Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Huyu Kijana Alimpenda Sana Yule Ahjumma.

Ahjumma Anaonekana Ana Mambo Mengi.
 
wewe naona tupo pamoja maana na mimi napenda drama za historia ya Korea kupitiliza
 
Historical drama nimeshaziona nyingi sana, nilianza na:-
*Legend of the Prince Jumong(2007/08)
*Queen Seondoek ( 2011/12)
*King Gwanggaeto the Great Conqueror(2012)
* Kim Suro(2012)
* The Gybaek(2012)
Hizo ndo Historical drama zangu 5 za awali kabisa.
😀😀 Nakumbuka kipindi hicho nasoma kipaimara.
 
wewe bwege kutoka pyongyang hivi kipaimara ndio wapi?
 
Jeon Mi-Sun

Nitamkumbuka Zaidi Katika SIX FLYING DRAGONS Alipocheza Kama Mama Yao Ddang-Se (Lee Bang-Ji) Na Boon-Yi Ambaye Ilimlazimu Awe Kiongozi Wa Taasisi 'Tata' Ya Moomyung Na Hivyo Kupelekea Kutengana Na Watoto Wake Wazuri. Ni Pigo Kubwa Sana Kwa Familia, Tasnia Ya Burudani Nchini Korea Kusini Pamoja Na Wapenzi Wa Filamu Za Kikorea Duniani Kote. My Deepest Condolences!
 
aminas kuja hapa mara moja kwa amri ya mkuu wa mkoa.
laiti kama ningelikuwa ni muigizaji basi kuna nafasi nisingelikubali kushiriki ikiwemo nafasi aliyocheza mzee song seung hwan ndani ya one spring night drama.

yule mzee ni kichaa sana na kuwa na baba mwenye fikra kama zile ni laana kubwa sana na si kharamu kumtoa uhai wake.
mzee ameamua kuifunga akili yake kwa sababu ya ahadi aliyopewa na baba yake gi seok pindi atakapostaafu kazi yake ya ualimu.

si hivyo tu mtoto wake ameshafanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia zaidi ya mara moja na mume wake cha ajabu kwake yeye anachukulia ni jambo la kawaida litakaloweza kutatuliwa kwa kurudisha tena upendo usiokuwepo na si kupeana talaka.

sipendi ninapomuona jung in anamwita gi seok oppa, kuendelea kumpa kwake heshima hiyo kunazidi kumfanya bwana yule awe mwehu haliyakuwa wamesha achana japokuwa jamaa analazimisha mahusiano.

natabiri:
one spring night drama inakwenda kubeba tunzo ya MBC daesang drama awards 2019.
hizi fashion za mwanadada han ji min zinanimaliza, mhhhhhh mwanamke wa kolomijee umletee zawadi ya nguo kama hizi mbona pataruka kivumbi kuliko shuti aliyopiga msenegali ndiatte.
 
upcoming drama
Designated Survivor: 60 Days
siku: jumatatu na jumanne
Release Date: July 1, 2019 --
kituo :TvN

Nina muda mrefu sana sijafuatilia drama zinaonyeshwa mwanzoni mwa wiki kupitia kituo cha tvn, nakumbuka mara ya mwisho niliangalia 100 days my prince na ilikuwa ni mwaka 2018.

Designated Survivor: 60 Days ni remake series ya kimarekani inayojaribu kuzungumzia hadithi ya aliyekuwa professor wa chemistry ambaye baadae anateuliwa nafasi ya waziri wa mazingira,

ebwana weee huyu fala alikula bonge la zari baada ya kutokea mripuko uliopelekea kifo cha rais wa nchi na warithi wake wanaofuata hivyo basi jamaa akapata nafasi ya kuwa raisi kwa siku 60.

jamani mbona hii hadithi inafanana na hali iliopo kwetu?
si nilisikia jamaaa wa lichadema alisukumiwa uwenyekiti kwa lazima?
si nilisikia siku ya harusi yake alikunywa soda ya fanta na mirinda?
ji jin hee amerudi tena
 
Zote nimeziona ila Kuna baadhi sikumbuki uhusika wake.
 
Huo ukatili una mwisho wake.

Nataka niendelee na Deep root je story yake inaukweli?! Au imefiksiwa!.
 
South Koreans wanaishi maisha ya kiushindani na kiupinzani kupita kiasi: Elimu, Ajira pamoja na maswala mengine mbalimbali ya kijamii. Katika mazingira kama hayo, ili uwe na mafanikio ya kuridhisha na kufanikisha maisha yako, inakubidi na wewe uwe ngangari kwelikweli la sivyo ukibaki nyuma, msongo ya mawazo utaanza kukuandama.
 
Mi Ukinipa Izo Navaa! Sema Hio ya Chini Ndo Itakua Na Ugumu..

Yule Babu ni Ndezii Wa Kiwango Cha Chini Sana, Kiboko Yake Ni Ji Min Tu Ndo Anaemueza Kwa Watoto Wake!..

Ila Gi Seok Ni Ndezi Nae Ila Wa Kiwango Cha Kati! Maana
 
Bidada Nahisi Mambo Mengi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…