Kwa Wajasiriamali wa Kilimo cha Mazao ya Chakula/wafanya biasahara wa nafaka za chakula

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,914
Wakuu kuna kila Dalili kwamba DUNIA inaenda kukumbwa na Uhaba wa Chakula ambao wachunguzi wanadai haujawahi tokea tangia Kuumbwa kwa Hii Dinia, Hali ni Mbaya sana USA na Marekani inaenda kukumbwa na Uhaba mkubwa kabisa wa Ngano na Mahindi, ila kwa USA wao wanatumia sana NGANO na Kiangazi ambacho hakijawahi onekana USA kimepelekea Upungufu mkubwa wa Mavuno ya Mahindi na Ngano

Hali si shwari kwa URUSI tena, URUSI ni Nchi ya Pili kwa Kuzalisha NGANO BAADA YA USA, na zote zina Ukame mkubwa sana

jammas.hussain20120719014603903.jpg

Mahindi yakiwa yamenyauka huko USA
ap_us_indiana_drought_16Jul12-975x683.jpg

Ukame USA

Drought-takes-toll-on-crops-across-Midwest-671SJ4A2-x-large.jpg

mahindi yakiwa yamenyauka
jammas.hussain20120719014619623.jpg

Ukame USA

Huu ni wakati wakujipanga kwani Hali haitakuwa nzuri kabisa na Bei ya NAFAKA inatarajiwa kupanda Mara Dufu
 
dah mbona adi nimeogopa huku Mungu atujaalie mvua nyingi ili mazao yawe yakutosha
 
USA ndo wamiliki wakubwa wa viwanda na ukiwambia wapunguze wanaleta siasa. Na Tz itakuwa hivyo maana naona sehemu zilizopakana na mbuka ....mfano huku Ngaramtoni Arusha mvua inatukwepa kwelikweli
 
Hii inaweza kuwa ni fursa nzuri ya kujikita kwenye kilimo, kwani kwa kipindi hiki cha uhaba wa chakula duniani, bei za mazao ya nafaka zitakuwa nzuri (zinalipa sana).
Kilimo cha umwagiliaji ndio haswa chenye uhakika wa kuvuna wakati huu wa upungufu wa mvua.

Mara nyingi dunia ikikumbwa na uhaba wa chakula kama hivi, huwa inachukua miaka miwili mpaka mitatu kwa hali kurudi kuwa kawaida. Katika kipindi chote hicho wakulima wanaomwagilia wanaweza kutoka saaana.

Wadau wa kilimo, tujuzane kuhusu fursa za kupata mitaji (funds) ili tujikite kwenye kilimo katika kipindi hiki cha uhaba wa chakula duniani.
Wadau wa kilimo, tuchangamkieni fursa hii.
Tujuzane, wapi tunaweza kupata mitaji (funds / mikopo, etc) kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Asanteni.
 
Huwa nasikitika sana nikiona hoja kama hizi za muhimu hazipewi kpaumbele na wadau wengi JF. Hili ni tatizo sana, nenda kwenye siasa au MMU, watu wanachangia sana, sikatai kubalance mambo katika maisha ila tusijisahau kwa mambo ya msingi.
 
Hapo umenena mkuu.

Haya wadau wa kilimo hapa JF, tupeane information za wapi tunaweza kupata funds za kilimo cha umwagiliaji ili tutumie fursa hii ya uhaba wa nafaka duniani.
Hii ndio fursa ya kuanza kilimo hiki kwani bei zikiwa nzuri, tunaweza kufanikiwa kurudisha gharama za uanzishaji mashamba, gharama ambazo huwa kubwa sana pale mkulima anapoanza shughuli za kilimo.
Tuchangamke wadau wa kilimo, tujuzane sources mbali mbali za mitaji ya kilimo.
 
Mkuu ni kweli kabisa, Tembelea jukwaa la Siasa na MMU, kule MMU ukinzisha uzi tu kijinga baada ya nusu saa utakuta wachangiaji 100 sasa njoo huku,

Ishu kama hii ni muhimu sana, lakini ndo kama hivyo mkuu, ni kama yalivyo Magazeti ya Udaku, mtaani yanasomwa kama nini, huwezi kuta mtaani mtu ana gazeti la mwanachi akisoma, ni udaku tu habari ziszo kuwa na ishu maishani
 
Ndio maana huwa naangalia watu wanavyoshabikia cdm, bila hata kujadili kwa kina wanamkakati gani wa kukabiliana na matatizo ya wananchi, matokeo yake hata kama chama kingine kikija kuchukua madaraka unaona kama hawafai huenda ikapelekea kuvuruga utulivu wa nchi.
 
mkuu, zungumzia mada husika, umeanza kuharibu hii thread kwa kuzungumzia siasa bila hata kujitambua

haupo makini kabisa
 
Hapo umenena mkuu.

Haya wadau wa kilimo hapa JF, tupeane information za wapi tunaweza kupata funds za kilimo cha umwagiliaji ili tutumie fursa hii ya uhaba wa nafaka duniani.
Hii ndio fursa ya kuanza kilimo hiki kwani bei zikiwa nzuri, tunaweza kufanikiwa kurudisha gharama za uanzishaji mashamba, gharama ambazo huwa kubwa sana pale mkulima anapoanza shughuli za kilimo.
Tuchangamke wadau wa kilimo, tujuzane sources mbali mbali za mitaji ya kilimo.

Haya wadau turudini kwenye hoja ya Mu-israeli.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu unachosema nikweli kabisa, Mimi nishuhuda,kaka yangu anafanya hii biashara ya mazao,yeye hujihusisha zaidi na Mahindi,angalia kwamfano msimu huu,alinunua debe moja( plasti ya lita 20) kwa shilingi elfu 5000 mpaka 5500, sasa anauza debe moja elfu 13000 mpaka 14000 pale Tabora! kwakweli hii fulsa tuitumie,Mazao nibiashara nzuri sana wewe unakuwa unacheza na msimu tu basi! Pia mimi naona kama kulima mwenyewe huwezi unaweza kununua ukaweka stoke kisha unauza baadaye kwafaida kubwa tu! mwaka huu lazima nianze namimi! tuamke wakuu tusitegemee ajira pekee! Biashara/fulsa kama hizi sizakuacha zipite!
 
Sawa kabisa. Ila changamoto ni mitaji ya kuanzisha shughuli zenyewe.
Wapi tunapata funds za kuwekeza kwenye kilimo ?? Hii ndio kikwazo kikubwa.
Mabenki yana masharti magumu sana. Hivyo maka kuna mahala pengine tunaweza kupata mikopo au funds za aina nyingine tujuzane wadau.
Kuna baadhi ya taasisi za kimataifa huwa zinatoa funds za namna hii, tatizo ni kupata information zao.
Tujuzane kuhusu mambo kama haya ya funds za kuwekeza kwenye kilimo.
 
Sawa kabisa. Ila changamoto ni mitaji ya kuanzisha shughuli zenyewe.
Wapi tunapata funds za kuwekeza kwenye kilimo ?? Hii ndio kikwazo kikubwa.
abenki yana masharti magumu sana. Hivyo maka kuna mahala pengine tunaweza kupata mikopo au funds za aina nyingine tujuzane wadau.
Kuna baadhi ya taasisi za kimataifa huwa zinatoa funds za namna hii, tatizo ni kupata information zao.
Tujuzane kuhusu mambo kama haya ya funds za kuwekeza kwenye kilimo.

Unachosema nikweli wengi tunakuwa namatanio yakuingia kwenye hizi fulsa,sasa mtaji ndiyo inakuwa shida! nadhani hili la mabank kutoa mikopo nitatizo pia! mimi Mkuu nimejikusanya walau nianze tu mwaka huu! nakuambia kwamahindi(ambayo walau niaidia fulani) mtaji unadouble kila mwaka!
 
Huwa nasikitika sana nikiona hoja kama hizi za muhimu hazipewi kpaumbele na wadau wengi JF. Hili ni tatizo sana, nenda kwenye siasa au MMU, watu wanachangia sana, sikatai kubalance mambo katika maisha ila tusijisahau kwa mambo ya msingi.

ni kweli kabisa ila sio kila mtu ana interests na mambo ya business.
Mkuu ni kweli kabisa, Tembelea jukwaa la Siasa na MMU, kule MMU ukinzisha uzi tu kijinga baada ya nusu saa utakuta wachangiaji 100 sasa njoo huku,

Ishu kama hii ni muhimu sana, lakini ndo kama hivyo mkuu, ni kama yalivyo Magazeti ya Udaku, mtaani yanasomwa kama nini, huwezi kuta mtaani mtu ana gazeti la mwanachi akisoma, ni udaku tu habari ziszo kuwa na ishu maishani

wewe sijawahi kuona comments zako mmu ila inaelekea unasoma sana kiasi kwamba unajua trend ya threads zinavyochangiwa... kuna uwezekano hata hapa business watu wanasoma sana ila hawapendi kuchangia. mi pia siasa huwa nasoma then napita kimya kimya ila kikubwa ni ujumbe umefika. usilaumu wala usisikitike.
 
Fursa kama hii ya uhaba wa chakula duniani ni muhimu sana kwa wajasiliamali wa Tanzania. Tatizo ni kwamba nafasi kama hizi huwa atuchukui advantage yake wakati zinapojitokeza. Ni muhimu kujipanga haraka nakuweza kuingia kwenye hii biashara ya mazao ya nafaka.
 
Ni sawa kabisa. Sasa tufunguke zaidi kwa kujuzana kuhusu wapi tutapata mitaji (mikopo, funds, n.k) kwa ajili ya kilimo kikubwa.
Tutambue kuwa kilimo kinalipa sana ikiwa kitakuwa ni kilimo kikubwa cha umwagiliaji.
Wana JF, tuambizane kuhusu sources za mitaji ya kilimo kikubwa.
Tuchangamke wana JF.
Kilimo kikubwa kinalipa.
 
Back
Top Bottom