Kwa wenye umri wa miaka 25 na kuendelea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wenye umri wa miaka 25 na kuendelea

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ben Saanane, Apr 15, 2010.

 1. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hebu niulize swali la kizushi,wakuu ni kosa gani ambalo umeshawahi kulifanya ukiwa na umri wa miaka 25-30 wakati ulipokua chuoni,kazini ambalo limekugharimu huko baadae na au ambalo ungetamani kuwa kama ungepewa nafasi nyingine ya umri kama huo usingelirudia?

  Tunataka tu kujifunza kutoka kwa wengine
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kampuni niliyokuwa naifanyia kazi mara ya kwanza ilikuwa liquidated, nikapewa mafao 2M kipindi hicho (Y2K), sikuifanyia lolote zaidi ya kuzinywa na kurekebisha tabia za warembo!!

  Only if wishes were horses...huh!
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kuishi maisha ya useja nikidhani nitatesa huko mbele ya safari. Sasa nimegundua kwamba hiyo nafasi nimepoteza kwani huku nilipo sasa ndo kugumu kuliko maelezo.
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Duh,mkuu kweli kwenye hii range ya miaka hali ni critical.Mkuu kwani kipindi hicho hukua na mchumba?ilikuchukua muda gani kujijenga upya?
   
 5. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Kipindi hicho nilipewa mradi wa biashara kuiendesha(kusimamia) lakini kwa uzembe za kupenda anasa baada ya kuwa na pesa nyingi vilinipotezea nikashindwa kufanya mambo mengi ya msingi katika maisha, nikaja kuamka wakati nanyang'anywa mradi.

  Natamani muda huo ungekuwa sasa kwani maisha nilichezea leo hii nalala njaa... CHEMSHA BONGO.
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Inauma lakini ni vizuri sana kwani ilikutokea wakati bado una muda wa kurekebisha makosa. Shukuru Mungu kama umetoka salama kwani tulio wengi pia umri ulio tayari ulishavamiwa na upupu! Experience is the best teacher.

  Wenzio hata experience kama zako tunazisikia kwenye bomba. Nahofia yanaweza kutukuta yale ambayo wengi wanasema kuwa ukimiss ujana wako utautafuta uzeeni. Ngoja nione kama nitakuwa Guinea pig!
   
 7. N

  Ngala Senior Member

  #7
  Apr 15, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huna sababu ya kujuta. utumishi wa umma enzi ulikuwa upuuzi mtupu mbele ya wafanyabiashara. 2m vilikuwa visenti tu enzi za ruksa na kupanga matumizi kwa figa hiyo ungepata kichaa vingine vyo ungerudi nazo kijijini pengine muda huu ungekuwa diwani
   
 8. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hahahaha mimi kitu nilichofanya nikaja kujutia lkn sasa hivi majuto yameisha ni kwamba ktk biashara zangu nilifanikiwa kuwa na saving kubwa. Sasa nilipokuwa nimepanga nyumba watoto wa kike wa mama mwenye nyumba walikuwa waanichokonoa sana kwa kero za kila namna sijui ilikuwa ni wivu maana nilikuwa dogo nina shughuli zangu wao wanashinda home tu!

  Siku moja kero zikanizidi rohoni nilikuwa na kiwanja nikatafuta fundi ujenzi nikamwonyesha ramani akafanya quotation, bila kufikiria nikajenga nyuma nzima hadi ikaisha nikahamia na visent vyangu benki navyo vikaisha na biashara ikayumba halafu sikuwa na hela za kuisave biashara, nilitamani kuchanganyikiwa na jumba nilliliona kama kaburi, watu walikuwa wananipa hongera wanasema mambo yako supa lkn walikuwa hawajui rohoni nilikuwa na crisis!

  NAMSHUKUU JEHOVA HIRE AMENIVUSHA NA SASA NAENDELEA VIZURI TENA lkn nilijifunza mambo mengi kutokana na kosa hilo.
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Apr 15, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  halo halo.Ben bana.Mmh,nitakuambia siku nyingine
   
 10. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hahaa.................. najua itakuwa ni ile ishu ya mzumbe,.................hahaha................. sehemu ya maisha tu hiyo sister...........
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  ha ha ha ha PJ
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Najaribu kukumbuka bado nacheza ndani ya nyakati....
   
 13. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  SOMEWHERE IN BETWEEN ndio nimeoa!
  sasa sina uhakika kama NIMEKOSA MIMI,NIMEKOSA MIMI,NIMEKOSA SANA
   
 14. R

  Renegade JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,769
  Likes Received: 1,074
  Trophy Points: 280
  Ben, nilipata pesa nikasahau shule, nikajirusha sana, nilivyokuja kukumbuka shule nikakuta wenzangu wako mbali, Nikarudi shule kwa nguvu! nashukuru niliweza kuziba ile Gap.
   
 15. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Dah! Hii imekaa vizuri sana. Nakumbuka mwaka 1998 nilipata kazi moja yenye mshahara mzuri sana kwa wakati ule. Jambo kubwa nililofanya kwanza kabisa ni kununua Chaser Mayai. Mazee huwezi kuamini sikumbuki kama niliwahi kusave pesa bank maana mshahara na pesa nyingine nilizokuwa nakamata at that time ziliishia pale Kwa Macheni magomeni na Lango la jiji ni mwendo wa kubadili akina dada kila kukicha. Mwisho wa yote ili kubaki kuwa juu nikaanza mpaka kudokoa na pesa za ofisi siku auditors wametia timu nilikuwa natoka jasho mpaka kwenye kucha za vidole vya miguu. Kiukweli nilitimuliwa kazi ingawa nashukuru sikushitakiwa na gari nikauza. Niliyumba sana mpaka nilipokuja kukaa sawa. Laiti nafasi ile ningeipata nikiwa na akili za sasa hivi ningefanya mambo makubwa zaidi.
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Lakini Cheusimangala kwa nn ulijuta huoni kama nyumba ni asset kubwa kwako ..kuliko pesa kukaa bank kila siku unacheki balance tu
   
 17. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mhhhhhhhhhhhhh to me I keep on making mistakes, but I take the as challenges and new experiences and move on cause kuna muungwana alisema "experience is what people calls their mistakes" Life to me is a school so everyday I learn new stuff and personal I dont regret any thing happened to my life cause they are significant in my life.
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  kuanzia 25.............hun kisanga Geoff :)
   
 19. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Dah....Kosa kubwa ambalo najutia sana(Naomba Mungu anisamehe) ni kuhusu uchaguzi wa kozi za kusoma huko chuo.Sikutaka kufuata moyo wangu unataka nini au ninapenda kusoma nini ambacho nitakifanyia kazi ninayoipenda.Nilifuata mazingira yanataka nini na watu(wakiwemo wazazi na serikali) wanataka nini(si mnajua zile za masomo ya sayansi).
  Kama ingekuwa tunarudisha muda,Nisingesomea hii profesheno niliyonayo.
   
 20. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hehehe!
  sina kwa kweli!
  lakini wewe fl1 naomba usiandike chochote kwa heshima yangu
   
Loading...