Kwaheri Biashara ya Utalii Tanzania....

Kwaheri Biashara ya Utalii Tanzania....

Niliwahi kushinda na njaa OR Tambo airport nikisubiri ndege kisa wenye biashara za migahawa hawataki dolar bali rand zao. Siku nyingine kwa bahati mbaya nikacheki in uwanja wa ndege wa Addis Ababa na pesa za Ethiopia. Nilipotaka kununua vitu kwenye maduka ya duty free wakasema hawataki madafu yao labda nitoke nje nibadili kuwa dolar. Hii ishu nikaja kugundua baadae kuwa
1. Uimara wa sarafu fulani dhidi ya dolar pamoja na mlinganyo wa kiasi cha uwezo wa hifadhi ya dolar ktk nchi husika pia ni LAZIMA kuwa na udhibiti madhubuti wa kubadilisha fedha (money exchange business) ktk masoko
2. Hapa nchini unaweza ukaenda na burungutu la USD kwenye bureau de change ukabadilishiwa bila kuombwa passport wala kitambulisho.
Kwa hiyo serikali iachwe ifanye kazi zake. Madhara yakitokea yanaweza kuwa ni muda mfupi lakini in a long run mambo yatatulia.
Kwa nini hujabadilisha ukapata rand? Ndani hapo kuna travelex za kumwaga. Umekaa na njaa bure.
 
Nan kakudanganya, una chenji ela pale unapotaka kuitumia maana uwezi kununua chochote na ela ya juvenile. Nimekuwepo jozi kwa siku 14 na dola na pula zimetulia kwenye wallet mbn sikufatwa.
Wachangiaji wengine wanafikiri kila mtu ni mshamba hapa. Hauwezi kumlazimisha mtu abadilishe pesa zake zote.

Sheria za kimataifa ni kuonyesha customs ukiwa na US$ zaidi ya 10,000 tu kwa nchi nyingi, unapoingia. Tumia upendavyo.
 
Nchi nyingi zinadhibiti bureau de change ata hao watalii huwa wanashangaa jinsi ilivyorahisi kubadilisha pesa za kigeni hapa nchini...
 
Kwa hili la kuingilia biashara ya fedha za kigeni kuna maana mbaya specifically kwa utalii Tanzania na biashara zote kwa ujumla. Leo hii serikali ya Magufuli imezindua rasmi black (parallel) market ya fedha za kigeni and by extension kuhamishia biashara zenye mwelekeo wa Kimataifa nchi za jirani. Kama kuna watu wanashangilia sasa hivi ni jirani zetu north of our boarder.

Seems the Magufuli regime's solution to the current economic woes is this one here below:
View attachment 939505
KARIBU ZIMBABWE YA MUGABE in a few months to come.
Ndio lengo kuu la itikadi za kijamaa zimekazia utawala zaidi kuliko kuinua uchumi, itikadi za kijamaa huwa ni kupambana na watu sio kupambana na maendeleo.
 
Hamna kitu kama hicho Magufuli sio mjinga mpaka akosee na hafanyi haya kwa ajili yake Bali kwa taifa Zima.tatizo lenu nyie mnajifanya mnajua kila kitu


Hata msemaje sisi tuna imani na Rais wetu
Toka kwa shemeji kafungue hata genge ujitegemee
 
Alifanya hivyo kwenye sukari, mafuta ya kula, mahindi, kwenye korosho amekuja kujiokoa mwishoni lakini bado kuna dhuluma kubwa inayoendelea uko Kusini.
Sasa anaenda kuua utalii uko Arusha, kila kitu anachogusa kina kufa.
Na hakuna atakayenyanyua mdomo yanayoendelea kule kusini
 
Rais ajae Atakuwa na Kazi kubwa sana kuirudisha nchi kwenye mstari huyu kainyosha hadi imepinda na kukatika kabisa,ajae ana Kazi kubwa sana ya kulipa madeni kupunguza deni la taifa,kuinua uchumi mfu, kurejesha tija na morali ya Kazi kwa Watumishi, kuwasukuma ndani wasiojulikana, kujenga demokrasia, kuvutia na kushawishi wawekezaji, kurejesha diplomasia ya kimataifa, kupunguza ttzo la ajira,kuimarisha shillings yetu, kuujenga upya umoja wa kitaifa,kurejesha imani ya vyombo vya dola kwa wananchi, kufukua makaburi yote na kuwasukuma ndani wote waluotumia vibaya Madaraka, vibaya kodi zetu,kukaa kimya juu ya upotevu wa watu,kuinua elimu,kurejesha mifumo ya haki ya kodi, kuifufua Bandari iwe bize kama zamani,nk.Kazi ni kubwa si ya kitoto.Ajae awe na nyota ya Pesa na mwenye BARAKA kila kitu kitakuwa sawa.
 
Hairuhusiwi kutumia dolar moja kwa moja. Nami sikutaka kubadili dola zaidi ya 20. Ukitaka kubadili lazima wabakie na dolar 10 kama commission yao. Manake lazima kubadili kuanzia dolar 50. Kwa ujumla wako strict na rand yao
Ni hasara kubadilisha pesa ndogo ndogo kwao.

Usitegemee nchi yoyote ubadilishe viji dola kidogo airport bila ya commission kubwa.. Airport ni " captive market".

Siku nyingine badilisha dola 50. Jirushe katika baa. Kula. Kunywa. Life is short. Enjoy.
 
Nasikia huko Jamhuri ya watu wa kusadikika wamekagua benki kuu yao wakaona hakuna pesa za kigeni. Yani reserve ya pesa za kigeni ni ndogo sana kiasi kwamba haitoshi kufanya purchase nje kwa miezi kadhaa ijayo. Kwahiyo wameamua kwenda kuzitafuta kwenye maduka ya kubadili fedha. Wanaamini zimefichwa huko. Kwamba wenye maduka wamezibana na hawataki kuziachia. Kwahiyo wameamua kwenda kuzisaka kwa mitutu ya bunduki. Songombingo za Kaboka mchizi.!

Ngoja niwape shule kidogo. Sababu za msingi za kupotea kwa 'dola' katika nchi hiyo ni hizi hapa.

#Mosi; nchi huwa inapata pesa za kigeni kwa kuuza bidhaa na huduma nje. Lakini nchi ya kusadikika imezuia kuuza mazao nje. Nasikia huko mahindi yanaozea ndani, mbaazi ndo kwisha habari yake, tangawizi hata ukitupa watu hawaokoti. Hivyo vyote vilikuwa vina soko kubwa nje ya nchi na vinaingizia nchi hiyo pesa nyingi za kigeni. Lakini mfalme wao akapiga marufuku wasiuze nje. Leo wanamtafuta mchawi. Maajabu.!

Koro-show nasikia nayo imezuiwa kuuzwa nje. Serikali ktk nchi ya kusadikika imesema itanunua yote. That means hakuna pesa zozote za kigeni nchi hiyo itaingiza. Kama makampuni binafsi kutoka nje yangeruhusiwa kununua yangekuja na 'dola'. Wangechange na kupata madafu ya kulipa wakulima. Hayo 'madola' yaliyochenchiwa yangeingia kwenye mabenki na hatimaye benki kuu. Kwahiyo serikali ingeongeza reserve yake ya pesa za kigeni. Lakini wameamua kununua koro-show zote wenyewe, leo wanatafuta dola kwa mitutu?

Na mfalme wao amesema akikosa soko atamwambia kila mtu kwenye nchi hiyo ale ratili mbili za koro-show. Hizo ratili mbili kwa kila raia zinanunuliwa kwa pesa ya madafu na zitaliwa na raia wa humohumo ndani. Kwahiyo koro-show zote zinaweza zikaisha bila kuingiza hata dola moja kwenye nchi hiyo. Hii ni biashara kichaa ktk historia ya biashara duniani.!

#Pili; nchi inapata pesa za kigeni kupitia mikopo na misaada mbalimbali ya kimataifa kama vile kutoka Benki ya dunia, IMF, na mataifa wahisani kama Marekani, Umoja wa Ulaya etc. Sasa nasikia Benki ya dunia imesitisha mikopo na misaada kwenye nchi hiyo. Baadhi ya mashirika ya kimataifa nayo yamesitisha shughuli zake huko. Umoja wa Ulaya nao unafikiria kusitisha misaada yote kwa nchi hiyo, na tayari balozi wao ameshafurushwa. Kwahiyo hakuna 'foreign grant wala loan' ambayo inaingiza pesa za kigeni kwenye nchi hiyo kwa sasa. Lakini wanaenda kutafuta pesa za kigeni kwa AK47 kwenye maduka ya kubadili fedha. Hekaya za Abunuasi.!

#Tatu; Nchi inapata pesa za kigeni kwa kukaribisha wawekezaji wa kigeni kwa wingi (Foreign investors). Mwekezaji akienda kujenga kiwanda katika nchi fulani haendi na pesa za madafu, anaenda na dola. Akifika huko hizo dola anazibadili na kupewa madafu. Dola zinaingia kwenye system na kuongeza reserve ya pesa za kigeni.

Lakini kwenye nchi ya kusadikika foreign investors wanafokewa na kunyang'anywa passport. Kiongozi akishashiba 'ugali tembele' anaropoka tu 'mnyang'anyeni passport'. Matokeo yake wawekezaji wanahamisha mitaji na kwenda kuwekeza kwenye nchi nyingine. Leo nchi ya kusadikika iko busy kutafuta nani kaficha pesa za kigeni kwenye sandarusi. Harakati za pimbi.!

#Nne; nchi inaingiza pesa za kigeni kutokana na jinsi inavyouza utaalamu wake nje ya nchi. Lakini kwenye nchi ya kusadikika wataalamu wamezuiwa kwenda kufanya kazi nje. Serikali yao imesema mtu yeyote anayepata kazi nje ya nchi inabidi aombe kibali kwanza akiambatanisha mkataba wa ajira. Na serikali inaweza kumruhusu au kumkatalia. Leo serikali hiyohiyo ipo 'busy' kutafuta dola kwenye maduka ya wahindi. Futuhi.!

#Tano; Njia nyingine ya kumaintain pesa za kigeni ni kuregulate kiwango cha kununua na kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi. Unatakiwa kuuza zaidi kuliko unavyonunua. Hakikisha unanunua nje vitu vya muhimu tu. Vingine vitengeneze mwenyewe. Hii ni kwa sababu kila unapoagiza bidhaa yoyote nje ya nchi unapunguza reserve yako ya pesa za kigeni. Lakini kanchi ka kusadikika kanatumia reserve yake ya pesa za kigeni kununulia hadi toilet paper, halafu leo kanatafuta pesa zilikofichwa. Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un.!

Malisa GJ
 
Inawezekana Luna agenda ya kuaanzanzeto to hero,lea kuflyekelea mbali ya wata gulizi na nyie mkuu za uchumi iliad asuka upya tuwe na sunrays na wavumilivu tukaze miranda.tuko kwenye njia sahihi

Mkuu nini mbaya?? Mbna unaandika kitu ambacho hakieleweki ila hapa mtaani kwetu tuna darasa la watu wazima na pia tunaanza na vile vitabu vya kusoma kwa hatua na pia tunafundisha jinsi kupangilia herufi, karibu sana .
 
Mkuu nini mbaya?? Mbna unaandika kitu ambacho hakieleweki ila hapa mtaani kwetu darasa la watu wazima na pia tunaanza na vile vitabu vya kusoma kwa hatua na pia tunafundisha jinsi kupangilia herufi, karibu sana .
Haaaaa kuna simu inanisumbua huko darasa nitajiunga mkuu nipate marini ya yaaani kwako
 
Haaaaa kuna simu inanisumbua huko darasa nitajiunga mkuu nipate marini ya yaaani kwako

Pole mkuu itakulazimu kubadilisha kioo cha hiyo simu ama ukabilishe touch,ienda ulikuwa na busara zako lkn tukashindwa kuchota hizo busara kutokana na tatizo la simu
 
Hamna kitu kama hicho Magufuli sio mjinga mpaka akosee na hafanyi haya kwa ajili yake Bali kwa taifa Zima.tatizo lenu nyie mnajifanya mnajua kila kitu


Hata msemaje sisi tuna imani na Rais wetu
Natamani kupima akili yako
 
Hamna kitu kama hicho Magufuli sio mjinga mpaka akosee na hafanyi haya kwa ajili yake Bali kwa taifa Zima.tatizo lenu nyie mnajifanya mnajua kila kitu


Hata msemaje sisi tuna imani na Rais wetu
Sisi na kina nani? Usipende kujumlisha vitu au watu bila utaratibu, sema "Mimi" sio "Sisi". Pumbav
 
Hamna kitu kama hicho Magufuli sio mjinga mpaka akosee na hafanyi haya kwa ajili yake Bali kwa taifa Zima.tatizo lenu nyie mnajifanya mnajua kila kitu


Hata msemaje sisi tuna imani na Rais wetu
Hata ZANU-PF walianzaga na vijimaneno vyenu hivihivi vya kwenye kanga ktk suala nyeti la uchumi wa nchi, mwisho wa siku waliongea lugha moja na wapinzani, tatizo muda tu....
 
Hamna kitu kama hicho Magufuli sio mjinga mpaka akosee na hafanyi haya kwa ajili yake Bali kwa taifa Zima.tatizo lenu nyie mnajifanya mnajua kila kitu


Hata msemaje sisi tuna imani na Rais wetu
Sisi tuna imani na Mungu siyo huyo udongo wenu
 
Back
Top Bottom