Kwako Waziri wa Afya: Matatizo matatu ya Hospitali ya Muhimbili na Mloganzila ni haya

Sijui ni wapi kuna ahueni kati ya hizo hospitali za serikali na binafsi. Maana unaenda hospitali binafsi tena kubwa ambayo inatoa huduma za aina fulani lakini inategemea wataalamu kutoka hospitali za serikali ambao nao unakuta wanahudumu hospitali zaidi ya moja. Mgonjwa inabidi apangiwe ratiba kutokana na ratiba ya daktari na sio hali yake. Daktari naye siku akifika anakutana na majukumu mengi hali inayofanya baadhi ya wagonjwa wasipate huduma kwa wakati. Pindi mgonjwa anapozidiwa anapelekwa tena hospitali za serikali. Pasipo umakini katika hii sekta tutashuhudia mengi sana.
Private ni hovyo kuliko! Hawana staff ya maana. Private wanaweka gharama utadhani 4star hotel. Watu wanalipa hadi laki4 kwa siki! Upuuzi tu! Matibabu hovyo!
 
Mheshimiwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, hizi ni Hospitali pacha zenye uzoefu wa uzembe zina matatizo haya matatu;
  1. Madaktari Wazoefu kuhangaikia Hospitali za Mitaani kuliko mwajili wao
  2. Kuwatumia Wanafunzi kujifunza bila Daktari mzoefu mbele ya mgonjwa
  3. Madawa ’feki’ kwa wingi ndani ya Hospitali
Madaktari wako hospitali za Umma kama Kituo cha kutafuta Wateja na kuwaelekeza kwenye vituo vyao vya mitaani ikiwa ni pamoja na Hospitali za binafsi. Kuna sababu gani ya kuendelea kuruhusu Daktari kuhudumu Hospitali za mitaani? Je, Askari Polisi au Askari Jeshi anaweza pia kuhudumu Kampuni Binafsi za Ulinzi?

Nasikia NHIF wanawalipa kutokana na malipo ya Mgonjwa hii ni hatari! Inawafanya kujiingiza kwenye tiba kubwa hata wasizoziweza ili tu wapate pesa

Wanafunzi wamefikia hatua ya kufanya mitihani mbele ya Mgonjwa ambaye hajapewa huduma lakini anatumiwa kama Kituo cha mtihani. Bila hata kuomba samahani, ukiwa hospitali Daktari anajiona kama anakumiliki, ni specimen yake.

Kuna madawa ’feki’ mengi yako kwenye maduka ya hospitali hizi. Yaonekana ni kwa sababu kuna Wagonjwa wengi na waletaji wana dili zao na wahusika.

Mara nyingi utapewa dawa inayoaminika kufanya vizuri katika ugonjwa lakini ukitaka usalama bora ununue ya maduka ya mitaani

Utawala wa hospitali ujiangalie upya! Hili siyo kutafuta sifa.
Kwani ulivyosikia serikali ya awamu ya tano ikihimiza uwekezaji kwenye viwanda vya dawa ili kutengeneza dawa hapa hapa nchini wewe ulielewa nini? au ulipiga vigeregere vya kumtukuza mtukufu bila kuelewa? anyway for your information, panadol zimekuwa zikitenfenezwa hapa nchini kwa muda mrefu but kwanini watu huuliziaga ya kenya au Italy au india?
 
Private ni hovyo kuliko! Hawana staff ya maana. Private wanaweka gharama utadhani 4star hotel. Watu wanalipa hadi laki4 kwa siki! Upuuzi tu! Matibabu hovyo!
Kinachokera na kuumiza ni kwamba licha ya kulipa gharama zote hizo na huduma mbovu bado wakikushindwa wanakupeleka kwenye hizo hospitali za serikali ili hatma yako ikapatikane huko na sio mikononi mwao.
 
Hakuna huo ujinga awamu ya tano, watu wamenyooka sasa nidhamu imerudi kwenye maofisi na watu wanachapa kazi balaa..
Nyie mtakuwa CDM..
Mkuu ndo ushangae watu wale wale wanaoimba mapambio ya kusifu na kuabudu wakimsifu Magufuli kwa kunyosha nchi na kurudisha nidhamu kwenye utumushi wa umma ndo hao hao wanalalamikia huduma mbovu kwenye hospital za umma,dawa feki na vitambulisho Kule NIDA. Yaani sijui kwa nini mtanzania hapigiwi Kura kuingizwa kwenye orodha ya maajabu ya dunia
 
Hivi mtu anapoituhumu mhimbili Mimi huwa sielewi na siamini nimewahi tibiwa hapo Mara tatu ,na nilikutana na doctors tofauti ukweli nilihudumiwa vizuri sana na ilikuwa mwaka 2018,kwa mloganzila sijawahi fika so I can't say anything

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bei ya dawa Muhimbili ni kubwa mno kulinganisha na maduka binafsi. Mdogo wangu aliandikiwa dawa kidonge kimoja sh 1,700+ hapo muhimbili nilipoenda duka binafsi kidonge kimoja hakikuzidi 400.
 
Bei ya dawa Muhimbili ni kubwa mno kulinganisha na maduka binafsi. Mdogo wangu aliandikiwa dawa kidonge kimoja sh 1,700+ hapo muhimbili nilipoenda duka binafsi kidonge kimoja hakikuzidi 400.
Na wewe sijui vipi kwa mnyonge anatetewa na serikali hii 1700+ kwa kidonge ni kitu gani,is just a peanut
 
Huduma zako Mara zote ulizipata kwa kufuata utaratibu uliopo au kupitia connection ? Kwa maana ya kwamba ulikuwa unafahamiana na mmoja wa wafanyakazi wa hapo.
 
We undhani wanapenda kufanya kazi umma na private..mishahara ya umma haitoshelezi mahitaji..na wenyewe wanapambana na maisha yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi watumishi wengine mishahara yao inawatosha?Nao wangefanya hivyo hali ingekuwaje kwenye utumishi wa umma? Hivi kwa mfano mshahara wa mwalimu wa chekechea unaweza kukidhi mahitaji yake? Ila wanapiga kazi bila manung'uniko. Tujitahidi kuthamini maisha ya wengine.
 
Wacha siasa mkuu. Wanaoandika mambo haya wameyaona. Mnavyoendelea kuona kuwa kila anayekosoa ni upinzani basi tutaja stuka kuwa maisha ya watu yanaendelea kupotea kizembe.

Nimewahi kukuta hii hali kwenye hospitali moja kubwa hapa nchini. Wakati huo mtoto wa ndugu yangu alikua na tatizo la figo. Lakini walikuja madaktari wanafunzi kibao kila mmoja anatoa suggestions za vipimo avijuavyo yeye na tuliwasikiliza. Wapo hadi walioshauri afanyiwe x ray ya kifua (cjui ni kwa nn lakini tulifanya)

Ilitokea daktari mmoja mkenya ndiye aliyetustua kuhusu hili. Yeye ndiye aliyekua anashughulika na huyu mtoto na mwisho wa siku alikuta msururu wa vipimo kwenye file. Na hii ni baada ya kuwa tayari tunefanya CT SCAN ambacho ndicho kipimo kilichokua na umuhimu ili dogo afanyiwe upasuaji. Yeye ilibidi atoe mawasiliano yake ili kila tulipokua tunahudhuria hospitali tumtafute ili wale wanaokuja kusomea pale kwenye mwili wa dogo wasitusumbue tena. Hili ndilo lililosaidia dogo kutibiwa kwa haraka.

Kwa hiyo ukweli upo kuwa wanasomea kwenye miili ya wagonjwa. Maana huyu docta alitudokeza kwamba suggestions za vipimo walivyoshauri vifanyike vikionekana vina ukweli basi wanafaulu.

Cku pia dogo anafanyiwa upasuaji tulitakiwa tutoe damu. Wakaja tena wajifunzao kutoa damu. Waliniwekea lile lisindano kwenye mshipa ambao sio mpaka alipokuja muhusika wa kitengo kile. Nilishuhudia akiwaelekeza jinsi ya kutoa damu kwenye mkono wangu (Nikawa specimen chaap) Kiukweli nilitaka kugoma kutoa ila ilibidi nitoe kwa kuwa mtoto ni lazima apone. Tunamshukuru Mungu kuwa alifanyiwa upasuaji salama na figo ilokua na shida iliondolewa.

HAYA MAMBO YANA UKWELI KWA HIYO ACHA YASEMWE WANANCHI WAPONE. UKIWEKA SIASA MBELE, WATU WATAKUFA. AU ILI NIKUFURAHISHE ACHA NIKWAMBIE KUWA "KURA ZITAPUNGUA" KWA SABABU MNAJALI KURA KULIKO WAPIGA KURA.

NAOMBA KUWASILISHA NA WEWE UBADILIKE

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mdau samurai ninavyomuelewa anaandika kejeli..labda kama ameamua kubadilisha gia angani.
 
Na wewe sijui vipi kwa mnyonge anatetewa na serikali hii 1700+ kwa kidonge ni kitu gani,is just a peanut
Peanut? Mgonjwa hana bima ya taifa na anatakiwa kutumia vidonge viwili kwa siku indefinitely!!! Kutokana na afya yake hawezi kufanya kazi. Mnyonge anatetewaje hapa? Bima za afya zinalizwa sana.
 
Nafikiri ni wakati muafaka kwa watumishi wa umma kwa sasa hasa madaktari kuwa na mwajiri mmoja hawe mwajiliwa wa umma au aende private sector.Hataki aingie mtaani aone watu wanavyosugua viatu..
Ishu ya dawa feki TFDA ndio inapaswa kulaumiwa..maana bongo kila kitu ni feki hadi nywele

Kwa sasa hamna TFDA

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mheshimiwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, hizi ni Hospitali pacha zenye uzoefu wa uzembe zina matatizo haya matatu;
  1. Madaktari Wazoefu kuhangaikia Hospitali za Mitaani kuliko mwajili wao
  2. Kuwatumia Wanafunzi kujifunza bila Daktari mzoefu mbele ya mgonjwa
  3. Madawa ’feki’ kwa wingi ndani ya Hospitali
Madaktari wako hospitali za Umma kama Kituo cha kutafuta Wateja na kuwaelekeza kwenye vituo vyao vya mitaani ikiwa ni pamoja na Hospitali za binafsi. Kuna sababu gani ya kuendelea kuruhusu Daktari kuhudumu Hospitali za mitaani? Je, Askari Polisi au Askari Jeshi anaweza pia kuhudumu Kampuni Binafsi za Ulinzi?

Nasikia NHIF wanawalipa kutokana na malipo ya Mgonjwa hii ni hatari! Inawafanya kujiingiza kwenye tiba kubwa hata wasizoziweza ili tu wapate pesa

Wanafunzi wamefikia hatua ya kufanya mitihani mbele ya Mgonjwa ambaye hajapewa huduma lakini anatumiwa kama Kituo cha mtihani. Bila hata kuomba samahani, ukiwa hospitali Daktari anajiona kama anakumiliki, ni specimen yake.

Kuna madawa ’feki’ mengi yako kwenye maduka ya hospitali hizi. Yaonekana ni kwa sababu kuna Wagonjwa wengi na waletaji wana dili zao na wahusika.

Mara nyingi utapewa dawa inayoaminika kufanya vizuri katika ugonjwa lakini ukitaka usalama bora ununue ya maduka ya mitaani

Utawala wa hospitali ujiangalie upya! Hili siyo kutafuta sifa.
Mkuu Zygot, sijui kama ulishafanya kazi katika hospitali yoyote au ya kutibu wagonjwa.
Tukiondoa hilo la madaktari na hospitali binafsi, hayo mengine yote ya wagonjwa kuwa 'specimen' na 'madawa feki' yanadhihirisha kwamba hujui kabisa mfumo wa matibabu na upatikanaji wa madawa hospitalini.
 
Hili tangazo la lishe ya watoto wa umri kuanzia miezi miwili na bei yake shilingi mia mbili hivi waziri Dr. Umi Mwalimu analusikia?

Mbona anaruhusu watoto wachanga kulushwa vitu badala ya nyonyo la mama?

Na je atakuwa na uhakika gani kuwa wachakachuaji hawawezi haribu afya za watoto?

Naomba mniulizie kwa Dr. Umi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dr Umi, (Ummy?) wa wapi?

Kuhusu "watoto wachanga kulishwa vitu badala ya nyonyo", mbona huiamini sayansi? Yale si ni maziwa tu, kama fomula nyingine yoyote inayoweza kutengenezwa?

Labda useme huna imani na mfumo mzima wa usimamizi wa utengenezaji na uhakiki; lakini sababu isiwe upungufu wowote wa lishe kwa hao watoto kutokana na hivyo vitu vilivyotengenezwa katika mazingira yetu duni.
 
Mkuu Zygot, sijui kama ulishafanya kazi katika hospitali yoyote au ya kutibu wagonjwa.
Tukiondoa hilo la madaktari na hospitali binafsi, hayo mengine yote ya wagonjwa kuwa 'specimen' na 'madawa feki' yanadhihirisha kwamba hujui kabisa mfumo wa matibabu na upatikanaji wa madawa hospitalini.
Unategemea aseme mtindo uko sahihi? Kama ulifundishwa kwa mtindo huo, huo ni uzembe na ndo maana hutakuwa daktari wa kutumainiwa.

wanaojitambua huwezi kumtuma mwanafunzi kumu attend mgonjwa bila kumwambia na bila qualified kumuongoza trainee. Huo ni upuuzi! Mbaya zaidi, Muhimbili imejaa trainees wanao attend wagonjwa na kuigiza ni qualified.
 
Mimi Si mtaalam sana, Ila ngoja nichangie kidogo...
Bei za dawa au bidhaa fulani, zinaweza kutofautiana kati ya sehemu moja hadi nyingine Kutegemeana na Ulivyoipata. Kuna njia nyingi za kupata dawa, na tofauti ni kubwa kati ya Manunuzi ya dawa katika hospitali ya Umma na Manunuzi hayo ya dawa katika Duka binafsi la dawa, Njia hizo zinaweza kuchangia kutofautisha bei kati ya hapa na pale.
Tofauti nyingine kubwa, Inaweza kuwa ; Dawa ni ile ile, Ila imetengenezwa na Kampuni mbili tofauti ambapo Moja Inatengeneza Katika Branded Formulation na nyingine ni Generic formulation.
Kidonge kimoja cha Loratin (Loratadine 10mg ya Kiwanda cha CIPLA) kinauzwa 500/-, Ilhali Kidonge Kimoja cha Claritin (Loratadine 10mg ya Kiwanda cha Scherring Plough) Kinauzwa 2500/-.
Unaona Tofauti??
Bei ya dawa Muhimbili ni kubwa mno kulinganisha na maduka binafsi. Mdogo wangu aliandikiwa dawa kidonge kimoja sh 1,700+ hapo muhimbili nilipoenda duka binafsi kidonge kimoja hakikuzidi 400.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unategemea aseme mtindo uko sahihi? Kama ulifundishwa kwa mtindo huo, huo ni uzembe na ndo maana hutakuwa daktari wa kutumainiwa.

wanaojitambua huwezi kumtuma mwanafunzi kumu attend mgonjwa bila kumwambia na bila qualified kumuongoza trainee. Huo ni upuuzi! Mbaya zaidi, Muhimbili imejaa trainees wanao attend wagonjwa na kuigiza ni qualified.
Hivi mnaibuka kutoka wapi; kuna jalala fulani mnakojificha na kuibuka kuzungumzia mambo msiyokuwa nayo ufahamu wowote?
 
Back
Top Bottom