Hahhaaaaaaaa!
FP, mbona si wazee tunakazi? Kama mzee mwenzangu kawekewa mpaka
microsoft excel usoni ili aonekana kijana kidogo, mi si ndiyo ndawekewa
Microsoft power point au
microsoft word kabisa?
lakini tukirudi kwenye ukweli baadhi ya wadada wa vyuo siku hizi wamejirahisi mno, na ni kweli wako kipesa kama alivyotanabaisha mdau hapo juu. Nidhamu, utu na heshima zao zimeshuka mno na ndiyo maana baadhi yao wamedirikia hata kuanza kuonekana maeneo fulani fulani wakijiuuza! Hebu fikiria msomi anayetarajiwa kuwa injinia au daktari, au mwanasheria au waziri au mkurugenzi nk leo hii kaanza ukahaba, hivi tutakuwa na taifa lenye viongozi wa aina gani miaka ijayo? Tutakuwa na watu wenye utu kweli au tutakuwa na watu viatu?