Kwa wenye magari binafsi piteni hapa

Ningekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ingekuwa ni marufuku kwa mtu yeyote yule kuendesha gari yoyote ile akiwa peke yake ndani ya gari.

Haiwezekani mtu atoke posta akiwa kwenye gari yenye siti nne na nyingine zina siti sita halafu mtu yupo peke yake wakati kuna watu wanasubiri daladala masaa mawili mpaka matatu.

Najua ni gari yako, ulinunua kwa pesa zako na hakuna aliyekuchangia ila kwa hilo mngeniona mchungu.

Najua nitakuwa navunja sheria ila nisingewaacha. Ukaguzi wa magari hayo private kwa watu wanaotoka posta na kariakoo ungekuwa unafanyikia Jangwani kwa wanaenda Ubungo, Ubalozi wa Ufaransa kwa wanaoenda Mwenge, kurasini kwa wanaoenda mbagala na temeke, UKIKUTWA UPO PEKE YAKO KWENYE GARI UNARUDISHWA POSTA KUBEBA WATU.
____________
UPDATE: Kama kumpa mtu lift unaogopa usalama wako basi hata gari ikikusumbua usiwaombe watu wakusukume maana huwajui hivyo itahatarisha usalama wako.

Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)

Kuna baba wa rafiki angu aliwapa lifti watu kutoka mwenge-posta..yule mzee aliweka pc chini ya kiti..na alipakia watu wazima na heshima zao..anasema anafika ofisini tu....kwishney...laptop imeondoka na doc zote za muhimu..haijulikani nani aliondoka nayo kati ya wale aliowapa lift... So watch out kwa dunia ya sasa mkuu. Mwanadamu ni zaidi ya umfikiriavyo..
 
Last edited by a moderator:
Afadhali ninyimwe lift ili nipate uchungu wa kununua la kwangu. Watu wezi siku hizi, toeni lift tu kwa strangers ila mwisho wa siku mtakuja hapa kulialia.
 
Mkuu Mchunguzi huru, mbona mii huwa nasimama niwape lift, ila maraia wenyewe huwa hawataki, wakiniuliza unaenda wapi, huwa nawajibu naenda Mabwepande! Hawapandi Mkuu MCHUNGUZI HURU

he he he umenichekesha mkuu.hata mimi sipandi aisee
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweli kuhusu hilo itakuwa ngumub kidogo kutokana na hali ya usalama hivi sasa watu hawana utu pia ukiangalia swala la ustarabu lipo kushoto kwa watu wengi kuhusu hilo pia itakuwa ni ngumu watu kukubaliana na mambo kama hayo.

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Wewe jamaa umeongea pumba, nashauri sio kila kitu cha kuweka hapa.

Anzisha hyo kabla hujatolewa mkuu wa mkoa kesho yake.
 
phd yako umripstia wspi sijui......pumba tupu huwezi kumpangia mali ya mtu.mtaolewaaaa
 
Wewe jamaa umeongea pumba, nashauri sio kila kitu cha kuweka hapa.

Anzisha hyo kabla hujatolewa mkuu wa mkoa kesho yake.
Ajiita mchaguzi huru, naona watu wameshaanza kumupuuza, page ya tatu toka jana.

badilika si kila kitu uandike.
 
yaani gari yangu imetoka kuoshwa 5min ago,na hizi mvua za dar nimpe mtu lift na matope yake na jinsi alivyoloa,na ki vitz changu kilivyo chini hivyo ukilinganisha na mabonde ya hapa riverside kibangu, weweeeeee hiyo haipo,mleta mada nashawishika kukuita mlevi
 
Moja ya udereva wa kujihami ni pamoja na kukatazwa kupakia mtu usiemfaham kabisa maana anaweza kukudhuru"Epuka kupakiza mtu usiemfaham katika gari yako"
 
acheni kuendekeza umasikini... kinachohitajika ni miundo mbinu

we should always strive to succeed and not to accommodate sheeedah ilimradi wwawajibikaji walale
 
Back
Top Bottom