KASULI
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 599
- 669
Hii inakuwa used wapi kiongoziiHizo used unaweza kupata kuanzia million 2.5 ziko za Yamaha, Suzuki, Mercury na Honda. Kwa ushauri ni vyema ukachukua Yamaha maana vipuri vinapatika Kwa urahisi na mafundi wengi wanauzoefu nazo.
Injini inafanya vyema kwenye maji yoyote iwe chumvi au baridi watengenezaji wametengeneza ifanye kazi maji yoyote.
Outboard engine maji hupooza injini Kwa kuvutwa na pampu kisha kuzunguka kwenye njia ya maji za injini kisha kurudishwa tena nje hizi hazina rejeta.
Kwa mtumiaji wa baharini inatakiwa awe makini kuhakikisha water impeller (pampu) ni nzima na kila akitoka kutumia anapoitunza atoe kwenye maji na kusafisha na maji Safi maana maji chumvi huwa na tabia ya kuganda hivyo upelekea kusababisha kutu kwenye injini na uharibifu wa injini.