Kwa Wanawake wote wa JF

Glenn

JF-Expert Member
May 23, 2015
65,797
156,924
Ni matumaini yangu mko salama wote popote mlipo.

Napenda niseme maneno machache katika siku yenu muhimu...mnaposherehekea siku ya wanawake duniani.

Kwa wale wasomi wa biblia kuna mistari kadhaa imewasifia wanawake kuwa ninyi ni kitu chema;

Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.

Mithali 18:22

Biblia inawaita ni ni KITU CHEMA.

Nami nasema hakika mwanamke ni;

- Ktu chema na cha baraka

- Nyie ni maua yenye harufu nzuri kwetu

- Hakika mnavutia sana

- Ninyi ni furaha ya familia na jamii

- Mmeumbwa kwa namna ya kipekee.

- Viumbe vya kuvutia kwetu

Tunawapenda sana

WANAWAKE KAMA WAZAZI
Wanawake kama wazazi na walezi mnapitia magumu mengi mno.

Ni vigumu mwanamke kumkimbia mtoto iwe jua au inyeshe.

Wengi wenu mnapitia changamoto za kukikimbiwa na wenza wenu lakini hakika huwa mnasimama imara kuhakikisha mnatulea kwa furaha na bila majuto.

Mungu awabariki mno.

Wakati naenda kuanza form one..
Marehemu mama yangu aliniusia maneno yafuatayo kwa lugha yake ya asili
( Kitutsi/kinyarwanda........Mwana wanjye Glenn wubahe abagore nka mama ,bashiki bawe numugore🙏🙏)

(Maana yake....mwanangu Glenn muheshimu mwanamke kama mama, dada na mke)

Hivyo kwangu mimi mwanamke ni;
  • Mama
  • Dada
  • Rafiki bora kabisa
  • Mpenzi/mke.
Najitahidi kuwaheshimu na kuwapa thamani yenu sana (JAPO KIUBINADAMU HUWA NAKOSEA PIA)

Sijawahi kusita kujitolea kusaidia au kuingilia ninapoona kuna uonevu akitendewa mwanamke bila kujali ninamfahamu au laa.

Huo naona kama vile nina wajibu wangu kumsaidia kama mama au dada...najua si mimi pekee bali ni wanaume walio wengi.

Hii ni kutokana na umuhimu wenu kwetu.
Mmetulea kwa upendo na mapenzi makubwa.

Jambo lingine kubwa zaidi ...ninyi ni mashujaa sana.
Mwanamke aweza kuolewa na mzee kuliko yeye na akampenda na kumtunza kwa upendo.

Anaolewa na baunsa, jambazi na jitu katili sana na akammudu bila tatizo hii ni ajabu sana...nawapongeza katika hili pia.

Hivyo mnapo sherehekea siku yenu msijione wanyonge bila kujali mnapitia hali gani.

Nawatakia siku njema na ya baraka wapendwa na vipenzi vyetu na...
TUNAWAPENDA SANAA MA..sweetheart wetu
ephen_ binti kiziwi Joanah Shunie @raymage Nourhan Amehlo Kalpana Depal
witnessj
Kapeace
Joannah
Evelyn Salt Nakadori Carleen Chakorii Antonnia Ms cee
Kelsea Mama pretty Amehlo Depal
Lenie Jadda Heaven on Earth Heaven Sent witnessj Makiwendo Mideko Palina winlicious
To yeye Unique Flower Bantu Lady Tinsleyooo Saint Anne Shunie Mzigua90 reymage Madame S Inna Joanah Nuzulati mawardat Amehlo Mideko
Joannah To yeye Demi Kalpana Darlin Shunie Debora Msiko
Mamndenyi mama D
Aksha Dejane
moneytalk
Clkey luckyline Valentina Nifah Dahan
Dr. Mariposa
sophy27 Lovelovie Ironbutterfly Iron Lady
Sky Eclat Joanah trudie
Hannah
FaizaFoxy Joannah
 
Back
Top Bottom