proskaeur
JF-Expert Member
- Mar 8, 2017
- 1,571
- 4,925
Habari za asubuhi wapendwa,
Lengo la kuanzisha uzi huu sio kujisifia kwa kupewa suspension shuleni, najaribu kukumbuka tu yale yaliyofanya nikapewa suspension shuleni.
Nakumbuka katika maisha yangu ya shule nimebahatika kupigwa suspension mara mbili, ya kwanza nikiwa o-level na ya pili nikiwa advance.
O-level nilipgwa ban shuleni kisa tu nilimbishia mwalimu darasani kwa alichokua anafundisha alkua anakosea sas kumwanbia ukwel ikawa nongwa nikapigwa ban ya wiki mbili.
Advance nikala ban kwa kumtukana mwalimu mkuu mbele ya walimu wenzake,
kulkua na kikao cha wanafunzi na waalimu, sasa katika ku-present hoja nikajikuta mizuka imenipanda nikamropokea mkuu wa shule, hapo ndio nilisoma namba maana nilikula ban ya mwezi na wiki mbili plus kupewa barua ya kupitisha kwa Afisa elimu wa wilaya yangu nakotokea.
Sasa kimbembe kikaja kwenye kupeleka barua isainiwe na Afisa Elimu wa wilaya, nilimkuta Afisa Elimu complicator balaa, cha kwanza akanambia nitafute fimbo anipigie ofisini kwake halafu ofisi yake iko mjini ghorofa kama ya pili hivi, nikashuka kutoka juu nikazunguka kwa nyuma ya jengo nikamkuta mlinzi mmoja nikamuelezea situation nzima akanikatia fimbo, sasa naanzaje kupanda nayo juu ukawa mtihani mwingine.
Lakini nashukuru nilipompelekea fimbo akasema alikua ananijarbu kama naweza kuleta au nitafanya kiburi, akadondosha sahihi nikarudi zangu school, kila nikikumbuka huwa nabaki kujicheka mwenyewe.
Karibuni wadau kwa aliyewahi kula ban enzi za shule tupeane experience ilkuaje na ni nini kilisababisha upigwe suspension?