Kwa wana CHADEMA halisi

Kwa wana CHADEMA halisi

user-offline.png
Josorobert

Yesterday 23:08
#1
MemberArray


Join Date : 14th September 2015
Posts : 12
Rep Power : 303
Likes Received14
Likes Given0


[h=2]
icon1.png
Mfumo unaotumika UKAWA[/h]
Kuna jambo jingine wanasiasa waupinzani wanatuaminisha kuwa CCM ina mfumo mbovu hata aje Malaika hawezi kusaidia kitu kubadili mfumo. Hebu tufikIri kwa pamoja kama hii ya upizani si mifumo

1.CHADEMA
Ni chama kinachojinasibu kwa demokrasia na kikiitaji tanzania kuwa na demokrasia.

MFUMO
Tangu chama kiwepo kimeongozwa na familia moja ya mzee mtei.
i. Mwenyekiti wa kwanza wa chama alikuwa mzee MTEI
ii. Mwenyekiti wa pili mzee Bob Makani akimuoa dada yake mzee MTEI (shemaji mzee Mtei)
iii. Mwenyekiti wa tatu ni Freeman Mbowe, ambaye anamuoa bintiye mzee Mtei (MKWILIMA)

ZZK aliwai kusema chadema wanaamini mikoa mingine wazazi wake hawawezi mzaa mwenyekiti.

Je huu siyo mfumo mbuvu?

Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu, akihojiwa na VOA alisema Slaa aliachana na chama chao kwa sababu ya kukosa uraisi na akasema Kamati kuu ya Chadema ilimpitisha Slaa mwezi Januari kuwa mgombea uraisi, na ikampitisha tena mwezi April kuwa mgombea. Kamati kuu moja ilimpitishaje mgombea mmoja mara mbili jibu wanalo wao. Je ilikuwa na haja gani baadae kusema watu wachukue fomu wakati chama kishampitisha mtu yule? .

Baada ya LOWASA kuingia akawazidi nguvu wakapindua maamuzi ya kamati kuu aliyosema Lissu,Naibu katibu Mkuu wao Salum Mwalimu, akasema Kamati kuu ikempitisha Lowassa kuwa mgombea uraisi pekee.

Kumbuka alipitishwa kabla hajachukua fomu ya kuomba uteuzi wa chama, afu kesho yake wakatangaza ati watu wachukue fomu za uteuzi wa uraisi na chama kikamsindikiza kwenda kuchukua fomu ya chama. Nani angeweza kwenda kuomba achaguliwe wakati kuna mgombea ashachukua fomu kwa kusindikizwa na viongozi na ashatangazwa kupitishwa peke yake.

Hili ndo sharti gumu alilowapa upinzani, kama wanamtaka asipambanishwe na yeyote.
HUO SIYO MFUMO MBOVU??

Pale kuanzia Slaa, Mbowe, Ztito, Lisu, Ndesapesa,etc wote kila.mmoja ana jamaa yake mbunge viti maalumu. Je huu si mfumo mbovu?

2. CUF
Hiki ni chama chenye mizizi mikuu zanzibar. Chama hiki tangu kiumbwe miaka karibu 25 kimeongozwa na mwenyekiti na katibu mkuu mmoja kwa kumbukumbu yangu, nimemsikia maalimu Seif na Prof Lipumba.

MFUMO
Tangu kuumbwa chama CUF wagombea uraisi ni walewale. Maalim seif huu ni mwaka wa 25 anagombea uraisi. Lipumba naye alishachukua fomu so ni yale yale.

Viongozi wake wakuu ni wale wale kabla ya juzi.Prof kuachana nao.
Nakumbuka hamad Rashid alijaribu kutia pua kugombea ukatibu akafukizwa uanachama na Maalim seif mwenye milk.ya maisha ya chama.

Unaniuliza ati kwa nn CCM ijione inafaa
kutawala miaka yote hujiulizi kwa nini Maalimu seif kwa nusu ya miaka 50 ya uhuru anajiona anafaa kuwa katibu wa chama na mgombea peke yake?

3. NCCR
Hiki ni chama ambacho walau kimebadiri viongozi japo nacho kina sifa kama hapo juu. Mbatia kukiachia si leo. Nakumbuka kafulila alithubutu kuutaka U chair naye akafutwa uanachama akaishi kwa mgongo wa mahakama. Baada ya kuhisi ni potential kuliko wote mle walimwangukia ila ni baada ya uchaguzi wa mwenyekiti kuisha.

4.NLD
Hiki nisikizumgumzie maana chama cha mfukoni cha makaidi na anatembea nacho mfukoni. Anajulikana yeye tu pamoja na kuwa chama ni cha muda mrefu.

Basi ndugu hawa wana uhalali wa kusema chama cha CCM kina mfumo mbovu bila kukiangalia wao??
Chadema imepoteza viongozi potential.wakilalamikia mfumo mbovu wa chama je.wameshasahau yao?
Ok twende na hoja ya mfumo maana wanaibeba ili kuwaaminisha watanzania wa kwao anafaa kwa vile ati ccm wana mfumo mbovu.

Wanaamini lowasa alikuwa mzuri ila tatizo mfumo wakati miaka nane wamemtukana kuwa lowasa ni mbovu na hawakuwai kusema mfumo. Hivi najaribu kujiuliza hawa wote UKAWA hakuna aliyesoma organization behavior?

Hivi unaweza kuwa na mtawala mbovu katika kampuni nzuri?

By then who makes a system. People makes a system and they can change a system.

Mbona Lowasa alienda akabadili mfumo wa uteuzi.wa UKAWA waliojiwekea?
Kwamba wanaamini lowasa atakuwa raisi afu wamtawale wao??
Ukiwauliza hawa wanakwambia awe mbovu alete maendeleo asilete tunachotaka mabadiliko. Ndo lema alisema Arusha hata likiwekwa jiwe litapita yaani tunageuzwa wajinga tusiyoweza kupambanua ati kisa mabadiliko.

Sisikii tena maamuzi magumu!!, Kauli rahisi za hadaa huku ukiamini unajitofautisha na unaopingana nao ni ajabu.

Tutafakari na kufanya maamuzi yaliyo sahihi.​





Mkuu hongera kwa mchanganuo mzuri ingawa nasikitika kuwa hakuna atakayekuelewa kwa kipindi hiki....tena unaweza ukaambulia matusi.....
 
Acha propaganda za kitoto tena za kizamani kama zile za omari mahita

wewe kada wa ccm tena uliyefirisika kielimu,kiuelewa, you are not creative.huwezi kumshawishi hata

mtoto wa darasa la saba. Usirudie utoto wako wapelekee huko kwenu mliopumbazwa na uongo wa chuo cha kigamboni cha propaganda
 
Hili wala lisiwasumbue mioyo wapenda mageuzi wa kweli; watu ambao wanatambua kilichotokea wanasubiri tu siku hiyo ili waizimishe daima hi safari isiyo na lengo. Wanachadema na wanamageuzi ambao wamekataa kuwa sehemu ya usaliti huu harakati wanajua nini kinahitajika na wanasubiri kwa hamu kukata kile tunachoweza kukiita ni "ngebe" ya kundi la wanasiasa ambao wamejaribu kuchukua njia ya mkato.
 
mmh,

..hapana.

..tukiwapa ccm itachukua miaka mingine 50 kuwatoa.

..bora tuwape ukawa halafu tutumie miaka mingine 5 kujipanga kupata hayo unayoita mageuzi ya kweli.

..nakuhakikishia itakuwa rahisi kuwaondoa ukawa 2020 kuliko kuwaondoa ccm.
 
Last edited by a moderator:
Chadema itabaki kuwa chadema....after october 2015...kura ni kwa ukawa...
 
Mtoa Mada una kiakil kdg xn, kwann utujumuishe ccm wapgie mwenyewe, jtegemee na ufkr Zaid
 
Hili wala lisiwasumbue mioyo wapenda mageuzi wa kweli; watu ambao wanatambua kilichotokea wanasubiri tu siku hiyo ili waizimishe daima hi safari isiyo na lengo. Wanachadema na wanamageuzi ambao wamekataa kuwa sehemu ya usaliti huu harakati wanajua nini kinahitajika na wanasubiri kwa hamu kukata kile tunachoweza kukiita ni "ngebe" ya kundi la wanasiasa ambao wamejaribu kuchukua njia ya mkato.

Kwa hiyo mwanamageuzi ni wewe???? Wewe ni msaliti tu na mchumia tumbo.

Kwani miaka ya nyuma mbona hukua na effect yoyote sasa? Pamoja na umageuzi wako?
 
njoo na wazo mbadala kama unalo maana sijaelewa ulichomaanisha

Mkuu ni kweli huwezi kunielewa, utatumia nini ili unielewe? Wazo mbadala ccm iondoke kwanza tuanze hesabu upya.
 
[/LIST]

Umenena yaliyo wazi. Tatizo humu ukumbini kuna wenye bongo zenye maziwa mgando ambao hawaoni kuwa wanatumiwa na TEAM LOWASSA kutimiza malengo ya Lowassa na sio malengo ya wanamageuzi.

Nyie mbwa acheni kupotosha umma.
Mnataka kusema hilo mnaloita kusanyiko ndo chanzo cha haya?
Kuua viwanda vyote
Kuuza kifisadi nyumba za serikali
ufisadi epe
Ufisadi richmond
Ufisadi meremeta
mikataba isiyo na manufaa ya madini
Ufisadi tagold
Ufisadi escrow
hospitali kukosa dawa
Barabara mbovu zinazoua watz kila uchao
shule kukosa madawati
Ufisadi mgodi wa kiwira
Mauaji ya maksudi mwangosi
gharama za maisha kupanda
maisha duni kwa watz wengi huku viongozi wa ccm wakineemeka
ccm NI CHAMA CHENYE LAANA
 
mmh,

..hapana.

..tukiwapa ccm itachukua miaka mingine 50 kuwatoa.

..bora tuwape ukawa halafu tutumie miaka mingine 5 kujipanga kupata hayo unayoita mageuzi ya kweli.

..nakuhakikishia itakuwa rahisi kuwaondoa ukawa 2020 kuliko kuwaondoa ccm.

Nakubaliana na wewe asilimia mia. Wenye akili tu ndo wataliewa hili. Ila IQ kinukta hawataka waelewe. Naamini watanzania wengi ni waelewe hawatafanya ujinga wa kuirudisha CCM madarakani.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wapenzi na wanachadema halisi wa chadema na mageuzi kwa ujumla, haihitaji kuwa na degree kujua tumesaritiwa na watu tuliwaamini na kuwapa vyeo ndani ya chama chetu ili watuongoze, cheo ni dhamani.
hatutakiwi kubeba makosa ya mbowe wala yeyote, kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe.
kutuletea mgombea uraisi wa kuchonga ni jambo lisiloingia akilini! katika watu wote ina maana hakuna mtu ambaye hangefaa kuongoza nchi? ina maana chama chetu kwa muda wote ni mamburula? kweli tunafikia sehem kwenda ikulu kwa kudandia lift ya gari bovu liliachwa na ccm! hii haiingiii akilini! huu ni udhalilishwaji mkubwa wa wanamageuzi wote! ndo maana wanamageuzi wa kweli wengi wamepiga u turn! bora tuwape ccm waendelee kuongoza japo kwa miaka mitano ili tujipange upya. kurudisha majeshi nyuma ukijipanga ni mbinu ya kijeshi. kwa hapa tulipofikia tukiendee mbele bila kujipanga upya hatutakuwa na real cause ya kuendelea na mapambano maana majemedali wetu wamepigika kiaakili, wako insane, hawana clear mind. mwanajeshi mtiifu yeyote kinachotakiwa kwa sasa ni kutumia akili na means yeyote kuwawekakando hawa majemedari na kurudi nyuma ili tujipange kuepusha maafa na madhara zaidi.
jeshi letu limeeingiliwa na mamluki aliyokuja nayo huyu mgombea wa kuchonga, wanatutumia tu kwa malengo maalum kwa kipindi huki! tusiiombe wapate wanachotaka! tutalia na kusaga meno jinsi watakavyotutifua! wao hawana chakupoteza!
ndo maana nawaomba sana wanamageuzi tufumbue macho! tafakari watu waliokuwa upande wa pili wamekuja huku kwa wingi na mambo yao yaleyale waliyokuwa wanayafanya kule ikiwemo matusi na kejeli na dharau kwa mtu anaye tofautiana nao mawazo! kwao matusi wala sio issue! kwao kuongopa wala sio issue! tabia ya virusi inapoingia kwenye system ina act kama genuine software kumbe ukishaikubali inaanza kula mafile na hatimaye kucolapse system nzima.
wanamageuzi tuungane kukataa mageuzi ya kitapeli haya ya virusi kwa njia moja tu, tuwape ccm muhula mmoja then kipindi hiki tujipange kwa mageuzi ya kweli.
tupingane na mabadiriko yasiyoweza kuratibiwa.
kama tunaipenda nchi yetu tukatae huu mkusanyiko wa chui wenye njaa wanaohubiri kukomboa kondoo kutoka zizi la simba walio shiba.
wanamageuzi wakweli shime tupigie ccm mwaka huu.

hizi za chadema halisi sijui nini si zilishavuja umu kabla sasa mbona mmezileta hivyo hivyo uku mkiwa mnajua hiyo mikakati ilishavuja umu au hamkuhabarishana kuna mpango umeleak?
 
Hivi hawa Chadomo na Ukiwa, walikuwa hawana mgombea kabisaa.Inanishangaza sana na sijaona mgombea aliyekataliwa kwa kashfa nyingi, eti ndiye mgombea wa Urais Tanzania, duu jamani!! hakukosea kikwete alivyo sema, akili za mwenzakoo changanya na za kwakoo!! yaani hii haitaji elimu kubwa, yaani hata mtoto wa chekechea angejiuliza tu, kabla ya maamuzi.
 
Mambo ya kumshawishi mtu umechelewa watu wanaenda kupiga kura 25 october 2015
 
Kuendelea kubaki chama cha Siasa Hai na Imara,CHADEMA ni lazima mgombea Urais wao ashinde na kutwaa kiti cha urais wa Tanzania; vinginevyo CHADEMA itaifuata NCCR mageuzi kwenye LIMBO.

Body with life but no soul.
Zombie Party
 
Hivi kuna mtu anaweza soma hilo bandiko hadi mwisho? Chadema halisi ni nini....... tulieni October mtapata majibu

UVCCM wana haha sana kuokoa lichama lao. Mara wajiite CHADEMA ASILIA mara mgombea wao ajiite M4C.

Shiida kweli.
 
Back
Top Bottom