Serikali ya Rais Samia ni imara haiyumbishwi na kelele nyingi za wachache

Fukua

JF-Expert Member
Jun 1, 2022
546
479
Amani iwe nanyi ndugu zangu.

Kwa kweli ukisoma waraka wa TEC kwa haraka bila tafakuri, ukisikiliza hoja za wapingaji wa mkataba kwa mihemko na ukisikiliza hoja na maelezo ya serikali kwa umakini kuhusu huu mkataba utagundua uzalendo na umakini wa serikali usiopimika.

Ni kweli pia hakuna kinacho kosa mapungufu na ndio maana serikali imetoa wito wa kusikiliza maoni ya watu wake kwa upole na staha kuu.

Kanisa katoliki limechanganya dini na siasa bila kificho. Ni wanufaika wa wizi mkubwa bandarini, hili jambo la uwekezaji ni mwiba kwao SI vyema kuwachagulia njia au namna ya kulia au kuomboleza.

Tuwavumilie maaskofu Hawa kwa kupotoka, hata wale watanzania wenzetu kama wakina mdude na mwambukusi wenye changamoto za akili tuwavumilie pia hawakupenda kuwa hivyo.

Wapinzani hawana hoja tumewazoe ni watu wa husuda, chuki. Wivu na mihemko ni waongo, wachonganishi na wasioitakia mema nchi yetu.

Kwa maoni yangu nasema wazi mwanzo niliingiwa na Pepo chafu la upingaji wa mkataba lkn baada ya kutulia, kumuomba Mungu aniongoze kutafakari a kusikiliza ufafanuzi na hoja za serikali nimejiona mkosaji.

Kwa kuwa serikali imeahidi kuchukua maoni ya wananchi Ili kuboresha zaidi sina shaka Tena na mkataba huu.

Nipongeze serikali chini ya mama Samia kutoyumbishwa na kelele za uongo na propaganda za kanisa katoliki, kwamba serikali itaendelea na uwekezaji wa bandari zetu.

Kuna wananchi wengi walisombwa na uongo, uchonganishi na propaganda za kanisa katoliki lkn Sasa wameelelewa njama hizo na kurudisha Imani zao kwa serikali.

Nimalize kwa kusema kwamba watanzania tuendelee kutafakari bila mihemko, bila udini na ukanda na mwisho tutaiona Nia njema ya serikali yetu kwenye mkataba huu, tuchambua hoja kwa umakini na utulivu.

Hakuna wa kuuza bandari zetu na hakuna mwenye uwezo wa kuivuruga amani yetu.
 
Back
Top Bottom