Kwa Wanawake wote wa JF

Kwa Wanawake wote wa JF

kwahiyo nyie ambao hamjalala saa8 hii kasoro ndio mabachela sugu wa jf? 😂😂😂

Me na Dahan tumeamka kuangalia vifaranga visijedondokea uvunguni
Ole wao waufanyao usiku kuwa mchana.
Maana yake: Ole wao wafanyao kiza kuwa Nuru.
Maana Nyepesi: Ole wao wafanyao dhambi kuwa halali.

Maandiko matakatifu yamepiga BAN kukesha na wanaokesha ni Popo 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Mimi nipo lindo nalinda maduka ya watu. Ila mbu wanag'ata Sana asee!!
Ole wao waufanyao usiku kuwa mchana.
Maana yake: Ole wao wafanyao kiza kuwa Nuru.
Maana Nyepesi: Ole wao wafanyao dhambi kuwa halali.

Maandiko matakatifu yamepiga BAN kukesha na wanaokesha ni Popo 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Wanawake wote mnaotokea Singida mna nafasi ya kipekee moyoni na akilini mwangu. Nawapenda sana
 
Ni matumaini yangu mko salama wote popote mlipo.

Napenda niseme maneno machache katika siku yenu muhimu...mnaposherehekea siku ya wanawake duniani.

Kwa wale wasomi wa biblia kuna mistari kadhaa imewasifia wanawake kuwa ninyi ni kitu chema;

Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.

Mithali 18:22

Biblia inawaita ni ni KITU CHEMA.

Nami nasema hakika mwanamke ni;

- Ktu chema na cha baraka

- Nyie ni maua yenye harufu nzuri kwetu

- Hakika mnavutia sana

- Ninyi ni furaha ya familia na jamii

- Mmeumbwa kwa namna ya kipee.

- Viumbe vya kuvutia kwetu

Tunawapenda sana

WANAWAKE KAMA WAZAZI
Wanawake kama wazazi na walezi mnapitia magumu mengi mno.

Ni vigumu mwanamke kumkimbia mtoto iwe jua au inyeshe.

Wengi wenu mnapitia changamoto za kukikimbiwa na wenza wenu lakini hakika huwa mnasimama imara kuhakikisha mnatulea kwa furaha na bila majuto.

Mungu awabariki mno.

Wakati naenda kuanza form one..
Marehemu mama yangu aliniusia maneno yafuatayo kwa lugha yake ya asili
( Kitutsi....Mwana wanjye Glenn wubahe abagore nka mama ,bashiki bawe numugore🙏🙏)

(Maana yake..mwanangu Glenn muheshimu mwanamke kama mama, dada na mke)

Hivyo kwangu mimi mwanamke ni;
  • Mama
  • Dada
  • Rafiki bora kabisa
  • Mpenzi/mke.

Najitahidi kuwaheshimu na kuwapa thamani yenu sana (JAPO KIUBINADAMU HUWA NAKOSEA PIA)

Sijawahi kusita kujitolea kusaidia au kuingilia ninapoona kuna uonevu akitendewa mwanamke bila kujali ninamfahamu au laa.

Huo naona kama vile nina wajibu wangu kumsaidia kama mama au dada...najua si mimi pekee bali ni wanaume walio wengi.

Hii ni kutokana na umuhimu wenu kwetu.
Mmetulea kwa upendo na mapenzi makubwa.

Jambo lingine kubwa zaidi ...ninyi ni mashujaa sana.
Mwanamke aweza kuolewa na mzee kuliko yeye na akampenda na kumtunza kwa upendo.

Anaolewa na baunsa, jambazi na jitu katili sana na akammudu bila tatizo hii ni ajabu sana...nawapongeza katika hili pia.

Hivyo mnapo sherehekea siku yenu msijione wanyonge bila kujali mnapitia hali gani.

Nawatakia siku njema na ya baraka wapendwa na vipenzi vyetu na...
TUNAWAPENDA SANAA MA..sweetheart wetu
witnessj
Kapeace

Evelyn Salt Nakadori Carleen Chakorii Antonnia Ms cee
Kelsea Mama pretty Amehlo Depal
Lenie Jadda Heaven on Earth Heaven Sent witnessj Makiwendo Mideko Palina winlicious
To yeye Unique Flower Bantu Lady Tinsleyooo Saint Anne Shunie Mzigua90 reymage Madame S Inna Joanah Nuzulati mawardat Amehlo Mideko
Joannah To yeye Demi Kalpana Darlin Shunie Debora Msiko
Mamndenyi mama D
Aksha Dejane
moneytalk
Clkey luckyline Valentina Nifah
Dr. Mariposa
sophy27 Lovelovie Ironbutterfly Iron Lady


Amen mkuu shukrani sana!! Hakina maneno mazuri sana ya kutia Moyo na kujenga!!
Be blessed 😘
 
Mkuu Glenn kwa niaba ya Wanaume wote Tanzania especially tuliomo humu kwenye familia ya JamiiForums nikupongeze kwa andiko lako kwenye siku hii maalum ya Wanawake/Wake/Dada zetu Duniani. Umeandika maneno mazuri yenye kugusa hisia kwa kila binadamu mwenye utimamu wa akili na hisia. Binafsi nawaheshimu, nawapenda na ninnawathamini sana Wanawake haijalishi Mwonekano, hali ya kimaisha na Upeo wa kufikiria pamoja na mapungufu waliyo nayo. Nimepitia malezi Wanawake zaidi ya Wanne. Bibi mzaa Baba alinilea na kunidekeza sana, Mama yangu alikuwa ni mwenye sheria na mkali sana, kuna Mama ambaye alinilea na kunitunza kama mwanae wa kumzaa japo tulikuwa tunafanya kazi nyingi lakini tulikuwa tuna enjoy sana maisha ikiwemo kuvaa vizuri na kwenda sana vacation sehemu mbalimbali na kuna royal family pale visiwani Zanzibar kuna Mama naye nilipitia mikononi mwake na nilikuwa najitegemea lakini alinifundisha vitu vingi sana ikiwemo hii modern life na alinisaidia sana ku control hisia na mihemko yangu. Yote kwa yote Mwanamke ni binadamu muhimu sana na ndiye aliyekuja kuikamilisha hii dunia.
Nawatakia heri nyingi sana Wanawake wote.
 
Back
Top Bottom