Kwa waliosoma Forodhani shule ya msingi

Kwa waliosoma Forodhani shule ya msingi

mwalimuu siwa alikuwa na upendo sana kama mwl ngongo, ehhh mnalikumbuka darasa la vidudu la mbao lile
 
Kuna anayemkumbuka yule baba alikuwa ana mguu mmoja amepiga kambi nje ya snow cream anaomba msaada? Baadae akawa anauza korosho. Kuna siku nilimkuta pale karibu na Imalaseko amepiga kambi, naona alihama baada ya snow cream kuisha umaarufu kama miaka 4 ilopita.

namkumbuka alikuwa na mguu wa bandia,sema wkt ule niwachache sana walikuwa wanakula ice snow cream...mm mpaka nikala kwa ukauzu
 
Du! mkuu mleta mada ahsante kwa kutukumbusha.

Nafikiri Forodhani ilikuwa ni moja ya shule maarufu sana lakini ngumu kupata nafasi kama ilivokuwa Bunge na Muhimbili.

Pia ilikuwa na sifa kwamba ni shule ilokuwa na uwezo wa kuchukua watoto wa kutoka kwenye familia za wenye uwezo na hata wale wa kutoka kwenye maisha ya kawaida tu.

Mimi nilikuwa katika moja ya madarasa ya kwanza ya A na B yaloanza mwaka 1983 baada tu ya kumaliza vidudu pale kwenye vijumba vilivyokuwa katikati ya shule.

Walimu tulokuwa nao wakati ule walikuwa ni walimu hasa na si walimu wa leo, kwani walikuwa wanafanya kitu kizuri kuimarisha misingi ya kwenda nayo maishani iwe kuendelea na kidato cha kwanza au kwenye vyuo vya ufundi.

Mwalimu Mbazigwa Hassan alikuwa ni mwanaharakati na siasa ilimkaa mwalimu yule na hasa nyimbo zake za uhamasishaji kama ule wa Amandla Ngawethu na ule alokuwa akitaka tuseme kila asubuhi kama ule wa "Our Motto is peace to All, we are! goodmorning sir".

Mwalimu Julius na fimbo zake za kila asubuhi kabla hajaanza kufundisha ndio ilikuwa ni sifa yake kuu. Hivyo kila mnapoanza mwaka kwenda pale darasa la tano pale kwenye kona chini au kule juu. mnakuwa mnajiandaa kwa fimbo za asubuhi asubuhi.

Kulikuwa na mzee Mselem ambae mihogo yake ya kuchemsha na kachumbari ilikuwa kiboko na alipoondoka yeye nadhani ndio akaja Mangi.

Nafikiri Mangi alipata bahati ya kuwa pale kukaanga viazi kwa sababu ya Mwalimu mkuu mama Mbuya. Yule mama alikaa kiualimu hasa na hakuwa na mchezo.

Walimu wote walotajwa walikuwa walimu hasa na sidhani kama hawa walimu wa leo wa shule za msingi wana uwezo kama ule wa wale walimu wa wakati ule.

Mwalimu Matata alikuwa na tatizo moja, alipokuwa akiandika ubaoni hakutaka mtu aongee na nafikiri alikuwa na tabia ya kujihisi kiaina kwamba labda watu wanamzungumzia.

Mwalimu Nyalika ambae alikuwa akifundisha Kiingereza nilipenda swali lake la "isn't it" alipomaliza kuelezea sentensi au kuelezea jambo. Alikuwa na wanawe palepale akina Timothy.

Mwalimu Manyama alikuwa mkali sana kama mwalimu sister Kimathi ambae alipenda kufinya. Mwalimu Manyama alipenda kutoa nasaha na sera nyingi juu ya mkosaji na hata kuweza kukwambia kwamba kama "ukifeli darasa la saba utakuwa mgeni wa nani".

Kuna akina Mwalimu Bange ambae alikuwa ni mpole lakini mkali wa hesabu, Mwalimu Ruta, Mwalimu Msaki, na walimu wengi tu walokuwa wanachangia kile chumba cha walimu kule juu au Staff Room.

Jamani mnakumbuka tulikuwa tukigawiwa madaftari na maziwa ya bure kabla ya kufutwa tulipoingia darasa la nne kama sikosei.

Pia tulikuwa tukienda kanisani kila jumatano St Joseph na ukichelewa inakuwa bahati yako kwani watu wanakuwa kanisani.

Halafu kuna anaekumbuka yule mwenzetu ambae aliingizwa chupa kichwani kwenye mazingaombwe ambayo yalikuwa yanaenda na wimbo wa dekidekidedee!

Nje ya shule nakumbuka Tanzania Elimu Supplies ambako tulipata madaftari na mikebe ya rula. Snow Cream na Salamander.


Ni mambo mengi sana kwa kweli ya kukumbuka.

NB:
Richard anaishi katika moja ya nchi za Ulaya na yupo huko tangia mwaka 1998
 
namkumbuka alikuwa na mguu wa bandia,sema wkt ule niwachache sana walikuwa wanakula ice snow cream...mm mpaka nikala kwa ukauzu

Mimi nilikuwa na mawazo kwamba yule jamaa alikuwa ni jasusi.

Wewe utakaaje mahala kama pale Snow Cream kwa miaka yote ile ukisafisha viatu tu?
 
wewe na mimi tumemaliza mwaka mmoja. tunafanyaga re union sana. kwenye harusi ya edward tulikutana classmate kama 50 hivi. na juzi kwenye msiba wa mama yake mary lyimo wadau kibao walikuwepo.

tuna group la watsup na facebook linatuunganisha sama.

ni kama kikundi cha kusaidiana shida na raha.

kwenye wedding ya edward forodhan 2000 tulitoa zawad fridge mpyaaa kwa kuchanga wote

na kwenye msiba wa mama mary target kukusanya laki 8 rambi rambi yetu na bado zinakusanywa

wewe itakuwa ulimaliza na kina kabila,ndomondo,adam,kelvin na ndugu yake,na wengine sikumbuki vizuri majina yao.
 
hahahahahahaha.....Judith swai alikuwa na kidoti,judith mwaingne alikuwa anaweza kuandikia mikono yote miwili,zuwena kiyungi,doborah,gerald katawany,b malingula,andrew,macdonald,hassan,bone stiven,kibacha,george,lilian mbeya,susan walikuwa wawili mnene na mwembamba,juma,gudluck,frank mkwiche,daudi,brenda,dalali,hans,adam kizua... i wish nikumbuke majina ya darasa zima la B.
 
yap,Assenga siwez kumsahau.kuna jamaa tulikuwa nae darasani hakuwa mpenda shule.mwal. Assenga alikuwa anamnunulia madaftali na kumkagua kila siku,nakumbuka alikuwa anaitwa Abdul.aliishia darasa la nne huyo jamaa kama sikosei.
 
yap,Assenga siwez kumsahau.kuna jamaa tulikuwa nae darasani hakuwa mpenda shule.mwal. Assenga alikuwa anamnunulia madaftali na kumkagua kila siku,nakumbuka alikuwa anaitwa Abdul.aliishia darasa la nne huyo jamaa kama sikosei.

Kuna rumors Assenga aligongwa na njemba moja hv mwanafunzi. Jamaa alikuwa jibaa kishenzi. Darasa alilokiwa anasoma ni lile karibu na wauza chips karibu na vyoo vya kiume.


The king.
 
Jamani shikamooni humu kumbe kuna watu tunawakosea adabu wameenda age namna hii? Kuna mdau hapo kamaliza standard 7 mwaka 1988!


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
wewe itakuwa ulimaliza na kina kabila,ndomondo,adam,kelvin na ndugu yake,na wengine sikumbuki vizuri majina yao.

Wekeni hiyo groupyenu ya whatsup to join nimeipendahiyo
 
Jamani shikamooni humu kumbe kuna watu tunawakosea adabu wameenda age namna hii? Kuna mdau hapo kamaliza standard 7 mwaka 1988!


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app

Naniliona unamrushiaga madongokama mkweo ndiomana naogopakujibu mtu ovyo ata akiniuzi navumilia

Lo
 
Kwanzaa nawashukuru walioniombea Nimefika ssalama arusha

leo nataraji kumuaga dadayangu mtmeru hosp
tumpeleke marangu kwenye nyumbayakeyamilee Bado na long jny
 
Back
Top Bottom