa kama hizi wanao Ushahidi na mimi pia nimewahi kushuhudia baadhi ya kasoro zilizo wekwa wazi hapa ,mambo ya Chama weka pembeni ili tuondoe Tatizo.Habari ya kusifia sifia tu kwenye Maisha ya Watu achana nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mod. hebu tuvumilie kidogo. Tujadili hospitali zetu badala ya barua ya mtu anayeitwa profesa na mkurugenzi.

Tabia za madaktari wetu ni hovyo na hasa kwa mtu ambaye umeshuhudia madaktari wa nchi zilizoendelea. Madaktari wetu bado wana tabia ya sekondari kuamini kwamba kazi yao ni bora kuliko za wengine dunia hii. Wanadeka na kila wakati wanataka kukuonesha kwamba wewe ni mbumbumbu.

Tabia ya kazi zao nje ya mwajili wao ni hatari kwa ubora wa afya za watu. Kuna baadhi wanajiita maprofesa lakini unawakuta saa za kazi wako mitaani upanga kwenye vyumba swa na kioski, wakikusanya elfu kumi kumi! Siyo sababu ya maisha magumu ila ni kutojitambua na tamaa iliyowajaa!

Madawa feki ni kweli kabisaaa! Ymejaa sana hospitali za serikali. Maduka ya mitaani pia yapo lakini hospitali ni zaidi! Nadhani ni kwa kuamini huko wateja ni wengi.
Tatizo ni pana kuliko unavyo lieleza
 
Tatizo mloganzila ni kuitenga na hospitali ya taifa muhimbili. kimapato na taaluma. Inatakiwa iwe hivi. Idara ya medicine na vitengo vyake mkuu wa idara either akae mloganzila makamu muhimbili upanga.Wafanyakazi wapangwe kwa zamu mwezi mmojamoja.Pia account iwe moja ya hospitali. Siyo leo wanalopa allowance mihimbili upanga ; mloganzila hakuna kitu.Wafanyakazi wanapoondolewa muhimbili upanga kupelekwa mloganzila wengi wanaona kama wameonewa.Chonde idara ziwe mmoja siyo kuwagawa.Utaratibu wa zamu ufuatwe pale.
 
Wacha siasa mkuu. Wanaoandika mambo haya wameyaona. Mnavyoendelea kuona kuwa kila anayekosoa ni upinzani basi tutaja stuka kuwa maisha ya watu yanaendelea kupotea kizembe.

Nimewahi kukuta hii hali kwenye hospitali moja kubwa hapa nchini. Wakati huo mtoto wa ndugu yangu alikua na tatizo la figo. Lakini walikuja madaktari wanafunzi kibao kila mmoja anatoa suggestions za vipimo avijuavyo yeye na tuliwasikiliza. Wapo hadi walioshauri afanyiwe x ray ya kifua (cjui ni kwa nn lakini tulifanya)

Ilitokea daktari mmoja mkenya ndiye aliyetustua kuhusu hili. Yeye ndiye aliyekua anashughulika na huyu mtoto na mwisho wa siku alikuta msururu wa vipimo kwenye file. Na hii ni baada ya kuwa tayari tunefanya CT SCAN ambacho ndicho kipimo kilichokua na umuhimu ili dogo afanyiwe upasuaji. Yeye ilibidi atoe mawasiliano yake ili kila tulipokua tunahudhuria hospitali tumtafute ili wale wanaokuja kusomea pale kwenye mwili wa dogo wasitusumbue tena. Hili ndilo lililosaidia dogo kutibiwa kwa haraka.

Kwa hiyo ukweli upo kuwa wanasomea kwenye miili ya wagonjwa. Maana huyu docta alitudokeza kwamba suggestions za vipimo walivyoshauri vifanyike vikionekana vina ukweli basi wanafaulu.

Cku pia dogo anafanyiwa upasuaji tulitakiwa tutoe damu. Wakaja tena wajifunzao kutoa damu. Waliniwekea lile lisindano kwenye mshipa ambao sio mpaka alipokuja muhusika wa kitengo kile. Nilishuhudia akiwaelekeza jinsi ya kutoa damu kwenye mkono wangu (Nikawa specimen chaap) Kiukweli nilitaka kugoma kutoa ila ilibidi nitoe kwa kuwa mtoto ni lazima apone. Tunamshukuru Mungu kuwa alifanyiwa upasuaji salama na figo ilokua na shida iliondolewa.

HAYA MAMBO YANA UKWELI KWA HIYO ACHA YASEMWE WANANCHI WAPONE. UKIWEKA SIASA MBELE, WATU WATAKUFA. AU ILI NIKUFURAHISHE ACHA NIKWAMBIE KUWA "KURA ZITAPUNGUA" KWA SABABU MNAJALI KURA KULIKO WAPIGA KURA.

NAOMBA KUWASILISHA NA WEWE UBADILIKE
Hakuna huo ujinga awamu ya tano, watu wamenyooka sasa nidhamu imerudi kwenye maofisi na watu wanachapa kazi balaa..
Nyie mtakuwa CDM..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iyo spitali nuksi sana.jamaa yagu moja kidogo akufie pare pare.selikali iiagalie jabo ili.
 
Bado tanzania hamjali afya. Hawa watu ni muhimu sana ila hawajaliwi. Kuna hospital wahudumu wanaingia zamu si zao ila bado malipo hamna wanasema wajitolee tu. Hivi nyie mnapilipana posho kwenye kusinzia na kugonga meza na huku mnataka wahudumu wetu wa afya wasilipwe mnategemea nini. Badilikeni wajalini hawa watu ili nao wawe na moyo wa kutuhudumia
 
waziri fukuza kazi bodi ya wakurugenz yote ya mhimbili wameshindwa kusimamia wafanyakaz wao
Hii umenikumbusha jambo niliosikia na kuona ni ajabu sana!! Eti mkuu wa bodi ya Muhimbili ni yule mkuu wa chuo cha Bugando. Unawezaje kuendeshwa na mkuu wa taasisi nyingine ambayo nayo inahitaji kurekebishwa. Hii ni sawa na IBM imtake mkuu wa Mac awe m/kiti wake. Watajidai hizi siyo biashara lakini mpangilio wa aina hiyo hauleti tija. That is suicidal and inbreeding of weaknesses.
 
Hakuna huo ujinga awamu ya tano, watu wamenyooka sasa nidhamu imerudi kwenye maofisi na watu wanachapa kazi balaa..
Nyie mtakuwa CDM..
We utakuwa ni Ummy nini? Ujinga gani? Madaktari hawatoi huduma hospitali na dispensary binafsi? Hakuna madawa feki? Wanafunzi hawatoi huduma za kitabibu?
Stupid!
 
Hakuna huo ujinga awamu ya tano, watu wamenyooka sasa nidhamu imerudi kwenye maofisi na watu wanachapa kazi balaa..
Nyie mtakuwa CDM..
Hapana mkuu.
Weka siasa pembeni kwenye suala la afya ya watu.
Asemayo mengi yana onekana yana ukweli.
Ingawa napenda kupingana nae hoja ya kutaka kuwazuwia madaktari wa hospital za umma wasifanye kazi muda wa ziada hospitla za binafsi.

Mkuu tunajuwa hispital zetu za rufaa ni chache sana, wagonjwa wanao hitaji kupata huduma za daktari bingwa ni wengi mno na miundombinu za hospital za rufaa za umma haiwezi kuhudumia wote ndani ya muda sahihi kitabibu.

Kufanyiwa upasuaji na daktari bingwa pale MNH inaweza kukuchukua siku nyingi wakati daktari huyo huyo anaweza kukufanyia upasuaji hospital nyingine kubwa za binafsi (nisingependa kuzitaja), tatizo Vifaa na vyumba vya upasuaji ni vichache kuliko idadi ya wagonjwa hapo MNH na hospital zingine za serikali.

Wanatupunguzia mateso na vifo vingi kwa kuendelea kutoa huduma ktk hospital binafsi kwa haraka.
 
Hakuna huo ujinga awamu ya tano, watu wamenyooka sasa nidhamu imerudi kwenye maofisi na watu wanachapa kazi balaa..
Nyie mtakuwa CDM..
Bila shaka hujakumbana hizo kadhia ndio maana unapata ushujaa wa kuandika maneno kama hayo ukiletea siasa ndani yake.
 
Hili tangazo la lishe ya watoto wa umri kuanzia miezi miwili na bei yake shilingi mia mbili hivi waziri Dr. Umi Mwalimu analusikia?

Mbona anaruhusu watoto wachanga kulushwa vitu badala ya nyonyo la mama?

Na je atakuwa na uhakika gani kuwa wachakachuaji hawawezi haribu afya za watoto?

Naomba mniulizie kwa Dr. Umi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi waziri mwenye dhamana kumbe naye ni Dr. ?Sasa sijui ni MD au PhD.
 
Sijui ni wapi kuna ahueni kati ya hizo hospitali za serikali na binafsi. Maana unaenda hospitali binafsi tena kubwa ambayo inatoa huduma za aina fulani lakini inategemea wataalamu kutoka hospitali za serikali ambao nao unakuta wanahudumu hospitali zaidi ya moja. Mgonjwa inabidi apangiwe ratiba kutokana na ratiba ya daktari na sio hali yake. Daktari naye siku akifika anakutana na majukumu mengi hali inayofanya baadhi ya wagonjwa wasipate huduma kwa wakati. Pindi mgonjwa anapozidiwa anapelekwa tena hospitali za serikali. Pasipo umakini katika hii sekta tutashuhudia mengi sana.
 
Mheshimiwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, hizi ni Hospitali pacha zenye uzoefu wa uzembe zina matatizo haya matatu;

Kuna madawa ’feki’ mengi yako kwenye maduka ya hospitali hizi. Yaonekana ni kwa sababu kuna Wagonjwa wengi na waletaji wana dili zao na wahusika.

Mara nyingi utapewa dawa inayoaminika kufanya vizuri katika ugonjwa lakini ukitaka usalama bora ununue ya maduka ya mitaani

Utawala wa hospitali ujiangalie upya! Hili siyo kutafuta sifa.


MKuu hizi feki zinatoka MSD ?
 
Hili Bandiko Natabiri Kuja Kukanushwa Na Wizara/Muhimbili National Hospital Vikali Sana.
Ingawa Mleta Mada Yupo Kwenye Kusema Ukweli Ambao Haubishaniwi Ataambiwa Hayo Yote Aliyosema Hayapo Tanzania Labda Nchi Jirani.


Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Anafanya Makubwa Sana Kutunusuru Ingawa Tunapita Kwenye Njia Nyembamba Sana
 
Back
Top Bottom