Kwa wenye magari binafsi piteni hapa

Kwa wenye magari binafsi piteni hapa

Wao hela zao wamejengea nyumba. Wanatupangisha na kodi tunawalipa alafu magari yetu ndio wapande buree eeh? Nyooo!
 
Ningekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ingekuwa ni marufuku kwa mtu yeyote yule kuendesha gari yoyote ile akiwa peke yake ndani ya gari.

Haiwezekani mtu atoke posta akiwa kwenye gari yenye siti nne na nyingine zina siti sita halafu mtu yupo peke yake wakati kuna watu wanasubiri daladala masaa mawili mpaka matatu.

Najua ni gari yako, ulinunua kwa pesa zako na hakuna aliyekuchangia ila kwa hilo mngeniona mchungu.

Najua nitakuwa navunja sheria ila nisingewaacha. Ukaguzi wa magari hayo private kwa watu wanaotoka posta na kariakoo ungekuwa unafanyikia Jangwani kwa wanaenda Ubungo, Ubalozi wa Ufaransa kwa wanaoenda Mwenge, kurasini kwa wanaoenda mbagala na temeke, UKIKUTWA UPO PEKE YAKO KWENYE GARI UNARUDISHWA POSTA KUBEBA WATU.
____________
UPDATE: Kama kumpa mtu lift unaogopa usalama wako basi hata gari ikikusumbua usiwaombe watu wakusukume maana huwajui hivyo itahatarisha usalama wako.

Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)

Phd = pengine huna degree..
 
Last edited by a moderator:
naomba kuanziaaa kesho mke wako na dada zako tutawapa lift bure tu usijali.......si ndyo unachotakaaa hicho usaidiwe
 
wewe naye mtu wa ajabu sanaaa! gari ninunue mimi na ushuru nilipie mimi na kodi ndg ndg nilipue mimi alafu nilazimishwe kuwapa watu luft hakuna kitu kama hicho, kwanza kiusalama hutakiwi umpandishe mtu usiye mjue wewe unaweza ukapataa balaaa ambayo hujaitegemea.....fikirini kabla ya kuamuaa jambo

Suala si kutoa lift, suala ni wew kuchangia kusababisha folen isiyo ya lazima mjini kwa wewe kutembea pekeyako na gari kumbe ungetumia public transport ungesaidia na wasio na magari kuwahi waendako kwa kupunguza msongamano wa magari na wewe kusave fedha ambazo ungetumia kwa mafuta na matengenezo ya gari. Tumia gari lako pale inapobidi kufanya hivyo tu na sio wote wapandao usafiri wa umma hawana magari....
Ni ushauri tu...
 
Natoka tunduma nipo chalinze nataka niingie posta na SEMI TREILA vp inawezekana? wakuu nijulisheni haraka.

Unaingia posta ya wapi? Humo kwny semi-trella umebeba barua au vifurushi?
 
Saa 4. hoya twendeni manzese midizini

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Suala si kutoa lift, suala ni wew kuchangia kusababisha folen isiyo ya lazima mjini kwa wewe kutembea pekeyako na gari kumbe ungetumia public transport ungesaidia na wasio na magari kuwahi waendako kwa kupunguza msongamano wa magari na wewe kusave fedha ambazo ungetumia kwa mafuta na matengenezo ya gari. Tumia gari lako pale inapobidi kufanya hivyo tu na sio wote wapandao usafiri wa umma hawana magari....
Ni ushauri tu...

huo syo suluhisho wala nini? mwishowe mnapokaa ukiona wenzenu wana mahitaji kuliko wengine mtataka kuombana chimvi na mafuta ya kipikia...syo lazima kumpa mtu lift ni hiyari tu ya mwenye gari....watu tushaishi sehemu ambazo watu kuonana ni kwa nadra tu lift hupewi, kiusalama tu hutakuwi mpa mtu lift udiye mjua kwani anaweza kukudhuru wewe au wewe mwenye gari ukamdhuru.....wazungu wana usemi wao mmja dont talk to strangers
 
Back
Top Bottom