Rais Samia apongezwe kwa hatua anazochukua, ni dhahiri kwamba mama yuko kazini

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Serikali ya Awamu ya Sita imesimama imara katika kutafuta fehda za miradi mbalimbali ya maendeleo, hivyo juhudi hizo zinapswa kulindwa maendeleo yapatikane kwa haraka katika jamii.

Uwepo wa ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya watendaji wasiokuwa waaminifu kama alivyobainisha CAG kupitia ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka 2021/2022 ni wakati sahihi wa hatua kuchukuliwa hatua.

Kuchukuliwa kwa hatua kutazidisha uaminifu ikizingatiwa kuwa Rais Samia ameshatoa uamuzi kwa watendaji watakaobainika kuhusika na uzembe au ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria.

Tunapongeza hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Rais Samia Suluhu ikiwemo kuwata watendaji kujibu hoja na kuzifanyia yote yaliyoibuliwa na CAG na kugusa maeneo yao.

Usimamizi madhubuti wa fedha za umma unapswa kuwa endeleu kutokana na serikali kutumia mabilioni ya fedha kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali, hivyo zinapaswa kulindwa.

Tunaamini sasa ni wakati sahihi wa kila taasisi ya umma kuhakikisha inalinda fedha za wananchi zinazotolewa kutekeleza miradi na kuhakikisha zinatumika kwa malengo yaliyopangwa kwa ufanisi na weledi.
 
Back
Top Bottom