Kwa picha: Ufahamu kuhusu Ulimwengu

Kwa picha: Ufahamu kuhusu Ulimwengu

elimu ya science ya ulimwengu ni elimu ya kusadikika haina ukweli wowote wala haiingii akilini kama tutakuwa na uwezo wa kufikiri,binadamu hatuwezi kuishi kwenye dunia yenye shepu ya chungwa,na kama ingekuwa kweli tungekuwa tunaweza kuishi kwenye milima mikubwa kwa kuganda pembezoni mwa milima bila ya kuanguka.

dunia haiwezi kuwa duara na maji kuganda nje ya dongo la dunia na kisha iwe inaruka angani kwa speed na masafa tunayoambiwa hii haiwezekani kabisa,katika uhalisi wa maji hayawezi kupinda kufata umbo la nje la kitu chochote,maji popote yalipo ni lazima yawe level hio ndio sifa kuu ya maji,na ndio mana tunatumia lever za maji kujengea majumba ili kupata usawa wa nyumba

jua na mwezi ni vitu vipo sawa sawa na umbali wake kutoka ardhini ni sawa sawa kama tunavyoviona,pia kama utaangalia jua na mwezi utakuta vipo ndani ya wingu la blue havipo umbali wanaosema,pia mwezi hauna ardhi ya watu kwenda kutua,tukiwa hapa tunauona kuwa mwezi ni kitu kinapitisha mwangaza(transparent),utazame mwezi mchana utaliona wingu la buluu kwenye mwezi na usiku utaona wingu jeusi kupitia kwenye mwezi.

tumefundishwa gravity ndio inayotuzuia tusipeperushwe na speed ya dunia hiki ni kichekesho kikubwa,kwanini gravity haiwezi kuzuia mabofu na mifuko ya plastic na ni vyepesi sana, kwa ufupi hakuna gravity ni vitu vizito vinabaki ardhini na vyepesi vinakwenda angani

hatuwezi kufahamu kila kitu lakini upo uwezekano kuwa ukubwa wa dunia ndio hauna mwisho(infinity) wala sio duara na haizunguki wala kuruka,uhalisi ni kama tunavyoona kila siku dunia ipo tuli imetulia.
akili yako fupii sana
 
Waafrika tumebarikiwa anga, anga yetu ni moja ya baraka,inawatia wivu astronomers wa ulaya na marekani,anga letu usiku ni safi sana unaiona milkyway bila light pollution wala vumbi vumbi la viwanda vizito.kuna watalii huwa wanakuja afrika kwa ajili ya unajimu tu.
 
images (4).jpg
 
Hapa unaweza kuiona milkyway na Andromeda kutoka Afrika hii ni baraka ambayo hatuitumii.
images (5).jpg
 
Hizi picha zinatupa matumaini makubwa ya uwepo wa viumbe zaidi katika galaxy ya milky way,swali ni je?viumbe hao ni kama sisi au ni wanyama pori tu ambao akili yao ni kuwinda na kula tu kama walivyokuwa madinosaurs.
 
Uwezekano wa kuwepo viumbe wengine kwenye matrilion ya ma terrestrial planets yanayozunguka matrilion ya nyota kwenye mabilion ya galaxies upo
 
Ndani ya milky way peke yake kuna uwezekano wa kuwepo mamilioni ya viumbe,lakini swali linabaki je ni viumbe wenye akili kutuzidi sisi au ni viluilui tu.na kama ni viumbe wenye akili kutuzidi sisi ni kwanini wasiwe wadadisi wa kututafuta?au na wao kinachowasumbua ni umbali?au wako njiani.na ikitokea je watakuwa viumbe rafiki au wanaweza kutufanya watumwa wao.
 

Hebu angalia wanadamu hapa hapa duniani wanapokutana kwa mara ya kwanza,inaonyesha tahadhari ni kitu natural, sasa siku mwanadamu akikutana na viumbe asiowajua itakuwaje.
 

Hebu angalia wanadamu hapa hapa duniani wanapokutana kwa mara ya kwanza,inaonyesha tahadhari ni kitu natural, sasa siku mwanadamu akikutana na viumbe asiowajua itakuwaje.

Kule AREA 51 NEVADA YASEMEKANA WAPO WALE ALIENS, KUNA UKWELI KUHUSU HILO ILA KM INAFICHWA KUNA TAARIFA NYINGI SANA KUHUSU VIUMBE HAWA. WENYE UKWELI KAMILI KUHUSU NI SERIKALI YA MAREKENI, WAO WAMEENDA MBALI MPAK KUWEKEANA MKATABA NA VIUMBE HAO.

NI AJABU SANA JUU YA HILI NA USIRI MKUBWA SANA KWANI KUNA MPK AINA FULANI YA NDEGE ZA KIVITA ZA MAREKAN INASEMEKANA WAMEIGA KUTOKA KWA HAO ALIENS.

KADRI SIKU ZINAVYOENDA TUTAZIDI KUYAJUA MENGI ZAIDI, JUU VIUMBE KUTOKA MBALI
 
UTALII WA ANGA ZA USIKU NCHINI TANZANIA

Utalii wa anga ni mwenendo mpya unaofanywa na watalii wa nchi za ulaya magharibi wanaokosa fursa ya kuona nyota kwa uwazi zaidi nchini kwao kutokana na taa na mwanga mkali unatumika katika miji yao. Taa na mwanga huo husababisha anga kuwa angavu zaidi wakati wa usiku na kuficha mwanga hafifu wa nyota. Kwa hiyo ni vigumu sana kuona nyota nyingi sehemu ambapo kuna mwanga mwingi. Mwanga na taa zisio za lazima huchafua mazingira yetu kwa mwanga mwingi mno unaodhuru na kutatanisha binadamu na viumbe vingine. Uchafuzi huu wa mazingira huitwa uchafuzi mwanga (light pollution)

Nchini Tanzania bado kuna maeneo makubwa yenye anga za kiza zaidi kwa sababu maeneo mengi hayana wakazi wengi wa mjini. Hii ni kweli katika Hifadhi za Taifa na maeneo tengefu yanayo hifadhiwa kwa ajili ya wanyama pori. Bahati nzuri hii inamaanisha kuwa tunahifadhi kiza katika mbuga zetu na hivyo pia kuzilinda dhidi ya uchafuzi mwanga.

Hata katika maeneo makubwa ya mijini kama vile Dar-es-salaam, usiku ni kiza kiasi cha kutuwezesha kuona nyota nyingi angani. Kati ya takribani nyota 3,000 ambazo mtu anaweza kuziona kwenye maeneo ya kiza sana, katika maeneo ya mjini tunaweza kuona kiasi cha nyota angavu sana 300 tu. Hizi zinatosha kukuwezesha kutambua makundi (constellations) maarufu na mawingu-nyota (nebulae).

Ingawa mbingu za kiza zinaweza kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wa kizungu, sisi wenyewe tunaelekea kutojali uzuri wa anga zetu wakati wa usiku. Wakati watalii wa anga huhitaji kwenda mbali sana na kwao, sisi tunaweza kutoka tu nje ya nyumba zetu na kufurahia uzuri wa anga linalotuzunguka.

Si hayo tu. Wakati inakulazimu kufunga safari za mbali kutalii miji mbali mbali Duniani, mbingu zinatufuata pale pale tulipo. Nyota mbinguni zinasogea polepole kiasi kwamba katika usiku mmoja tunaweza kuona mbingu yote inayozunguka Dunia yetu. Hii ni kwa sababu Dunia yetu inazunguka katika mhimili wake kila masaa 24 . Pia, ukiangalia tu anga kwa saa maalum kila siku, kwa mfano saa mbili usiku, katika mwaka mmoja utaweza kuona mbingu yote inayotuzunguka. Hii ni kwa sababu mwelekeo wetu wa kuangalia anga hubadilika pole pole kila siku kwa vile Dunia inaizunguka JUA mara moja kila mwaka.

Kwa hiyo badala ya kutumia fedha kwenda kuona sehemu mbalimbali za mbingu, sisi nchini Tanzania tunaweza kutoka nje ya nyumba zetu tu na kuangalia nyota zote mbinguni kwa kuziangalia nyakati mbalimbali za usiku au saa hiyo hiyo ya usiku kwa nyakati tofauti za mwaka. Kwa hiyo ondoka kwenye luninga yako, au klabu za starehe mbali na kinywaji chako, au hata nje ya ofisi yako kwa wale wanaofanya kazi hadi usiku, na toka nje na kuwa mtalii wa anga kwa kuzifanya nyota kukujia. Unacho takiwa ni kuinua kichwa chako kuangalia juu au kulala mkekani ukiangalia mbingu kwa utulivu. Ukitumia darubini utaongeza burudani yako maradufu.
 
Mwezi huu wa Februari utaona nyota na sayari za kuvutia zifuatazo mbinguni.

MWEZI huonekana kwa uraihisi sana mbinguni. Takribani MWEZI unaonekana vizuri zaidi unapokuwa nusu, yaani kati ya MWEZI mchanga, Februari 22 na MWEZI mpevu Machi 8. Kwa hiyo tarehe zinazofaa zaidi kuangalia MWEZI ni mwishoni mwa Februari.

Mwaka huu Februari ni mwezi wa kipekee kwa sababu, katika nusu ya kwanza ya usiku, unaweza kuona sayari zote zinazoweza kuonekana kwa macho matupu. Siku za mwisho za Februari zitakuwezesha pia kuangalia sayari mbili angavu sana katika anga ya magharibi. Sayari hizo ni ZUHURA (Venus) na SUMBULA (Jupiter) zinazong’ara vikali kuanzia JUA kuchwa kwa JUA hadi saa 3:00 usiku. Kati ya tarehe 25 na 27 Februari, MWEZI Mwandamo utaungana na sayari hizo mbili. Kwa kutumia darubini ya wastani, ZUHURA inaweza kuonekana kama kizio (nusu duara), wakati SUMBULA itaonekana na miezi yake midogo minne na tepe mbili ya mwingu sambamba na ikweta.

Sayari nyingine inanyong’ara sana itakayoonekana mwezi huu ilichomoza upande wa mashariki kabla ya saa 2 usiku na inaonekana usiku kucha ikikatiza anga kuelekea upande wa magharibi kadiri usiku unavyoendelea. Sayari hii ni MIRIHI (Mars) inayong’ara na kuonekana nyekundu. Itang’ara zaidi tarehe 5 Machi wakati itakapochomoza mkabala na JUA linalotua. Mng’aro huu unatokana na mwanga ulioakisiwa kutoka sura ya sayari hiyo ambao tunaona kuwa ni mwanga mwekundu. Kwa kutumia darubini nzuri, utaweza kuona sura yake nyekundu na utandao mweupe wa theluji nchani. Anagani tarehe 7 Machi, MWEZI mpevu utakuwa karibu sana na MIRIHI.

Tarehe 29 Februari ambayo ni siku ya mwisho ya mwezi mrefu, utaona angani sayari nne na MWEZI zimejipanga mbinguni kutoka magharibi kuelekea mashariki. Siku hiyo mara baada ya JUA kuchwa mnamo saa1:00 usiku, angalia Zebaki (Mereury) kwenye upeo wa magharibi, ikiwa na ZUHURA inayong’ara juu yake, kiasi cha nyuzi 30 kutoka kwenye upeo, na kufuatiwa na SUMBULA inayong’ara nyuzi 40 mbinguni na juu yake zaidi utaona nusu MWEZI kwenye mwinuko wa nyuzi 50 juu ya upeo. Zote hizi zimejipanga kwenye mstari unaoitwa njia ya sayari (ecliptic). Ni kwenya njia hii tu ndipo unaweza kuona vitu vyote vilivyo katika Mfumo wa JUA; kama vile MWEZI, JUA na sayari zote, kwa sababu vitu vyote katika Mfumo wa JUA vimepangwa katika bapa moja. Kama unafuata mstari uliyoundwa na ZEBAKI (Mercury), ZUHURA, SUMBULA na MWEZI angani na kuuendeleza hadi upande wa pili, yaani mashariki, utaona kwamba MIRIHI inayachomoza upande wa mashariki pia ipo katika mstari huu huu.
 
Sayari ya mwisho ya kuweza kuonekana ni ZOHALI (Saturn), inachomoza mnamo saa 4:00 usiku ambao bado ni muda muafaka wa kufurahia kuangalia sayari hii. Kwa vile sayari hii haing’ari sana imejificha kati ya nyota zingine jirani yake. Ukilinganisha mng’aro wa nyota za kawaida zinazomeremeta, mwanga wa sayari haumeremeti. ZOHALI ni sayari ya kufuraisha sana kuiangalia katika darubini kutokana na seti yake ya pete bapa vinavyoizunguka sayari hiyo. Ni miongoni mwa vitu vya kuvutia sana unavyoweza kuviona kwenye darubini.

Mkondo wa Nyota (Miliky Way) linakatiza katikati ya mbingu kutoka kusini-mashariki kuelekea kaskazini-magharibi makundi ya nyota yaliyopo ndani ya njia ya kundi la nyota ni CANIS MAJOR lenye nyota yake kali kuliko zote, iitwayo Sirius, MWINDAJI (ORION) yenye nyota nyingi, NG’OMBE (TAURUS) yenye kundi lake la nyota Hyades na Pleiades; PERSEUS yenye kundi maarufu la mfumo wa nyota liitwalo ANDROMEDA, na mwisho ni kundi lenye umbo la “W” la CASSIOPEIA, lililoko kaskazini. Kinachongezeka mwezi huu ni MSALABA BANDIA (FALSE CROSS), ni umbo linalofanana kwa karibu sana na msalaba wa kusini (Southern Cross), lakini mstari mlalo wake hauelekei kusini. Tafuta kundi la MSALABA BANDIA baada ya saa 3:00 usiku ukichomoza upande wa kusini-mashariki. SIMBO (Leo), inachomoza kichwa chake upande wa mashariki mnamo saa 2:00 usiku na kuweza kutambuliwa kwa urahisi mnamo saa 3:30 usiku.

Nyota tano miongoni mwa nyota angavu sana kumi zinaweza kutambuliwa angani. Ya kwanza kati ya hizo ni, nyota angavu zaidi kuliko zote, Sirius, ikiifuatiwa na Canopus, ambayo ni ya pili kwa kung’ara, inayoonekana upande wa kusini. Rigel imo kwenye kundi la MWINDAJI, na Procyon iko upande wa mashariki. Achernar inatua upande wa magharibi na Betelgeuse iko kwenye kundi la MWINDAJI. Nyota mbili Alpha- na Beta- Centauri, ambazo zinatengeneza mstari chini ya MSALABA WA KUSINI, zitaonekana baada ya saa 4:00 usiku.
 
Angalizo pamoja na maelekezo hayo hapo juu,angalau inatakiwa ujue kutambua nyota,sayar husika wakt ukifuatiliamaelekezo ya kutambua mizunguko ya hapo juu.

Tujitahid angalau tulijue hata kidogo kwan kadri siku zinavyoenda Mungu akituma uzima tutayajua mengi sana
 
Back
Top Bottom