KUZALIWA KWA NYOTA.
Kabla ya nyota kuzaliwa inaanza kama sayari ya kawaida wakati vumbi na hewa (sana sana hydrogen) ikijikusanya. Kadri hii hewa na vumbi vinavyoongezeka basi gravity nayo pia inaongezeka. Tukichukulia ukubwa/uzito wa jua letu kama kiwango (solar-mass) basi mkusanyiko wowote ule wa vumbi na hewa chini ya 0.013 solar-mass (1.3% ukubwa wa jua letu) hiyo itakuwa ni sayari (planet) tu. Kuanzia ukubwa wa 0.08 solar-mass na kuendelea gravity inakuwa kubwa sana (kilo moja hapa duniani ukiipeleka huko itakuwa na uzito wa kilo bilioni 100 na zaidi). Huu mgandamizo mkubwa wa gravity unafanya joto kupanda zaidi ya nyuzi milioni 15 celcius. Hili joto na mgandamizo wa gravity ndio kibiriti kinachofanya hydrogen ichanganyike ketengeneza helium na kutoa nguvu hizi za nyuklia (fusion). Hivi ndio jua linavyozaliwa.
Nyota zinakufaje?
Maisha ya nyota yanategemea sana na ukubwa wake. Nyota ndogo zinaishi muda mrefu sana (zinachoma hydrogen yake taratibu taratibu) kuliko nyota kubwa. Kwa mfano, nyota ndogo kama jua letu inategemewa kuwaka kwa miaka bilioni 10 wakati nyota kubwa sana kamaBetelgeuse zinategemewa kuwaka kwa miaka million 10 tu.
Wakati nyota inawaka kunakuwa na uwiano (equilibrium)wa nguvu ya gravity na nyuklia. Gravity inakandamiza chini wakati milipuko ya nyuklia inasukuma vitu nje. Uwiano huu unaendelea hata baada ya hydrogen ikiisha. Baada ya hydrogen kuisha helium nayo italipuka kinyuklia kutengeneza Carbon na Oxygen. Baadae carbon nayo italipuka kunyuklia kutengeneza iron (chuma). Mara tu nyota inapoanza kutengeneza chuma (iron), mchezo umekwisha. Chuma ni kama maji yanayouzima huu mlipuko wa nyuklia mara moja. Milipuko ya nyuklia ikiacha, ule uwiano (equilibrium) wa gravity na nyukilia unakuwa haupo tena na gravity inashinda. Kila kitu huanguka chini na mlipuko mkubwa sana wa mwisho hutokea na mwanga mkubwa sana (super nova) huonekana.
Vitu viwili vinatokea wakati wa hii super nova. Kwanza, madini nzito zaidi ya chuma (iron) yanatengenezwa kama vile dhahabu, urani, nk. Hii ndio maana dunia yetu pamoja na sisi tunaitwa vumbi la nyota (star dust) kwa saababu kama hizi super nova zisingetokea basi dunia yetu na sisi tusingekuwepo. La pili linaliotokea baada ya kishindo (collapse) ni kuwacha tumba (core) ndogo sana lakini yenye uzito (density) mkubwa wa ajabu. Hii tumba ndio ijulikanayo kama BLACK HOLE.
(For correctness sake, not all stars die and turn into black holes. For instance, our sun is too small to turn into a black hole. When it dies it will collapse into a dense core with properties nowhere close to those of black holes)
Black holes na makaburi ya nyota.
Black holes zinazotokea baada ya nyota kubwa sana (super massive stars) ku-collapse ni vitu vya ajabu sana. Chupa moja ya bia (ujazo wa 0.5 lita) ya hii black-hole ina uzito wa zaidi ya tani 3,000,000,000,000. Gravity inayotokana na hizi black holes ni kubwa kiasi ya kumeza kitu chochote kile (majua, sayari, nk) kinachoikaribia. Hii gravity ni kubwa kiasi cha kumeza hata mwanga (even light cannot escape it) na ndio maana zinaitwa BLACKHOLE kwa sababu hazionekani (mwanga pia unamezwa). Kuwepo wa black hole kunajulikana tu kwa vitu inavyovimeza au vinavyo izunguuka. Usiku ukitoka nje angalia juu. Ukiona ukanda wa nyota nyingi basi huo ndio mkusanyiko wetu wa nyota (Galaxy yetu) unaoitwa MILKYWAY. Katikati ya hii galaxy yetu lipo hili black hole moja ambalo jua letu na nyota nyingine zote zilizopo kwenye hii galaxy yetu zinalizunguuka. Ukitaka kujua hii blackhole yetu iko wapi angalia juu na kama unaijua constellation ya Virgo basi usawa huo ndipo lilipo.
Natumaini hii itasaidia pa kuanzia katika kuzijua nyota.
Sasa tuanze na Big Bang Theory.
Hii ni dhana inayosema kuwa mwanzo kabisa hakukuwa na kitu chochote isipokuwa nishatiiliyokuwa sehemu moja ndogo sana (singularity). Ile nishati ililipuka (big bang -hakuna anaejua kwa nini ililipuka) na kwa kupitia nyenzo ziitwazo Higg's Boson hii nishati ilibadilika na kuwa element nyepesi sana ambayo ni hewa ya hydrogen. Hii hydrogen ilijikusanya kwa wingi na gravity ilipokuwa kubwa hydrogen ili-fuse kutengeneza helium katika mlipuko wa nyuklia (fusion) kama nilivyoainisha hapo awali.
Tatizo ni kuwa hii nyuklia fusion inaweza kutengeneza helium, carbon, oxygen na elements nyingine ambazo ni nyepesi kuliko iron (chuma). Chuma kikianza kutengenezwa tu basi hiyo nyuklia reaction inasimama. Kwa hiyo madini kama zinc, tin, gold, nk. ambazo ni muhimu mwilini mwetu na pia kwa matumizi mengine hizi hutengengenezeka tu wakati wa mlipuko wa supernova.
Baada ya supanova kutokea, tumba (core) inakuwa blackhole na vumbi vumbi lililosambaa linajikusanya makundi makundi na kutengeneza sayari kama dunia yetu.