Kwa wanaosema biashara ya duka haina faida, soma hapa tafadhali

Nimefanya sana hiyo biashara pale Mlandizi jirani na Bar ya Kauli ya Bibi, kikubwa ni lazima ukae mwenyewe dukani au mkeo, vinginevyo utapigwa tu. Mimi nilikosa usimamizi sababu naishi Kimara kazi nafanya mjini, kule nakwenda wikendi tu, mwisho wa siku nikaamua kuliuza duka kwa jamaa. Lakini ukweli ni kwamba inalipa sana ukiwa mwenyewe, pia niliweka na vibia viwili basi mwendo ulikuwa oya oya tu.
You are just talking to your diary

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kumbuka siku ukinywa bia kama tano ni 2000 X 5= 10,000/: ukila na kitimoto kilo moja na ndizi ni 12,000/: hapo utakua na demu nae atakunywa santiana au dompo 15,000/: ukitoka hapo ingia gesti ya bei rahisi ya 20,000/: mtoe demu asibuhi na hata 20,000/: utakuta umekula creti la pepsi,kreti la coca,paketi za sigara,pampers zisizohesabika, viberiti mabunda kadhaa nk. Kazi ya kuuza duka hata ukila mchana ujue shelfu itakutizama. Munisamehe

Sent using Jamii Forums mobile app

Wew jamaa wew, haki umenipa burudani asubuhi hii

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Katika maisha tambua kitu "Muda"

Hakuna biashara mbaya kwenye maandishi.. Zote zinalipa vizuri sana but kiuhalisia changamoto ni nyingi sana..

Unauza kreti 1 ya soda ndani ya muda gani kukamilisha hiyo buku jero?

Ni watu wangapi kwa muda gani unamaliza katoni moja ya soda takeaway.

Kila biashara inafaida kama kutakua na mahesabu vs muda.
 
Kumekuwa na arguments kuwa biashara ya duka hasa rejareja haina faida....leo ntaleta baadh ya bidhaa tu kupinga arguments hzo...(maana ndo ishu nnayoifanya)

Just kabla sijaanza....ukitaka kuona mafanikio ya hii biashara...wew muuzaji uwe mtaji wa kwanza...!!kichwa chako kiwe mtaji dukan pia mazoea kwenye duka plus mahusiano ya kimapenz weka pemben kabsa

1.Soda
Pepsi huuza kreti kwa sasa 9500(soda jumla hua 24 kwenye kreti)
Ukiuza jumla utapata 12,000(faida hua ni 2500
Coca wanauza 10,000(hapa faida 2000)
-take away zinauzwa katon 9,000 na znakuwa 12(faida 3,000)

2.vocha (hapa nazungumzia za kurusha...za kukwangu sincerely speaking sijawah kuuza na sitarajii)
-Tigo hutoa 6% kama faida kwa kila float utakayonunua(ukinunua float 10,000 unapata 600...(hapa bado faida za kwenye vifurushi ukiunganisha...(Internet ya buku kwenye float wanakata 900 mteja atakupa 1,000..100 ya kwako)
-voda hutoa 8% kila unaponunua float(ukinunua float 10,000 unapewa 800(hapo pia kuna faida ukiunganisha vifurush)

3.Maji makubwa uhai
Lita 6 unanunua ma5 kwa 8500 utauza kwa elfu 2 jumla unapata 10,000(1,500 ya kwako)
Lita 12 unanunua kila moja 2500 utauza kwa 3,500(1,000 kila dumu moja ni ya kwako)

4.Viberiti unanunua dazan 4,500 unapata 9,000(4,500 ya kwako)

5.pampers unanunua 14,000...zinakuwa 40(kila moja utauza 500...unapata 20,000....elfu 6,000 ya kwako)

6.sabuni ya kufunga
Utanunua kiroba 31,000....ukifunga vizuri na kwa kipimo cha 500( faida mpaka 10,000 unapata)

Kuna vingi vya kuweka ila sitamaliza leo....hapo bdo sijataja unga..mchele....sukari..ngano...maharage....tomato na vingne kibaaao

Just hakuna biashara mbaya....just ni wew mfanyabiashara....!!msimamo wako na unavoichukulia biashara yaki

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujazungumzia msaidizi mwizi,kodi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kumbuka siku ukinywa bia kama tano ni 2000 X 5= 10,000/: ukila na kitimoto kilo moja na ndizi ni 12,000/: hapo utakua na demu nae atakunywa santiana au dompo 15,000/: ukitoka hapo ingia gesti ya bei rahisi ya 20,000/: mtoe demu asibuhi na hata 20,000/: utakuta umekula creti la pepsi,kreti la coca,paketi za sigara,pampers zisizohesabika, viberiti mabunda kadhaa nk. Kazi ya kuuza duka hata ukila mchana ujue shelfu itakutizama. Munisamehe

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana tajiri aliyejiajiri,fedha yake atumii ovyo ukilinganisha na walioajiriwa.
 
Back
Top Bottom