Gift mzalendo
JF-Expert Member
- Dec 13, 2019
- 1,033
- 1,227
Habarini wakuu,
Kwanza nipongeze juhudi mbalimbali za taifa letu katika kujikomboa kiuchumi. Niwapongeze pia vijana wenzangu tuliomua kujiajiri kwa njia mbalimbali Machinga mama lishe boda boda nk.
Nirudi kwenye mada yangu , katika kutafakari kwangu nimejaribu kuangalia Mambo muhimu yanayofanya uchumi wa nchi kuwa imara. Yapo mengi isipokuwa
Moja ya Jambo muhimu ni uimara wa sekta binafsi haswa katika suala la uzalishaji na kuajiri. Kiuhalisia hakuna serikali duniani inayoweza kuajiri watu wake wote, isipokuwa kazi kubwa ya serikali makini Ni kutengeneza mazingira mazuri kwa sekta binafsi kuajiri na kuzalisha zaidi.
Tunapokuwa na sekta binafsi imara kiuchumi pia tunakuwa na taifa imara na serikali imara kiuchumi. Tukumbuke serikali inajiendesha kutoka kwenye Kodi inazozikusanya kutoka kwenye sekta binafsi rasmi na zilizofanikiwa. Lakini ili kupata sekta binafsi zilizofanikiwa na imara lazima zitengenezewe mazingira mazuri na mifumo mizuri. So Kama tutaendelea kutengeneza mazingira ya kuwa na sekta binafsi zisizorasmi , tusitegemee ukuaji mzuri na imara wa kiuchumi.
Wakati huo huo tutakuwa tunaongeza mzigo mkubwa kwa watumiaji wa mwisho (consumer). Bidhaa moja inafa yiwa biashara na watu wengi zaidi na Kila mmoja anataka apate faida mwisho mtumiaji wa mwisho ndo atalipia faida ya mzalishaji, Kodi ya bandari, muagizaji, muuzaji wa jumla na reja reja, Machinga wa kwanza wa pili nk. Kwa hiyo mlolongo wote huo mlaji au mtumiaji inabidi azibebe.
Kwa ishu ya Machinga na mama lishe inatakiwa iwe ni mpango was muda mfupi huku tukiandaa mpango wa kuwaaandaa ili waweze kuingia kwenye mfumo was sekta binafsi rasmi , ambazo zinaweza kuwasaidia na kusaidia uchumi wetu. Niseme tu hili suala limetazamwa kisiasa zaidi kuliko kiuchumi. Siamini Kama Kuna mtu anatamani azungushe bidhaa juani , wakati huo hana uhakika was soko.
Tunahitaji kuandaa vijana waweze kuanzisha biashara ambazo ziko kwenye mifumo. Tumekuwa na biashara ambazo zinaanzishw a na zinakufa pindi mmliki akifa kutokana kutokua kwenye mifumo inayoeleweka. Mifumo imara za biashara katika sekta binafsi Ni moja nguzo imara katika uchumi endelevu.
Moja ya uimara wa uchumi wa nchi Kama marekani ni kuanzishwa kwa makampuni mengi katika sekta binafsi. Tunatamani tuone vijana wetu machinga wanaunganishwa na wanaandaliwa kuanzisha makampuni ya kutengeneza kusambaza bidhaa mbalimbali
Mama ntilie nao wanaandaliwa wanaunganishwa kuanzisha migahawa mizuri. Biashara huria inasaidia uchumi lakini biashara holela itazidi kuua uchumi.
Suala la kuruhusu Machinga na mama lishe kujaa kwenye majiji na miji yetu pasipo mpangilio maalum na bila future inayoeleweka , lisi we Ni la mpango wakudumu Bali liwe la mpito. Tukiwandaa kuingia kwenye mifumo rasmi ya biashara. Na siku moja biashara zote zikae kwenye mifumo.
Na majiji yetu yabaki kuwa majiji yenye mpangilio mzuri yaliyosayarabika.
Hayo ni maoni yangu.
Karibuni