Kwa wakristu wote, imfikie hadi papa, wazo la kuboresha kiapo cha ndoa cha kikristu

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Mar 29, 2022
2,396
3,068
Mambo yanasonga na dunia inabadilika.

Kama tuliweza kukaa na kujadili tunafanyeje kuhusu masuala ya ndoa na ubatizo wa watu wale, basi tunaweza kukaa na kujadili kuboresha mambo mbalimbali.

Siamini kama maelekezo yote yanatoka top down tu. Naamini yanaweza pia kutoka down up. Maji yakapanda mlima!!

Na kutokana na viongozi wakubwa kwa baadhi ya dini kutokuoa basi ni muhimu zaidi kusikiliza mapendekezo toka kwa walio field mojakwa moja. Kama jeshini tu.

Oneni. Katika kiapo kilichopo, kinachovuma makanisani kina mapungufu. Ukitulia ukachunguza unaona ni kama kujinenea laana iliyofichwa katika baraka za hapa na pale.

1. Tunapaswa kuamua kuwa tunachotaka katika ndoa yetu sio shida na raha (sa ndo nn) bali tunaitaka furaha tunapopitia yote ya maishani

2. Tunapaswa kuamua kujiombea maisha ya milele na sio kukipa promo kifo, ati kitutenganishe. Unajuaje kama hakuna uwezekano tukawa mabest hata huko mbinguni.

3. Umaskini na utajiri kwanza hata haimake sense.

4. Tuitake afya na tuwe na shukrani maana hata magonjwa mengi ni matokeo ya kuwa na afya. Hivyo tukubaliane kuitunza zaidi. You are never a sick person trying to regain health. You are a healthy person keeping it that way and fighting diseases (Imetoholewa toka kwa Mazed Charahani)

Ebu soma kwa utulivu hiki kiapo:

Screenshot_20231127-154332_Chrome.jpg

Sie waamini, wenye imani. Ni kwa nini tusijinenee mema kila wakati. Tunaweza kuiacha kusema waziwazi. Tukaziacha imejificha hizo laana za kifo, shida, magonjwa na umasikini. Tukasisitiza zaidi katika baraka za furaha, afya na utajiri🤔

Nisiwachoshe sana pendekezo lenyewe hili hapa:
Screenshot_20231207-121944_Notein.jpg

Nyongeza: Kuhusu kifo: Sijakikataa kifo kutokuwepo, bali nimesema hakina haja ya kupewa nguvu ya kutenganisha watu. Wapendwa wanaweza kuendelea kuhusiana kwa mahusiano mbalimbali hata kama marafiki au washirika hata wakiwa huko mbinguni. Mradi tu wameamua kuendelea kuwa washirika kwa upendo na hiyari.

Kwani wanaposema mbinguni tutawaona wapendwa wetu unadhani ina maana gani?

Kimsingi nnaona kama kauli ya kifo kututenganisha haina maana njema kwanza hatujui kikamilifu baada ya kifo. Na ni kutukuza kifo (usingizi mfupi tu).

Au nyie wenzangu bado mnaamini tutakuwa formatted memory na kila kitu? Unafahamu kiuhalisia ukifanya hivyo then huyo mtu husika anakuwa amekufa. Sasa hujui kama kumbukumbu za zamani zinahusisha pia watu na ndizo zinamdefine mtu🤔 cmoooon bhanaa wake up🤨.

Pia ni kutokuwa na imani kwamba wote tunaweza kuokoka na kuurithi uzima wa milele yaani ni upungufu wa imani to the core.

Itoshe tu kusema kuwa 'Ninakubali kuishi nawe maisha yetu yote, wewe uliyekubali kuambatana nami maisha yetu yote' Hili ni jambo endelevu.

Ps: Kwa makanisa ya kiroho, ya manabii na mitume ambao ndio maaskofu haohao naomba mlitafakari halafu muwe wa kwanza kuifanya hiyo reform. Hamnaga bureaucracy nnajua. Roho wa Bwana akaseme nanyi🙏

Muwe na siku njema
 
Hata mimi naunga mkono hoja.
Sijui nani mbunifu wa kwanza wa hicho kiapo.
Inaonekana alipitia taabu nyingi sana.
Mkristo hana shida, ni mitihani tu ambayo akifudhu anahama daraja.

Huwezi kuingia kwenye familia ukiwa umejiapizia mashida.
 
We ni mjinga au mpumbavu..haya maisha ya Duniani penda usipenda kuna kupitia shida hata kama unamali, kwahiyo mkikumbwa(mkipata) na matatizo muachane...jaribu kuface reality na facts..unaweza ukawa pesa ukapata magonjwa ya ajabu,ajali n.k..acha hizo
 
We ni mjinga au mpumbavu..haya maisha ya Duniani penda usipenda kuna kupitia shida hata kama unamali kwa mkikubwa na matatizo muachane...jaribu kuface reality na facts..unaweza ukawa pesa ukapata magonjwa ya ajabu,ajali n.k
Usijitabilie shida.
Maneno yanaumba
 
Tunapaswa kuamua kujiombea maisha ya milele na sio kukipa promo kifo, ati kitutenganishe. Unajuaje kama hakuna uwezekano tukawa mabest hata huko mbinguni.

Mkuu unajua faida za watu kufa ni nyingi kuliko hasara?
 
Unajuaje kama Mungu anaweza kuwachukua wote na gari la moto kama eliya.

Mambo ya imani yaende kiimani sio uhalisia
 
Unajuaje kama Mungu anaweza kuwachukua wote na gari la moto kama eliya.

Mambo ya imani yaende kiimani sio uhalisia
Sina tatzo mkuu na ngoma ya juma na uledi, ila kufa ni njia ya asili kabisa ili maisha yaendelee kuwepo , hakuna uhai bila kifo na hakuna kifo bila uhai.
 
Sina tatzo mkuu na ngoma ya juma na uledi, ila kufa ni njia ya asili kabisa ili maisha yaendelee kuwepo , hakuna uhai bila kifo na hakuna kifo bila uhai.
Ona chief;

Uhai ndio kitu kipo.

Kikikosekana tu ndio hiyo hali huitwa kifo.

Kwa hiyo inawezekana kabisa kukawepo na uhai bila kifo. Kifo sio lazima.

Ni sawa na mwanga na giza: Mwanga ndio kitu kipo, kikiondoka ndio utapata giza.

Unapolikubali giza na kulipa uzani sawa na mwanga hauutendei haki mwanga.

Iweke sasa kwenye muktadha uhai na kifo
 
Mkuu umechambua vitu bila kujerea topic ya kutegemea kwa viumbe hai darasa la sita .

Je wajua kwenye biblia yako hakuna sehemu iliyotaja Hadith ya Mungu aliumba giza? Kuwa giza lilikuwepo tu ndio akafanya mwanga?
 
Ona chief;

Uhai ndio kitu kipo.

Kikikosekana tu ndio hiyo hali huitwa kifo.

Kwa hiyo inawezekana kabisa kukawepo na uhai bila kifo. Kifo sio lazima.

Ni sawa na mwanga na giza: Mwanga ndio kitu kipo, kikiondoka ndio utapata giza.

Unapolikubali giza na kulipa uzani sawa na mwanga hauutendei haki mwanga.

Iweke sasa kwenye muktadha uhai na kifo
Uhai na kifo ni kama sarafu , kuna upande wa kichwa na mwenge kuunda sarafu moja.
 
Kabisa, hili nishawahi kuliandikia blogu kabisa kwamba.

View attachment 2835651

Kifo kama tunavyokifahamu, sio lazima.

Link yake inachelewa kufunguka lakini ukitulia itafunguka utasoma na utaiona point. Tafadhali wote mtakaombishia matunduizi muisome👇
Sio lazima mtu afe. Hapo ndio huwa nawashangaa watumishi wanaohubiri maswala ya vifo.

Musa alikuwa mtu kama wewe. Aliuliwa na Mungu, alafu akamtumiq malaika kumfufua na kumpeleka mbinguni.

Hata wewe ukiwa na mahusiano na Mungu anaweza kukufanyia zaidi ya hilo.
Tusimuwekee Mungu mipaka
 
Tatzo ni pale tunapolazimisha hadithi za kwenye vitabu viwe kwenye uhalisia , kama unauhakika na unachokiamini fanya kama story ya eliya moto utoke juu tuone.
 
Tatzo ni pale tunapolazimisha hadithi za kwenye vitabu viwe kwenye uhalisia , kama unauhakika na unachokiamini fanya kama story ya eliya moto utoke juu tuone.
Sio mimi Kufanya Mungu afanye. Anawezs akitaka. Na haihitaji kufanya ili aonyeshe watu. Ndio maana hilo tukio liliwahusu wt wawili
 
Sio mimi Kufanya Mungu afanye. Anawezs akitaka. Na haihitaji kufanya ili aonyeshe watu. Ndio maana hilo tukio liliwahusu wt wawili
Hizo ni imani tu , mimi siamni Mungu na wewe unamini tunaweza tukafanikiwa kimaisha au tusifanikiwe kwa sababu mbalimbali na sio uwepo wa Mungu .

Mimi nisiye amni uongo wa uwepo wa Mungu , ni sawa tu na wewe unaeamini uongo wa uwepo wa mungu , tukikaa kwenye level moja ya ufikiri . ila fikra zetu tofauti kuelekea utendaji wetu ndio zitakua na nguvu ya kubadili matokeo yetu.
 
Kuamini mamno ya fikra ni dini mpya asili yake mashariki ya mbali. Unaamini miungu ya kihindi bila kujua
 
Back
Top Bottom