Kwa waliozaa kabla ya ndoa


Inaonekana huyo mkeo anahela kukuzidi.
 
Daaah aisee umenihuzunisha sana. Umebeba mimba miezi tisa....umeenda leba umenyonyesha af mtu anakunyang'anya mtoto hivihivi.....ningekuwa mimi ningemuiba nitokomee nae huko

Umethibitisha ukweli wa maelezo yake? Nimeona mengi sana hapa duniani watu si wakweli hawasemi kwa usahihi ukweli wa mambo.
 
Umethibitisha ukweli wa maelezo yake? Nimeona mengi sana hapa duniani watu si wakweli hawasemi kwa usahihi ukweli wa mambo.

Kwani mangapi yanatusikitisha na kutufurahisha hapa jukwaani ilhali hatujui undani wake? Mimi nimesikitika kwa ku-assume hii ni ya kweli
 

wewe inaelekea hujaolewa jinsi unavyoreason. unadhani wewe ungekuwa na mtoto wa nje mmeo angeruhusu uliezaa nae aje aje kwako eti kumuona mtoto? na angekataa ungemlaumu kama unavyomsema mwanamke mwenzio eti ana visa visivyo na logic?!

nahisi uko kwenye nafasi kama ya huyo dada mwenye mtoto ndo maana unaongea kwa kuwa upande wake. khaaa!
 
Mimi ni mwanaume nilibahatika kupata mtoto wa kiume nje ya ndoa.
Sasa miaka 10 baadae nimeoa na nimemchukua huyu mtoto wangu naishi naye.
Kuna nini kimebadilika mpaka ukaamua kumchukua? Shule? Mama yake hawezi kuendelea kumtunza/kukaa naye? Mama yake ameolewa na mwanaume mwingine?

Sasa mke wangu ameniwekea masharti ambayo nafikiri ni magumu kutekelezeka.
Ni lazima kuwepo na masharti. Suala hili haliwezi kubakia holela na ndoa yenu ikabaki salama.

Naamini kuwa mwanamke niliye zaa naye ana haki ya kumuoma mtoto wake kila anapohitaji kufanya hivyo.
Hakuna haki isiyo na mipaka. Ndio anayo haki ya kumuona mwanaye lakini haki hiyo inaishia pale ambapo haki za wengine (mke wako kwa mfano) zinaanzia. Haki ni lazima iendane na wajibu na pia kuheshimu haki za wengine. Kwa mfano, hana haki ya kuja nyumbani kwako achilia mbali kwa muda anaotaka yeye isipokuwa kama wewe na mkeo (wenye nyumba) mmeridhia.

Sasa mke wangu hataki huyu mama mtoto afike nyumbani kumuona.
Yupo sawa. Mkeo anayo haki ya kuamua ni nani aingie nyumbani kwenu.

Hataki mtoto aende kwa mama yake.
Hapa mkeo anavuka mipaka. Hana haki ya kumzuia mtoto kwenda nyumbani kwa mama yake.

Anataka mama mtoto akitaka mtoto tumtume housegirl ampeleke mtoto hoteli foleni halafu wakimaliza kuongea arudi naye.
Nyie wanne (mume, mke, mama mtoto, na mtoto (miaka kumi tayari anajitambua, ni lazima kupata maoni yake)) muweke utaratibu ambao utazingatia haki na wajibu wa kila mmoja. Bila ya shaka kila upande utalazimika ku compromise ili kulinda haki za wengine kwa kiasi kinachokubalika. Hiyo proposal ya mke ni mmojawapo ya options tu, lakini ningeshauri kuwepo pia na frequency inayoeleweka na isiyoweza kuleta usumbufu usio wa lazima (sio kila akitaka, analetewa!, anaweza kutaka kila siku, mtaweza?) - kwa mfano inaweza kuwa fortnightly au monthly etc. Njia nyingine, badala ya house girl wenu kumpeleka, mama mtoto yeye atume mtu wa kuja kumchukua mtoto. Hata hivyo hili ni suala la muda mfupi tu, akifikisha miaka 12 (anaweza kuwa form one hivi) naamini huyo mtoto ataweza kwenda mwenyewe tu. Wengine huamua kuwapeleka kwa ndugu (mjomba, babu, bibi, shangazi etc) watoto wa namna hiyo. Lakini kubwa katika utaratibu wowote mtakaokubaliana ni wewe kutofanya vitendo vitakavyoweza kuashiria kuwa bado una mahaba na mama mtoto. Hii itampa hofu mamsap wako na hivyo kutokukuamini.

...Hali hii imeniingiza kwenye migogoro maana mama mtoto anaona namnyanyasa na upande mwingine mke wangu anaona pia namnyanyasa.
Kama nilivyosema hapo juu, katika suala hili ni lazima kila upande uta compromise maana ni lazima kuzingatia haki za wote. Bila ya shaka mkeo alijua kuwa una mtoto kabla hajaamua kuolewa na wewe. Suala hili la mtoto wako linaelekea halikuzungumzwa vizuri kipindi hicho. Haya mabadiliko kwa namna moja ama nyngine ni lazima yatamsumbua mkeo hasa kama unakwenda kinyume na matarajio yake. Lakini hilo haliondoi ukweli kuwa ameolewa na mwanaume ambaye tayari alizaa na mwanamke mwingine na hivyo haki zake katika ndoa hiyo kwa vyovyote vile zitazingatia haki za baba wa mtoto, mtoto na mama wa mtoto.
 
Huyo mkeo ana common sense kweli?

wewe ndio huna common sense. wewe ungeoa mwanamke mwenye mtoto ungeruhusu mwanaume alezaa nae aje aje kumuona? hebu jiweke kwenye viati vya huyo mama kabla hujauliza mambo ya common sense bwana.
 

teh!teh! teh! kwani akili za wanawake zikoje!?
 
wewe ndio huna common sense. wewe ungeoa mwanamke mwenye mtoto ungeruhusu mwanaume alezaa nae aje aje kumuona? hebu jiweke kwenye viati vya huyo mama kabla hujauliza mambo ya common sense bwana.

Kuja nyumbani kwangu hapana, lakini siwezi kukataza huyo mtoto asiende kwa baba yake.
 

Aisee umeporomoka utamu sana. Ushauri mzuri sana.
 
Ah mambo mengine kupunguziana siku za kuishi Tu!
 
Hapo hofu ya mkeo ni ww na mama mtoto kupasha kiporo.. cha muhimu wekeni utaratibu wa nyinyi kumuona mtoto bila kuonana... amfuate hapo hotelin amchukue akakae nae muda ukifika amrudishe hapo hotelin simple... nahisi ww ndo umesababisha hayo maana unaeza kuta unaviashiria vya kuendelea kumkubali mzazi mwenzio... ila mkeo mkabaji mzuri, tatizo anasahau haki za mama na mtoto
 

Nimesikitika sana.
 

Wewe kweli extremist. Nimecheka sana.
 
@MBEBA MAONO KAJA kwa nini wanakutendea yote hayo

Pole sana

Mungu wa Mbinguni atakufariji

Damu haipotei

Kila jambo linalotokea ni mpango wa Mungu

Huyo ni mwanao aliyekaa tumboni mwako 9 months.....ni wa kwako

Jipe moyo

There is one day utakuwa pamoja na mwanao

Story yako imenigusa sana

Pole
 
Mi nafikiria tu akili ya mtoto sasa hivi inafikiria nini, i cnt imagine ningekua vipi kama dad kaoa mwingine afu nimekua na mom then niende kuishi kwa dad mom niwe namuona kwa kubahatisha ati hotelini, duh! mkuu kama head inabidi ukae ujifikirie mara mbilimbili maana ushuri wangu kwa sasa ni useless.. Mimi kama nimempa binti mimba hata by mistake huyo ndo angekua mke wangu, ingebidi nijifunze kumpenda tu jinsi alivyo.. Ila hiyo option haitokusaidia maana its too late for u..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…