SoC03 Bomoa bomoa ya makazi kilio cha Watanzania

Stories of Change - 2023 Competition

Rayvanny wa jamiiForums

Senior Member
Apr 7, 2023
132
347
BOMOA BOMOA YA MAKAZI
KILIO CHA WATANZANIA

Utangulizi

Bomoa bomoa ya makazi imekuwa ni kilio kikubwa kwa watanzania. jambo ambalo limesababisha adhali nyingi sana kwa wananchi na kupelekea wengi wao kukosa makazi kwa kubomolewa makazi yao na kuangukia kwenye umaskini wa kupindukia. huku waathirika wakuu wakiwemo walemavu, wagonjwa, watoto, wajawazito, vijana na wazee. ambapo kwa asilimia kubwa wengi hujikuta wakigeuka kuwa omba omba wa barabarani na watoto wa mtaani pasipo kutegemea.

FB_IMG_16819569883620658.jpg

FB_IMG_16824283701900632.jpg

(Tazama, Picha kutoka mtandaoni)

Jambo hili limesahulika kwa wengi japo ni janga sugu ambalo siku hadi siku limekuwa likiendelea kujirudia. bomoa bomoa ya makazi siyo kitu kigeni kulisikia masikioni kwa wengi Iicha ya serikali kufanya maamuzi kwa kuchukua hatua kwa kuweka utaratibu wa sheria nzuri ya ujenzi wa makazi, lakini bado kumekuwa na ongezeko la idadi kubwa ya ujengaji usiyo fuata utaratibu wa sheria hizo. Huku mamlaka zinazo husika kwenye ardhi na ujenzi zikiendelea kutoa vibali hivyo vya ujenzi na makazi sehemu zisizo sahihi kinyume na utaratibu wa sheria.
.

Je, sheria zilizopo zimeshindwa kukidhi mahitaji ?
hili ni swali la msingi sana ambalo unaweza kujiuliza kwa sababu nyumba nyingi sana zilizo jengwa kwenye maeneo ya sehemu zisizo sahihi zina vibali vya kisheria vinavyo onesha kuwa eneo hilo limethibitishwa, limekubaliwa, limepimwa na kuruhusiwa na mamlaka husika kwaajili ya kufanya ujenzi wa makazi. sasa linapokuja suala la bomoa bomoa ya makazi wakati wananchi wanavibali ni wazi kwamba sheria zilizopo haziwapi kipaumbele wananchi.

Pengine pia labda ni kwasababu ya uwepo wa wataalamu ambao hawana elimu ya kutosha kuhusiana na jamii. inamaana kwamba wataalamu tulionao wanakiwango kikubwa cha elimu ya uchumi pekee, ni kitu ambacho kinachangia kwa kiwango kikubwa kuleta adhari kwa jamii hasa pale linapo kuja suala la ujenzi wa miradi mbambali ya maendeleo huwa hawaangali adhali zinazo weza kuwapata wananchi.

Mfano mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR jijini dar es salaam iliyopita katikati ya maeneo ya ukonga, ambapo maeneo mengi ya mradi huo wa SGR wakazi wake wanapitia kwenye makalavati ya maji machafu kama njia mbadala ili kujipatia mahitaji yao ya msingi, ni baada ya kuwekewa senyenge yenye ukuta mrefu ulioziba sehemu muhimu kama za vituo vya afya, daladala, shule, sehemu za ibada ambapo sehemu hizo zilitakiwa ziwe na njia. lakini ujenzi wa mradi huo umejengwa kwa kuziba umbali mrefu zaidi bila kuacha njia na ukizingiatia maeneo kama hayo kuna wagonjwa, walemavu, wajawazito, wazee, watoto na vijana.

FB_IMG_16824277490677081.jpg

FB_IMG_16824276551373829.jpg

(Tazama, Picha kutoka mtandaoni)

Ushauri
• Nashauri serikali iwekesheria zinazowapa kipaumbele na wananchi pia badala ya kupendelea miradi pekeyake.
Mara nyingi kwenye ujenzi wa miradi mikubwa ya serikali huwa haiwapi kipaumbele wananchi matokeo yake kupendelea miradi pekeyake ketendo ambacho kinapelekea ukiukwaji wa haki za binadamu mfano wananchi wanapo bomolewa makazi yao wakati wanavibali halali vya kisheria.

• Nashauri serikali kuchukua hatua za kisheria kwa mamlaka zinazotoa vibali vya ujenzi sehemu zisizo sahihi za hifadhi.
Ushauri wangu kwa serikali ni juu ya mamlaka za ardhi na ujenzi. kwa sababu linapo kuja suala la maendeleo hususani kwenye upande wa ujenzi wa miradi mikubwa ya serikali huwa haliepukiki, kama kutakuwa na makazi ya watu kwenye eneo hilo la mradi ambalo lilitengwa kabla ya wakazi hao kujenga nyumba zao na ikiwa watakutwa na vibali vilivyo tolewa kihalali na mamlaka husika za ardhi na ujenzi, ni vyema mamalaka zikachukuliwa hatua za kisheria kwanza kwa kuwajibishwa kwamba ilikuwaje wananchi waruhusiwe kujenga na kupewa vibali kwenye hifadhi wakati wakijua kabisa kwamba kuwa eneo hilo ni kwaajili ya miradi ya serikali badala ya kuwabomolea wananchi ambao wengi wao walikuwa hawajui kuwa eneo hilo ni la hifadhi.

• Nashauri serikali kuunda kitengo maalum kitakachokuwa kina simamia kwa uwazi mfumo mzima wa utoaji wa vibali vya ujenzi wa makazi kisha kitengo kiwe kina wasilisha taarifa kwa serikali.
Kitengo hichi kitakuwa kinasaidia serikali kupata taarifa muhimu ili kubaini vibali vilivyo tolewa kinyume cha sheria kwenye sehemu ambazo zilitengwa za hifadhi kwaajili ya miradi ya maendeleo ili kuchukua hatua mapema kabla ya waliopewa vibali hivyo kimakosa kujenga katika eneo hilo.

• Nashauri serikali wataalamu wa masuala ya ujenzi na ardhi wapewe elimu muhimu zaidi kuhusu jamii.
Wataalamu watakapo pewa elimu zaidi kuhusu jamii kutaleta matokeo chanya kwenye miradi ya maendeleo itakayojengwa karibu na makazi ya wananchi ili izingatie mahitaji ya msingi ya jamii husika iliyo karibu na mradi huo.

Hitimisho
Ninapofikia mwisho naomba nitoe pongezi zangu za dhati kwa jamiiForums kwasababu imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono Uhuru wa kujielezea siyo hivyo tu bali ni chombo pekee kinachotoa nafasi kwa Watanzania kujielezea na kuhakikisha kuwa maoni na mitazamo inayowasilishwa inafika moja kwa moja kwenye mamlaka husika na kufanyiwa kazi. lakini pia mwisho nipende kuiomba serikali ichukue hatua sahihi zitakazo weza kuleta mabadiliko na usawa ndani ya taifa zima kwa ujumla.
 
Ili ujenzi holela uishe twatakiwa kuwa na serikali z mitaa zinazoongozwa na walioelimika
 
Ili ujenzi holela uishe twatakiwa kuwa na serikali z mitaa zinazoongozwa na walioelimika
Ili ujenzi holela uishe twatakiwa kuwa na serikali z mitaa zinazoongozwa na walioelimika
Pia hilo ni jambo la msingi sana lazima tupate viongozi wenye elimu waliovutwa na changamoto za wananchi ili kuweza kutatua moja kwa moja changamoto za wananchi.
 
Ili ujenzi holela uishe twatakiwa kuwa na serikali z mitaa zinazoongozwa na walioelimika

Kuwa na watendaji wa serikali za mita walioelimika tu haitoshi ni lazima wawe pia ni watu wenye hadhi ili waepukane na vitendo vya rushwa.
Tatizo la bomoa bomoa ya makazi ya watu linatokana na watendaji wa serikali kutokufuata Sheria za mipango miji na pia wananchi kuvamia sehemu na kujenga sehemu ambazo hazitakiwi kujengwa!

Hivi karibuni akihitimisha hotuba ya bajeti Waziri Mkuu alielekeza wizara ya Maliasili kutokungoja wananchi wavamie na kujenga/ kulima ndani ya hifadhi za Wanyamapori ndio wazinduke na kwenda kuwabomolea makazi yao ndani ya hifadhi! Ni jukumu lao kuhakikisha kuwa wananchi hawavamii mapori hayo ili kuepusha kuja kuharibu mali zao baadae!

Hili ni agizo ambalo linatakiwa litekelezwe na wizara nyingi zikiwemo TAMISEMI na wizara ya Ujenzi ; Kwani bomoa bomoa nyingi zinafanyika mijini na sehemu ambako barabara zinajengwa. Mijini viongozi wa wilaya wakimo MaDC na Wakurugenzi wao wanawaacha wananchi wakianza kujenga sehemu zisiruhusiwa mpaka sehemu hizo zinakuwa makazi makubwa ndipo wanazinduka kwenda kuwabomolea watu Nyumba zao ; laiti wangewasimamisha mapema hasara inayopatikana kwa bomoa bomba hizi ingeweza kuepukika!

Hivi ninavyoandika kuna sehemu kule MBEZI BEACH ufukweni karibu na Nyumba ya bwana RUPIA. Kuna open beach space ambayo watu wamevamia na kujenga na kufanya biashara zao pale, walianza kidogot kidogo na sasa pamekuwa kama kijiji cha makazi. Kitu cha kushangaza DIWANI wa Kawe anapita sehemu ile kila leo { Kama hajaenda TABATA!!} na anawaona jinsi wanavyojenga lakini hakuna hatua inayochukuliwa kuwasimamisha. Itakuja wakati kijiji kimekua kikubwa na uchafuzi wa mzingila umekithiri ndio wahusika watazinduka na kuja kubomoa hayo makazi!! Kumbe wakiwasimamisha mapema hasara ya kuwabomolea ingeweza kuepukika! Hili ni suala ambalo Viongozi wa wilaya ya Kinondoni hawana budi kulishuhulikia haraka.
 
Je, wakazi wa maeneo hayo hawana vibali vya kisheria Unaweza kushangaa kuwakuta wakazi hao wanavibali sasa tutasemaje wamevamia wakati wana vibali vya ujenzi na hati ya umiliki wa eneo hilo kutoka kwenye mamlaka za ujenzi na ardhi ?

Ni vyema kukata mizizi ya mti kuliko kukata matawi madogo madogo hizi mamlaka za ardhi na ujenzi zimejaa rushwa na linapukuja suala la bomoa bomoa ya makazi kunakuwa na ushahidi kabisa kwamba wananchi wote walio jenga maeneo ya hifadhi wanavibali kutoka kwenye mamlaka za ardhi na ujenzi alafu serikali hata haizichukuli mamlaka hatua zozote za kisheria wakati ushahidi upo.

Eneo hilo utakuta kuna viongozi wa serikali Wa ngazi mbalimbali wanajua kinacho endelea hapo ila wamekaa tu kimya mpaka siku ya bomoa bomoa ndiyo wanajitokeza hii siyo sahihi
 
e, wakazi wa maeneo hayo hawana vibali vya kisheria Unaweza kushangaa kuwakuta wakazi hao wanavibali sasa tutasemaje wamevamia wakati wana vibali vya ujenzi na hati ya umiliki wa eneo hilo kutoka kwenye mamlaka za ujenzi na ardhi ?
Mfano huo niliotoa wa Mbezi Beach hiyo ni open space ufukweni ambapo haparuhusiwi watu kujenga!! Sidhani kuwa wamepewa vibari vya kujenga hapo ; inaelekea walibeep wakaona kimya nao wakaendelea!! Rushwa inaweza kuwa imetembea kwasababu DIWANI wa Kawe anaishi sehemu hizo lakini anajifanya hajui kitu kinachoendelea1
 
Kwa mkoa mkubwa kama dar es salaam tena maeneo maarufu ya mbezi beach kwamba wananchi waje wajenge sehemu mpaka ifikie mtaa wenye watu wengi hivyo alafu ni dar es salaam sizani Kama mamlaka hazina taarifa kuhusu hilo au hazijawapa vibali wakazi wa napo.

Na kama kuna mkazi amejenga kwenye jiji kubwa kama dar alafu mamlaka isijue chochote basi kuna pengo kubwa kwenye uwajibikaji Lazima mamlaka zinajua kila kitu na viongozi wa ngazi mbalimbali karibu na maeneo hayo wanajua kinachoendelea.
 
Ni kweli inawezekana wahusika kwasababu ya rushwa wanalifumbia macho suala hili!
 
Ni kweli inawezekana wahusika kwasababu ya rushwa wanalifumbia macho suala hili!
Lazima kuwe na sheria zitakazo wapa kipaumbele wananchi ili haki itendeke endapo likija suala la bomoa bomoa ni vyema serikali ikaanza na mamlaka, pamoja na viongozi walio fumbia macho jambo hilo ambao wameruhusu wakazi hao wajenge kwa sababu ni wajibu wao Kama viongozi kuzuia huo ujenzi holela.
 
Back
Top Bottom