Siku moja bhana umeme ulikatika bwenini kuna dogo akawa anarushia watu viatu kwenye vyumba vyao..
Bahati mbaya kiatu kikanipata nikamtamfuta nikampata nikampa Onyo,kwasababu nilikuwa muhuni sana pale shuleni kila mtu alishangaa nilipomsamehe yule dogo..
Nikarudi chumbani kwangu huku kuna giza kali ile napanda tu kitandani kiatu hicho shavuni..
Nikamfuata Dogo Nikapiga kichwa kwasababu ya giza sijua napiga sehemu gani kile kichwa kikampata kwenye mfupa wa pua..
Dogo si akaanguka hapohapo huku damu zinamtoka puani alaf kama anashindwa kuhema nikajua nimeua ile nabeba bengi langu nitoroke Mlinzi wa bweni akanizuia kanishikilia mpaka asbuh dogo akakimbizwa hospitali..
Asubuh naingia school nilifurahi kumuona dogo mzima kasimama na head master..
Kuna mwalimu alikuwa anaitwa NDITI alikuwa na mwalimu wa nidhamu alafu hanipendi kishenzi hapo amesha attempt mara kibao kumshawishi head master nifukuzwe shule ila Head master alikuwa anakaza kwasababu nilikuwa naongoza darasani hvyo akawa anasema huyu ataitangaza shule Form4..Basi hiyo ndio ikawa chance ya Tr.Nditi bhana akashawishi kishenzi nifukuzwe..
Head master akaingia ofisini ikapigwa kengele ya dharura m nikajua hapa ndio mwisho wangu kusoma AGAPE,nikashanga head master ananipa sunspaaa ya wiki mbili tu..
Tr.Nditi alikasirika sana kwasababu wiki kazaa nyuma alinikuta Bar nimetoroka shule usiku akamwambia Head Master nikapewa tu adhabu ya kulima shamba la shule huko kwenye shamba la shule kuna ukuta wa bweni la wasichana nikatoboa katundu kadogo nikawa nachungulia mabinti wanavyooga, Tr.Nditi anakuja kukagua nilivyolima anakuta mtu nachungulia mademu akaenda kusema tena Kwa Head Master ,akashangaa Head master kaniambia tu andika barua..
AISEE MIMI NA HEAD MASTER TULIKUWA ZAIDI YA MAGUFULI NA BASHITE..