Nilikuwa nje nimechelewa kuingia darasani kwa dakika chache.
Nikamkuta mwalimu darasani ana beef na wanafunzi hawajamsalimia vizuri (mwalimu alikuwa mnoko tu, wanafunzi hawamfagilii).
Basi nikaingia, nikakuta darasa zima limesimamishwa, sijui sababu.
Mwalimu akaanza kuwachapa wote.
Akafika kwangu, anataka kunijumuisha.
Nikamwambia, kama mwanafunzi sina tatizo na kuchapwa na mwalimu,ila nataka kuelezewa tu nilichokosea ni nini na kwa nini anataka kunichapa.
Mwalimu akakataa kunielezea, anataka kunichapa tu. Nikamwambia hujanichapa hivyo bado.
Akawa anataka kunichapa ovyo mwili mzima na fimbo yake.
Nikaichukua fimbo nikaivunjilia mbali, mashetani yakanipanda, nikamkunja, nikamkwida, nikamsukumilia mbali.
Nikapandisha mashetani zaidi na kuanza kumpaka kwa sauti ya juu sana ya hasira,akakimbia darasanikwenda kushtaki kwa walimuwenzake huko.
Nilipewa adhabu kali lakini nilisimamia haki yangu ya utu. Masela walinisaidia kumaliza ile adhabu kali.