Fursa kama hii ya uhaba wa chakula duniani ni muhimu sana kwa wajasiliamali wa Tanzania. Tatizo ni kwamba nafasi kama hizi huwa atuchukui advantage yake wakati zinapojitokeza. Ni muhimu kujipanga haraka nakuweza kuingia kwenye hii biashara ya mazao ya nafaka.
Nchi letu limejaliwa kuwa na ardhi yenye rutuba na mito mingi isiyokauka lakini kwa bahati mbaya pia tukajaliwa kuwa na viongozi legelege chini ya uongozi wa CCM. Kama serekali ingekuwa na akili nzuri ingewezesha wakulima wengi ambao wako karibu na vyanzo vya maji wakalima kilimo cha umwagiliaji. Kilimo kingewatoa wananchi. Sasa kama nchi kama Marekani inalia ukame sisi tufanyeje? Kutegemea mvua peke yake hakitatutoa!!