Haki zangu ni zaidi ya hizo ulizoorodhesha,Mimi sikuwahi kutumika/wala kutumwa na yeyote.Serikali inakunyima haki ipi mkuu? Ushawahi kuzuiwa kutoka nje ya nyumba yako? ushawahi kuzuiwa kwenda hospital ukapate tiba yako? ushawahi kukatazwa usipande basi au kutembea na gari yako? Ushawahi kukatazwa kula chakula chako? I mean hiyo haki unayozungumzia hapa inahusu zaidi masilahi ya wanasiasa katika harakati zao za kutafuta kupiga hela kupitia vikao vya katiba kama ilivyotokea kwa ile katiba ya mwanzo. Ww kama mwananchi wa kawaida unatumiwa tu kama daraja na wanasiasa hao ili wafikie malengo yao. Ila swala la kunyimwa haki raia kama raia halina mashiko.
Ninapohitaji Katiba Mpya in kukataa hii chakavu ambayo inatumiwa na wanasiasa walafi wa CCM kujimilikisha kila kitu na kuidumaza Tanzania kiuchumi.
Hatuendelei kwa sababu licha ya kuwa na watu wa kutosha na ardhi yenye kila kitu tumekosa siasa safi na uongozi bora mikononi mwa TANU&ASP na baadaye CCM.