Mmexico
JF-Expert Member
- Nov 1, 2016
- 369
- 333
Mlisema hivi zilipopitishwa sheria ya tozo za VAT kwenye utalii Bunge la Bajeti 2016. Mlitabiri kuwa sekta ya utalii itaenda kufa na majirani zetu watapata faida zaidi.Alifanya hivyo kwenye sukari, mafuta ya kula, mahindi, kwenye korosho amekuja kujiokoa mwishoni lakini bado kuna dhuluma kubwa inayoendelea uko Kusini.
Sasa anaenda kuua utalii uko Arusha, kila kitu anachogusa kina kufa.
Magufuli akawaonyesha kuwa mnakosea na hamjui lolote, Sababu sekta iliongezeka mara dufu kwa Kutoa Mapato na idadi ya watalii wa kigeni zaidi ya miaka yote ya nyuma. Ongezeko hilo limeonekana zaidi 2017 na linaenda ongezeka zaidi 2018, wakati huo wote jirani zetu ukuwaji wa sekta hiyo imekuwa ya kusuasua.
Kuna wakati huwa tunakuwa na wasiwasi kuliko uhalisia wa mambo, nia ya sisi kupata chochote toka sekta ya utalii/nyinginezo zisitufanye tukasahau vitu vya msingi ambavyo vinaweza kutughalimu zaidi. Tunalegeza sheria kwenye mambo ya utalii kwa kuhofia kenya na matoleo yake tunakuwa hatupati faida yeyote inayo onekana.
Nchi zinazoongoza kufaidika na utalii Africa ni Misri,,Madagascal, Maultania,Africa kusini,Kenya,Namibia,Morocco na zote hizo wanahakikisha sheria za kubadirisha fedha zinafuatwa. Uganda,Rwanda,Ethiopia na hata Kenya biashara ya forex haifanywi kiholela kama hapa Tanzania. Tuamke.