Elli
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 55,499
- 86,037
Kwa muda mrefu nilitaka kuandika hili la Sababu za "kitoto" za kuzuia magari yasisafiri usiku, hatimae Mbunge Tulia ameliona Hilo, tusubiri mamlaka zitekeleze. Mimi ni mdau wa safari za usiku sana, kwahio Wacha niwape experience....
1. Zile Coaster za Arusha zinazuiliwa pale Mkata wa saa Tano, matokeo yake, mkifika pale mnachangishana gari inaongeza wese mnazungukia Handeni, hii ni hatari.
2. Pale pale Mkata Kuna uchochoro, kwahio Dereva anazima Taa mnapita kwenye huo uchochoro kwenye makazi ya Watu, risk inazidi kuongezeka. Unajiuliza, hivi barabara ya Dar to Arusha Ina hatari Gani Hadi hizi gari zizuiliwe kama sio kutengeneza mazingira ya Rushwa tu?
3. Coaster za Dar to Mbeyaz wakifika Moro waliweka Picha ya Marehemu kuwa wanasafirisha msiba...tunajua kilichotokea, laiti ingekua ni route Hali.
4. Hivi kuna umuhimu Gani wa mabasi yote kuanza kufukuzana Pale stand kuu saa 12 asubuhi? Mfano, basi linalokwenda Kigoma, Kasulu, Musoma, n.k kwanini wasiondoke saa tatu asubuhi? Au saa Nne? Ili wasilale? Maana madereva ni wawili wawili, sasa watakimbizana kutwa nzima then watalala Kaliua saa nne usiku Hadi saa 12 asubuhi
5. Hivi kwanini Mabasi ya Bukoba, Ngara, Burundi, nk walazimishwe kulala Kahama na sio Nyakanazi? Siku hizi eneo lote liko salama.
6. Kwanini Mamlaka husika wasiruhu mabasi ambayo madereva wake na mabasi Yao yanatambulika kuliko hii ya kukata Kibali Cha Coaster Kila baada ya muda? Hatuna uhakika wa zile Coaster Wala madereva wake....
Inaendelea..
Inaendelea....
Muda huu ninapoandika hili ni 21:45 ukienda pale Mbezi Kituo Cha Daladala au pale Ubungo Kimara Kuna abiria wengi sana, hawa wanakwenda Mbeya, Dodoma, Mwanza na kwingine, huu ni mfano tu lakini situation kama hio utaikuta Dodoma CBE, Singida pale Nje, Makambako, Mbeya, Moro, Mombo-Tanga, na kwingine.....
Hawa wote wana-risk maisha Yao, kwanini tusiukubali ukweli kuwa route za usiku haziepukiki? Tuhalalishe hizi safari tupunguze ajali za magari ya IT na zile za magazeti, mfano, ndani ya miezi 36 MAGARI ya magazeti yameondoka na maisha ya watu wasiopungua Kumi, coaster za Usiku zimeondoka na maisha mengi the same to IT na Malori. Tukihalalisha tutapunguza tatizo
=====
“SERIKALI IRUHUSU MAGARI YA ABIRIA KUSAFIRI WAKATI WOTE HADI USIKU”- DKT. TULIA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameitaka Serikali kuangalia upya utaratibu uliowekwa katika baadhi ya maeneo nchini wa kuyazuia magari ya abiria kufanya shughuli za usafirishaji nyakati za usiku kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi.
Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Novemba 10, 2022 wakati aliposhiriki Semina kwa Wabunge kuhusu usalama Barabarani iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Amesema kuwa ni lazima ifike wakati sasa Wananchi waweze kufanya shughuli zao muda wote na kuondoa dhana iliyozoeleka ya magari ya abiria kuwekewa vikwazo vya kufanya kazi kwa sababu zizisokuwa rasmi wakati magari mengine yakiwemo ya mizigo yanaruhusiwa.
“Kunashida gani ya kuzuia gari ya abiria kusafiri usiku? Tunatamani nchi yetu kuchangamka Zaidi kiuchumi sasa kwanini magari haya yawe na zuio wakati magari mengine yanaruhusiwa kusafiri hadi usiku. Kama ni changamoto ya miundombinu basi ishughulikiwe na shughuli zifanyike” amesisitiza Dkt. Tulia