U mrembo binti,na sio kwamba ninakusifia,hapana ila ndio ukweli wenyewe na hata kama nitaamua kukusifia basi sina shaka kuwa Dunia nzima haitoweza kujaa vitabu vyenye sifa zako.Ila kikubwa kilichonisukuma kuandika waraka huu kwako ni upole wako na mapenzi yako kwa kila mtu,awe mkubwa au mdogo.Umebarikiwa upole kama wa njiwa na busara zisizopimika.Ninajua kuwa una wakati mgumu sana hasa kipindi hiki ambapo vijana wa kila aina wenye uwezo na sifa tofauti wanapojitokeza kwako kuomba hifadhi katika moyo wako.Lakini kwa upole na hekima ya hali ya juu umeweza kuwajibu kistaarabu na kuendelea na maisha bila kumuumiza kiumbe yoyote aitwaye mwanaume aliyewahi kukupenda.Binafsi ninaelewa wazi kuwa sina uwezo wa kukumiliki na kuwa baba wa watoto wako,ila hilo halinizuii mimi Mtakatifu kusimama na kusema kuwa unastahili kuwa Miss Chit Chat wetu wa mwaka huu.Na nina imani vilevile hata baada ya wewe kutwaa taji hili basi utaendelea na ustaarabu wako na upole wako na mapenzi yako vile ulivyojaaliwa.
Nisikuchoshe na maneno mengi ila tu ninakutakia kila La akheri na kuomba kila atakayesoma uzi huu basi akupigie kura wewe ili uweze kuwa Miss ChitChat wa mwaka huu.
Copy:
Baba V Erickb52 Filipo marejesho Kipipi Pombekali Arabela Dark City Mungi Asprin