Kwa wana CHADEMA halisi

Kwa wana CHADEMA halisi

huna unachojua, mmekuja juzijuzi tu mnajidai wanamageuzi milobobea, muda wote mlikuwa wapi! kama wanaume si mngeanzisha chama chenu muda mrefu!

Rudi ukaanzishe majeshi nyuma.
Sisi majeshi mbele
 
2013, Madela Wa- Madilu,

..siyo rahisi hata kidogo kwa cdm kuzorota kama nccr.

..cdm tayari kimeshaweka misingi ya kitaasisi. Nccr hawakufanya hivyo wakati walipokuwa maarufu.

..cdm pia ina hazina ya viongozi ambao wana wito wa kufanya siasa na harakati. Nccr iliundwa na viongozi ambao walikuwa wanasheria maarufu ni masuala ya siasa walikuwa wanafanya on part-time basis.

..cdm hata wakishindwa wataendelea kuwepo tu na hata kustawi zaidi. Sasa hivi ni wapinzani, kwa hiyo hawatakuwa ktk mazingira yoyote yale mapya ikiwa watashindwa.

..chama ambacho kitakuwa na wakati mgumu ikiwa kitashindwa ni ccm. Hawa wamezoea kubebwa na dola. Pia viongozi wake wengi wapo kimaslahi zaidi, na vilevile hawana mtaji wa viongozi wenye wito wa kufanya siasa za upinzani.

..hivi unategemea watu kama philip mangula, abdulrahman kinana, john magufuli, samia suluhu, january makamba, na wengine wanaweza kuvumilia shuluba na dhiki za kufanya siasa za upinzani ikiwa ccm watashindwa?

..ccm ni sawa na watoto wa "kula-kulala" au "openi-friji", kila kitu wanapewa na baba. Sasa siku baba akitangulia mbele za haki watoto huingia ktk dhiki na mifarakano isiyoelezeka.

Cc ZeMarcopolo, zumbemkuu, Mkandara, NasDaz
Ni kweli kwamba hata kama CHADEMA watashindwa hawatazorota kama ilivyokuwa kwa NCCR lakini ikiwa watashindwa, kule juu kutakuwa na msukosuko sana labda tu ni kwavile Mbowe is untouchable kama ilivyo kwa Maalim Seif vinginevyo, lawama nyingi za kushindwa zitamwangukia yeye kwamba "endapo asingemkaribisha Lowassa, basi haya yasingetokea!" Yanapotokea majanga, kwa hulka ya wanadamu watatafuta mtu wa kumdondoshea jumba bovu!

Wapo pia ambao hivi sasa wamekaa kimya... wapo waliokaa kimya kwa maslahi ya chama lakini pia wapo waliokaa kimyaa kwa kukosa uthubutu wa kutoa hisia zao wazi wazi ingawaje pia wapo waliokaa kimya kwa kuchelea kujimaliza kisha mwisho wa siku Mbowe akaja kuonekana ndio shujaa wa mchezo kwa hatua yake ya kumkaribisha EL! Hawa wote, endapo Lowassa atashindwa, hatimae watajitokeza hadharani na kurusha lawama za waliomkaribisha EL ndani ya CHADEMA!

Nusura ya CHADEMA ni kupata viti bungeni ambavyo, kimsingi hata mimi ambae sitafurahia kuona Lowassa akienda Magogoni lakini nasali CHADEMA wapate viti vingi zaidi vitakavyomaliza nguvu ya CCM bungeni. Lakini ikiwa CHADEMA watashindwa hata kupata viti vingi basi watakuwa kwenye hali ngumu sana na busara ni kwa Mbowe kuachia nafasi ya uenyikiti kabla muda wake haujaisha kuonesha uwajibikaji.
 
Mkuu umenena vema sana, kama hawa hajamaa watakosa kule juu lazima kupasuke na Ili niipende Chadrma tena lazima Mbowe atoke kule juu kabla mda wake haujaisha
 
Ndugu wapenzi na wanachadema halisi wa chadema na mageuzi kwa ujumla, haihitaji kuwa na degree kujua tumesaritiwa na watu tuliwaamini na kuwapa vyeo ndani ya chama chetu ili watuongoze, cheo ni dhamani.
hatutakiwi kubeba makosa ya mbowe wala yeyote, kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe.

Kutuletea mgombea uraisi wa kuchonga ni jambo lisiloingia akilini! katika watu wote ina maana hakuna mtu ambaye hangefaa kuongoza nchi? ina maana chama chetu kwa muda wote ni mamburula?

kweli tunafikia sehem kwenda ikulu kwa kudandia lift ya gari bovu liliachwa na ccm! hii haiingiii akilini! huu ni udhalilishwaji mkubwa wa wanamageuzi wote! ndo maana wanamageuzi wa kweli wengi wamepiga u turn! bora tuwape ccm waendelee kuongoza japo kwa miaka mitano ili tujipange upya.

kurudisha majeshi nyuma ukijipanga ni mbinu ya kijeshi. kwa hapa tulipofikia tukiendee mbele bila kujipanga upya hatutakuwa na real cause ya kuendelea na mapambano maana majemedali wetu wamepigika kiaakili, wako insane, hawana clear mind. mwanajeshi mtiifu yeyote kinachotakiwa kwa sasa ni kutumia akili na means yeyote kuwawekakando hawa majemedari na kurudi nyuma ili tujipange kuepusha maafa na madhara zaidi.

jeshi letu limeeingiliwa na mamluki aliyokuja nayo huyu mgombea wa kuchonga, wanatutumia tu kwa malengo maalum kwa kipindi huki! tusiiombe wapate wanachotaka! tutalia na kusaga meno jinsi watakavyotutifua! wao hawana chakupoteza! ndo maana nawaomba sana wanamageuzi tufumbue macho! tafakari watu waliokuwa upande wa pili wamekuja huku kwa wingi na mambo yao yaleyale waliyokuwa wanayafanya kule ikiwemo matusi na kejeli na dharau kwa mtu anaye tofautiana nao mawazo!

kwao matusi wala sio issue! kwao kuongopa wala sio issue! tabia ya virusi inapoingia kwenye system ina act kama genuine software kumbe ukishaikubali inaanza kula mafile na hatimaye kucolapse system nzima.

wanamageuzi tuungane kukataa mageuzi ya kitapeli haya ya virusi kwa njia moja tu, tuwape ccm muhula mmoja then kipindi hiki tujipange kwa mageuzi ya kweli.

tupingane na mabadiriko yasiyoweza kuratibiwa.
kama tunaipenda nchi yetu tukatae huu mkusanyiko wa chui wenye njaa wanaohubiri kukomboa kondoo kutoka zizi la simba walio shiba.

wanamageuzi wakweli shime tupigie ccm mwaka huu.

LOWASSA hawezi acha ujangili. Mbwa Mzee Hafundishiki Tabia Mpya.
 
Tumekusikia ila hatujakuelewa
Kaungane na doctor Mihogo.alafu ni vzur ukistaafu siasa.
 
huna unachojua, mmekuja juzijuzi tu mnajidai wanamageuzi milobobea, muda wote mlikuwa wapi! kama wanaume si mngeanzisha chama chenu muda mrefu![

Anamaanisha Chadema Asili na Chadema Mbowe. Mbowe kavunja misingi yote ya Chadema na sasa haina tofauti na ccm kwa kumleta fisadi lowasa. Hata wagombea wabunge na madiwani wengi wanaona aibu kumnadi lowasa kwenye kampeni zao. Sisi Chadema Asili tutawapigia kura wabunge na madiwani lkn kura za rais hatupigi tutarudisha tupu. Baada ya uchaguzi Mbowe ajitayarishe kung'atuka!
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Back
Top Bottom