Kwa wenye magari binafsi piteni hapa

Kwa wenye magari binafsi piteni hapa

kwasasa hicho kitu hakipo na ndiomaana unaona kama ajabu ila itakapozoeleka litakuwa jambo la kawaida. Changes begin with you.

Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)

mi nashauri kabla ya kuwachukulia hatua wenye magari binafsi uanze na wale wanaoendesha ya serikali na mashirika.ya umma na peke yao. hiyoitakuwa phase one na baada ya miezi sita inahamiakwa watu binafsi. hata waoga.hawataogopa kupanda ambayo yana namba za serikali
 
Last edited by a moderator:
Kwanini wenye magari mnawaonea, mfano ukiwa kwa mguu ukamwambia mtu umsaidie kubeba kamzigo kake kwa kuwa mnaelekea uelekeo mmoja atakukatalia kwa kuwa hakujui pia hajui una nia gani though unaweza kuwa lakini linapokuja suala la gari watu mnapenda kupewa lift hata kama mwenye gari humjui.
 
Naomba niwatetee kidogo wenye magari... Si kwamba hawataki kutupatia lifti..ila dunia ya leo ndugu yangu imegeuka kichwa chini miguu juu. Uhalifu umekuwa mkubwa mno kiasi kwamba watu wanaogopa kutoa na kuomba msaada. Unaweza kumpa mtu lifti matokeo yake ukaishia kuporwa kagari kako na mwili wako ukaokotwa mabwepande hukoo. Tanzania ilikuwa ni nchi inayosifika kwa ukarimu wa watu wake lakini taratibu na sisi tunauvaa ukauzu maana tumeona ukarimu wetu unageuzwa dili.
Mimi binafsi hata niwe na shida kiasi gani eti atokee mtu from nowhere simjui hanijui ananiambia panda twende wala sipandi aisee.....najua wapo wenye nia nzuri lakini siwezi kufanyia majaribio roho yangu.

Shost umenena .....waga nawashangaa wamawake wengne et amjui mtu kasimamisha gar lake anapanda....ndio maana wengne wanakomesheaga unapanda tu mbelen anaenda kukutolea li jini lake ulinyonyeshe lol
 
Yaani hayo yote. Kuna mtu ananuka miguu, mdomo ama jasho. Kuna wadakuzi anapekenyua kila mahali hadi unamshusha keshachana na seat na kuharibu power window. Kuna wezi, ubebelee simu yako, sio laptop na hata viatu vya ziada. Hukawii kukuta mwingine anakula muwa na hawezi kumeza maganda ( cc Matola).

halafu jioni umejichokea, ama asubuhi una stress huna hela. Umebeba complete strangers kwenye gari, mnaongea nini?! Saa zingine unataka kublast mamiziki ujiimbie kama mwehu usahau stress zako!

huu ushauri nao!
Issue nyingine pia Privacy hata kama upo mwenyewe maana unaweza ukapigiwa simu mfano upo kwenye foleni unashindwa kuongea mambo yako kisa kuna stranger ndani, pia hata sheria inakataza kumpakia mtu usiemjua sema kibongobongo huwa tunapakiana pasipokujua unaweza mkapata ajali alafu mwenye gari ukapona alafu abiria wako kafa unaambiwa unaulizwa basic information zake huna alafu mara mke au mume wa mtu na Tanzania udaku unauza na ndio utasingiziwa kila kitu
 
Mkuu tatizo wizi mwingi!kuna daktari mmoja alitoa lifti kwa mtu asiyemjua jamaa akashuka la laptop yake!pia sikuizi usalama ni kidogo maadui kuanzia ofisini hadi mtaani!

Pia ni kosa kisheria kumpakia mtu usiemjua maana kuna lolote laweza kutokea njiani na wewe basic information zake huna
 
Shost umenena .....waga nawashangaa wamawake wengne et amjui mtu kasimamisha gar lake anapanda....ndio maana wengne wanakomesheaga unapanda tu mbelen anaenda kukutolea li jini lake ulinyonyeshe lol

Hee kunyonyesha jini tena...??!!
 
Hee kunyonyesha jini tena...??!!

Ujawah ckia kuna mdada alipewa lift kufika mbele akatolewa kitu anyonyeshe inavosemekana ilikua ni jin tena imetokea mara nyingi tu na kisa ni lift
 
sijui shibe ngoja nkalale nikiamka ntakuja ku comment
 
Mimi sikupi lift labda niwe nakufahamu, hii darisalama watu watakunyonga bure waende na gari
 
Wewe Mchunguzi huru kumbe siyo Mtanzania mbona umesahau barabara moja inayoyotoka katikati ya mji. Wale wa barabara ya Nyerere ukaguzi ufanyike wapi. Pole wakuja
 
Ningekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ingekuwa ni marufuku kwa mtu yeyote yule kuendesha gari yoyote ile akiwa peke yake ndani ya gari.

Haiwezekani mtu atoke posta akiwa kwenye gari yenye siti nne na nyingine zina siti sita halafu mtu yupo peke yake wakati kuna watu wanasubiri daladala masaa mawili mpaka matatu.

Najua ni gari yako, ulinunua kwa pesa zako na hakuna aliyekuchangia ila kwa hilo mngeniona mchungu.

Najua nitakuwa navunja sheria ila nisingewaacha. Ukaguzi wa magari hayo private kwa watu wanaotoka posta na kariakoo ungekuwa unafanyikia Jangwani kwa wanaenda Ubungo, Ubalozi wa Ufaransa kwa wanaoenda Mwenge, kurasini kwa wanaoenda mbagala na temeke, UKIKUTWA UPO PEKE YAKO KWENYE GARI UNARUDISHWA POSTA KUBEBA WATU.
____________
UPDATE: Kama kumpa mtu lift unaogopa usalama wako basi hata gari ikikusumbua usiwaombe watu wakusukume maana huwajui hivyo itahatarisha usalama wako.

Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)

kumbe wewe ni mchunguzi jina, wala huna maarifa yoyote juu ya uchunguzi, unaandika kile kinachokugusa moyoni, mchunguzi gani wewe.! Ndio maana kuna magari ya biashara...
 
Last edited by a moderator:
...tofauti itakuwa wapi sasa kama mwenye gari na asiye na gari wote wana wahi kufika town/kazini...
 
Ningekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ingekuwa ni marufuku kwa mtu yeyote yule kuendesha gari yoyote ile akiwa peke yake ndani ya gari.

Haiwezekani mtu atoke posta akiwa kwenye gari yenye siti nne na nyingine zina siti sita halafu mtu yupo peke yake wakati kuna watu wanasubiri daladala masaa mawili mpaka matatu.

Najua ni gari yako, ulinunua kwa pesa zako na hakuna aliyekuchangia ila kwa hilo mngeniona mchungu.

Najua nitakuwa navunja sheria ila nisingewaacha. Ukaguzi wa magari hayo private kwa watu wanaotoka posta na kariakoo ungekuwa unafanyikia Jangwani kwa wanaenda Ubungo, Ubalozi wa Ufaransa kwa wanaoenda Mwenge, kurasini kwa wanaoenda mbagala na temeke, UKIKUTWA UPO PEKE YAKO KWENYE GARI UNARUDISHWA POSTA KUBEBA WATU.
____________
UPDATE: Kama kumpa mtu lift unaogopa usalama wako basi hata gari ikikusumbua usiwaombe watu wakusukume maana huwajui hivyo itahatarisha usalama wako.

Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)
Utafiti umekwishabainisha kuwa chazo kimojawapo cha msongamano wa magari ktk miji yetu ni suala la empty seats za magari private.Hii haihitaji akili nyingi sana kulitambua kwa mfano nyakati za asubuhi ukisimama kati ya traffic lights za ubalozi wa Urusi na Palm Beach, barabara ya Ali H. Mwinyi, ukahesabu idadi magari yaliyojazana barabarani na ukalinganisha na idadi ndogo ya abiria walioko kwenye magari hayo.
 
Kweli aise, ukizingatia pollution inayosababishwa na gari lake inatuathiri wote.
 
Basi itabidi sumatra watoe leseni magari yote binafsi kubeba abiria
 
Utafiti umekwishabainisha kuwa chazo kimojawapo cha msongamano wa magari ktk miji yetu ni suala la empty seats za magari private.Hii haihitaji akili nyingi sana kulitambua kwa mfano nyakati za asubuhi ukisimama kati ya traffic lights za ubalozi wa Urusi na Palm Beach, barabara ya Ali H. Mwinyi, ukahesabu idadi magari yaliyojazana barabarani na ukalinganisha na idadi ndogo ya abiria walioko kwenye magari hayo.

Siku nikukute umempakia mamsap wangu au binti yangu huyu wa kidato cha5 kwenye kigari chako eti umewapa lift, nakunyonya mimacho Mimi. Dar es Salaam huwezi kumkuta mtu from nowhere eti umpe lift, nyokoooo
 
Kwa jinsi mie nilivyojijengea akilini kwangu eti gari isimame iniambie lift sijui twende nikusogeze huwa nakataa nahisi ana jambo jingine zaidi ya lift.So mie kama kukubali lift ni kwa yule ninaemju
 
Back
Top Bottom