Kwa waliowahi kupatwa na bomoa bomoa ya makazi tupeni uzoefu

Sep 27, 2015
99
182
Habari wa na JF,

Swala la bomoabomoa ni moja ya jambo linaloweza kuathiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa maisha ya mtu...Hizi bomoa bomoa zinaweza kuwa kwa makosa ya mtu binafsi labda kujenga ndani ya eneo lisilo sahihi au upanuzi wa project mbalimbali za serikali.

Katika changamoto hii tupeane ujuzi na jinsi ya kujiandaa kimwili, kiakili ili kupunguza makali ya hili zoezi kwa mtu husika.

Mimi naweza kuwa mhanga wa zoezi hili kwa sababu ya upanuzi wa project flani ya serikali.

Kulipa watalipa lakini kuna vitu vingine kwenye maisha haviuziki NOTFORSALE na havina BEI (PRICELESS) labda kwasababu ya maana inayobebwa au kumbukumbu inayoletwa na hicho kitu katika maisha.

Mimi binafsi hii nyumba inayotaka kubomolewa ni kitu pekee ambacho kinabeba kumbukumbu ya mama yangu kipenzi , maisha ya utoto na kila kitu kizuri kinachohusu maisha yangu ya utotoni. Kitu kama hichi maishani kwangu sioni kama unaweza kukiwekea bei, lakini wanapokuja kufanya valuation vinavyopimwa ni vitu vinavyoonekana labda na gharama kidogo ya kuhamisha vitu vyako. Wajuzi watueleweshe.

Kitu kingine kinacho nikwaza nikwamba sina uhakika kama wanafikiria umbali wa kiwanja chako kutoka barabara ya lami wakati wanafanya valuation, maana ukisema una unafanya sawa kwa vyote bei haiwezi kulingana hata sikumoja kwenye dunia ya sasa. Wajuzi watueleze.

Je, kama ni project itakayo fanywa na serekali au wawekezaji, naweza kukataa kulipwa nibakiziwe eneo langu ambalo halikiwa mali ya serekali kama mahakama ilivyo ainisha?

Mimi sina mpango wa kukaa katika mji husika (DAR) na ninaishi mkoa wa mbali sana kutoka DAR kama 1200KM.
Je? Nitawezaje na niwapi nitauzia mabaki ya nyumba nitakayo bomoa ili kupunguza machungu
Je? Katika zoezi la kubomoa matofali ,mawe ya chini , mbao za kench, mabati, milango na madirisha vinaweza kutolewa kwa ufanisi unaoweza kufanya vitu hivyo kuuzika kwa bei nzuri.

Je, kwa DAR vitu hivyo nitaviuzia wapi bila mlolongo mrefu kwa bei nzuri ili nikaridi kwenye maisha yangu mkoani?
 
Kubomolewa nyumba bila ya fidia yoyote isikie tu kwa wenzako mzee utalia na kusaga meno ua kufa kabisa kama ndio hapo hapo unategemea na umri umesonga.

But ukilipwa fidia ni shavu, unaweza kutoa milango vizur,madirisha,na matofali (ila sio yote mengi yataharibuka)na mbao na bati (hazitofaa kuenzeka tena labda kujengea banda na matumizi mengine)kuhusu kuuza uza uko uko mwanza huku utapata hasara tu wale madalali wanalilia sana bei vitu vikiwa hvyo,hasa wale wanaovaa kofia za chepeo na mustach, anawaze akakwambia vyote hvyo kula laki moja tu ukalale😁
 
Ungesema nyumba Ipo wapi?

Kuna watu wananunu nyumba hiyo wanavunja wenyewe kila kitu.

Piga hesabu zako vizuri wewe unauza nyumba ila kwa bei ya hasara hasa.
 
Back
Top Bottom