Kwa wadau wa vyombo vya majini, boti ndogo na Jet Ski Kwa ajili ya uvuvi,utalii na michezo

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,945
12,509
Uzi huu ni Kwa ajili ya wadau wa vyombo vya majini Kwa ajili ya shughuli za uvuvi,utalii na michezo.
Mnakaribiahwa Kwa ajili ya namna ya kufanya usajili,Sheria za vyombo vya majini, marekebisho, utunzaji, sehemu za kununua vipuri, changamoto za utumiaji vyombo, sehemu za kuunda boti na kununua injini.

images (4).jpeg

Kwa wale wa boti za mbao za kuchonga hutegemea aina ya mbao atakayo na zinazopatikana.

images (1).jpeg

Boti za fiber kuna za kuagiza nje au kutengeneza hapa hapa nchini, hizi hutumika sana kwenye shughuli za utalii,uvuvi na michezo kulingana na hitaji la mmiliki.

images (2).jpeg

Kwa upande wa injini kuna injini za ndani ya boti(inboard engine) na nje (outboard engine).
Boti injini zake zinatumia mifumo ya propela na jet propulsion.

images (5).jpeg

Kwa wadau wa michezo ya majini kuna Jet Ski (pikipiki maji) hizi zinatumia mfumo wa jet propulsion. Na zipo zinazotumia nishati ya umeme na petrol.
images (3).jpeg

Karibuni Kwa mawazo, maoni, maswali,ushauri, mchango wowote kuhusiana na vyombo vya majini.
 
Boti ndogo ya kutalii yenye Kila kitu inauzwa min tsh ngo..!?

Na je zile cruzi zinauzwaje
Bei inategemea na ukubwa wa hiyo boti (urefu*upana), vitu utakavyo hitaji viwepo Choo,chumba, jiko,friji Kwa upande wa luxury.

Kwa makadirio za kuagiza inabidi uwe na USD 40,000 na kuendelea.

Ila kama upo tayari unaweza kuleta pendekezo/mchoro na vitu utakavyo unaweza ukatutafuta Spabiton Marine, tunatengeneza Fiber Boat za aina zote tupo Dar na Tanga.
 
mnaweza kutengeneza zile mbalawa kubwa kama MV mariamu , MV maua za pale ferry pembezoni gharama zikoje kwa mtu anayetaka kukodishwa kwa mwezi au mwaka?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Tunatengeneza aina yoyote ya boti kadri ya uhitaji wako, pia tunafunga mifumo ya boti kutumia nishati ya jua na mota za umeme kama mbadala wa mafuta.Tunafanya conversion za injini za gari kutumika kwenye boti na kuziwekea marine gearbox na mfumo wa Jet propulsion.

Gharama za kukodisha sijui Kwa wale wa ferry Ila hutegemea aina ya chombo na mashine anayotumia.
 
Kama hizi hapo chini kwenye picha.
Hizo zinatengenezwa kwenye Site yetu ya Mkwaja mkoani Tanga.
Ila ukihitaji tunakuja popote au tunatengeneza na kukufikishia, Dar tupo na site zetu.
IMG-20201023-WA0002.jpg
 
Tunatengeneza aina yoyote ya boti kadri ya uhitaji wako, pia tunafunga mifumo ya boti kutumia nishati ya jua na mota za umeme kama mbadala wa mafuta.Tunafanya conversion za injini za gari kutumika kwenye boti na kuziwekea marine gearbox na mfumo wa Jet propulsion.

Gharama za kukodisha sijui Kwa wale wa ferry Ila hutegemea aina ya chombo na mashine anayotumia.
Asante sana je hapo kwenye mifumo ya boti kwa kutumia nishati ya jua na mota za umeme je inawezekana kuongezea mfumo wa gas kwenye boti kama ya uvuvi kupunguza gharama ya mafuta?
 
Kama hiyo hapo inaweza kutengenezwa kwa mfumo wa fiber na gharama yake inakuwaje mpaka kukamilika.
Ndio inawezekana kutengenezwa mfumo wa fiber. Kwa boti ya urefu wa Mita 6 na upana wa Mita 1.5 fiber boti bila injini ni million 7.

Injini tunakuagizia ukihitaji au ukanunua mwenyewe.
 
yah aina hizo hizo vipi gharama mpaka kukamilika ni kiasi gani? na nikihitaji kwa kukodishwa mambo yanakuwaje?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Fiber boat bila injini unaweza kupata kuanzia million 7, injini wewe utachagua utumie ya mtumba au mpya.

Kama utafanya biashara ya kukodisha itabidi uonane na watu pale Kivukoni au Msasani. Boti ndogo unaweza ukaikodisha Kwa Masaa au Kwa siku. Kama utaikodisha Kwa watalii bei huwa mpaka laki 2 Kwa siku.
 
Ndio inawezekana kutengenezwa mfumo wa fiber. Kwa boti ya urefu wa Mita 6 na upana wa Mita 1.5 fiber boti bila injini ni million 7.

Injini tunakuagizia ukihitaji au ukanunua mwenyewe.
Asante sana kwa ufafanuzi mzuri kuna zile boti za mbao zinapatikana mwambao wa Ziwa Tanzanyika sijui zinakuwa na urefu na upana wa mita ngapi maana nilikua nataka kujua kwa ukubwa ule gharama inakuaje kwa mfumo wa fiber?
 
Boti kama zile pia ukitengeza inabadilishwa kuwa fiber bei inategemea ukubwa wa boti.
 
1.1 Hizi outboard motor horse power 9.9, na 15 used ni bei ganii..? Zipo kampuni gani..??
1.2. Je, ni kweli hizi injini za maji chumvi hazifai maji baridii
 
Uzi huu ni Kwa ajili ya wadau wa vyombo vya majini Kwa ajili ya shughuli za uvuvi,utalii na michezo.
Mnakaribiahwa Kwa ajili ya namna ya kufanya usajili,Sheria za vyombo vya majini, marekebisho, utunzaji, sehemu za kununua vipuri, changamoto za utumiaji vyombo, sehemu za kuunda boti na kununua injini.

View attachment 1637202

Kwa wale wa boti za mbao za kuchonga hutegemea aina ya mbao atakayo na zinazopatikana.

View attachment 1637167

Boti za fiber kuna za kuagiza nje au kutengeneza hapa hapa nchini, hizi hutumika sana kwenye shughuli za utalii,uvuvi na michezo kulingana na hitaji la mmiliki.

View attachment 1637190

Kwa upande wa injini kuna injini za ndani ya boti(inboard engine) na nje (outboard engine).
Boti injini zake zinatumia mifumo ya propela na jet propulsion.

View attachment 1637192

Kwa wadau wa michezo ya majini kuna Jet Ski (pikipiki maji) hizi zinatumia mfumo wa jet propulsion. Na zipo zinazotumia nishati ya umeme na petrol.
View attachment 1637191
Karibuni Kwa mawazo, maoni, maswali,ushauri, mchango wowote kuhusiana na vyombo vya majini.
Mkuu weka mawasiliano nataka mnitegenezee ya kufanyia utalii (binafsi lakini), iwe na sebure, chumba, jiko, choo, min bar etc, je mnaweza tengeneza?
 
1.1 Hizi outboard motor horse power 9.9, na 15 used ni bei ganii..? Zipo kampuni gani..??
1.2. Je, ni kweli hizi injini za maji chumvi hazifai maji baridii
Hizo used unaweza kupata kuanzia million 2.5 ziko za Yamaha, Suzuki, Mercury na Honda. Kwa ushauri ni vyema ukachukua Yamaha maana vipuri vinapatika Kwa urahisi na mafundi wengi wanauzoefu nazo.

Injini inafanya vyema kwenye maji yoyote iwe chumvi au baridi watengenezaji wametengeneza ifanye kazi maji yoyote.
Outboard engine maji hupooza injini Kwa kuvutwa na pampu kisha kuzunguka kwenye njia ya maji za injini kisha kurudishwa tena nje hizi hazina rejeta.

Kwa mtumiaji wa baharini inatakiwa awe makini kuhakikisha water impeller (pampu) ni nzima na kila akitoka kutumia anapoitunza atoe kwenye maji na kusafisha na maji Safi maana maji chumvi huwa na tabia ya kuganda hivyo upelekea kusababisha kutu kwenye injini na uharibifu wa injini.
 
Back
Top Bottom