Kwa wale wazee wa suspension shuleni

Habari za asubuhi wapendwa,

Lengo la kuanzisha uzi huu sio kujisifia kwa kupewa suspension shuleni, najaribu kukumbuka tu yale yaliyofanya nikapewa suspension shuleni.

Nakumbuka katika maisha yangu ya shule nimebahatika kupigwa suspension mara mbili, ya kwanza nikiwa o-level na ya pili nikiwa advance.

O-level nilipgwa ban shuleni kisa tu nilimbishia mwalimu darasani kwa alichokua anafundisha alkua anakosea sas kumwanbia ukwel ikawa nongwa nikapigwa ban ya wiki mbili.

Advance nikala ban kwa kumtukana mwalimu mkuu mbele ya walimu wenzake,
kulkua na kikao cha wanafunzi na waalimu, sasa katika ku-present hoja nikajikuta mizuka imenipanda nikamropokea mkuu wa shule, hapo ndio nilisoma namba maana nilikula ban ya mwezi na wiki mbili plus kupewa barua ya kupitisha kwa Afisa elimu wa wilaya yangu nakotokea.

Sasa kimbembe kikaja kwenye kupeleka barua isainiwe na Afisa Elimu wa wilaya, nilimkuta Afisa Elimu complicator balaa, cha kwanza akanambia nitafute fimbo anipigie ofisini kwake halafu ofisi yake iko mjini ghorofa kama ya pili hivi, nikashuka kutoka juu nikazunguka kwa nyuma ya jengo nikamkuta mlinzi mmoja nikamuelezea situation nzima akanikatia fimbo, sasa naanzaje kupanda nayo juu ukawa mtihani mwingine.

Lakini nashukuru nilipompelekea fimbo akasema alikua ananijarbu kama naweza kuleta au nitafanya kiburi, akadondosha sahihi nikarudi zangu school, kila nikikumbuka huwa nabaki kujicheka mwenyewe.

Karibuni wadau kwa aliyewahi kula ban enzi za shule tupeane experience ilkuaje na ni nini kilisababisha upigwe suspension?
Nakumbuka kipindi hicho nikiwa Mosho shule fulani kubwa nilikamatwa ma kesi ya simu iliyonifanya nipelekwe adi kituo cha polis ndio ilikuwa sunspension ya kwanza olevel advance nilipata tatu mbiliza mwanzo ilkuwa kumiliki simu na kutohudhuria vipindi ya mwisho tulikamatwa na simu baada ya inspection kali kupitishwa then wenye simu zetu tukashinikiza mgomo shule nzima ndo nikapatikana katika hatia ya kushinikiza mgomo daah mpaka leo matecher haawaamin kama mimi nilitia kijiti tena PCM but huwa nikikumbuka nacheka sana na sijutii tenaa maana naona ni kama historia katika maisha yangu ahsantee Mungu leo naziona ndoto zangu japo nilikutana na vikwazo vingi vya kukatisha tamaa
 
O level nilikula Ban moja ya wiki 2 kisa mimi mtu wa mkoa wa Mara..Mwalimu hataki nijieleze, kauli mibu, fimbo kwanza!

Mungu ni mwema nikafaulu!

Advanced level nako majina yakawa yananiponza, kila mwalimu ana-assume mkurya ni mkorofi, dah!

Nako nikala moja yangu binafsi, moja nyingine ya shule nzima!..

Napo nashukuru Mungu nilifaulu!

Sasa tena tumepewa suspension ya ajira na Magu...dah!

Mungu ni mwema, naamini nitatoboa na hapa, nitakuwa na maisha mazuri sana, I am still struggling!
 
Nilimtiaga Mimba Mtoto wa Mwalimu Mkuu, Nikapigwa Suspension ya Miezi Sita (Shukrani kwa Wazee Wangu walikaa na Mwalimu Mkuu kiutu Uzima) kipindi hicho niko form two...Nikaamishwa shule na kuletwa Day, Nilipofika Form Four nilimtia Mimba beki tatu wa mwalimu wa Nidhamu, Nikapigwa Suspension mpaka mtihani wa Mwisho (NECTA)...Kutokana na hiyo misukosuko Watoto wangu huwa nawaitaga Suspension Squad (SS)
 
Mi nakumbuka nilikula suspension ya kukaa chaka AkA Dago Maeneo ya Bundikani sec Aisee Nakumbuka Tulikurupushwa Na wagambo Mpka shule Tukala kipigo na Mkuu wa kituo cha polisi Halafu tukala Ban ya wiki 2 Dah ctasahau
 
Nimesoma olevel 4 nlianza na government nkampiga ticha manat nkàpigwa ban miez mi2 ckurud nkaomba private hapo shule mbil nkapigwa ban moja kutembea na mtoto wa head na ya pil kwenda kucheck uefa ucku.... Nkahamia shule ya NNE nkapoa nkamaliza kimagumashi ... Mmmmh sitakag kukumbuka
 
Nikiwa form two nilipewa suspaa kwa kumkata njuka mkia aafu ilikuwa shule ya day huko.

Miezi miwili home aafu narudi nikafikia pepa nikalichapa vizuri.

Siku nyingine tulimchapa viboko ticha usiku alikuwa anakula mundende kwa mwanafunzi wa kike msituni. Akajua ni sisi tu maana tulikuwa wakorofi.
Akaniwinda, siku moja kanikuta nimesimama na msichana nampiga sound.
Nikapelekwa kwa head master na kuambiwa nikalete mzazi.
Nikapewa adhabu ya kuchimbua visiki 10.

Nikalipa mtu akaenda kuvichimba kumbe yule mwalimu anafuatilia. Alivyojua nikaambiwa niandike barua ya kujicommit kuwa nikirudia kosa nifukuzwe shule.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom